Lakini unakuta sometimes mko watu kama watano hivi, kila mtu anaongea, but yeye pekee yake unaonaje mzee wa calculus?Sio tabia nzuri kabisa,ila wengi unakuta hawako interested na hayo mazungumzo au unam-bore sema anashindwa kusema...
hakika wengi ni urimbukeni uliopitiza kwani ndo matokeo ya sms 250-300 au zaidi za BURE BURE kwani ingekuwa kila text unayotuma unalipia kama tulivyokuwa tunafanya kipindi cha nyuma , hakika heshima ingekuwepo, coz hii tabia ya kujifanya uko busy na simu ina kera tena sana, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kutoa machungu yangu dhidi ya tabia hii hasa kwa maduu an mabraza men.
Nawasalimia wana JF, Mambo.
Aise kunatabia moja kweli huwa siipendi.
Unakuta labda mko sehemu fulani mmekaa eidha kwa maongezi au mmetoka out.
Unakuta, mmetoka na mtu yaani yeye yuko busy na simu, anachati tuuuuu haoneshi ushirikiano kama mko pamoja.
Wakati mwingine anacheka peke yake na simu. Yaani hii tabia inanikera sana.
Unakuta sometime mmetoka out malipo unafanya mwenyewe na mko na mazungumzo ya muhimu.
Kwa kweli binafsi hii tabia siipendi kabisa, wakati mwingine mtu unamuheshimu kabisa halafu yuko busy na simu, hivi haya ni maendeleo, usasa, dijitali au kitu gani sasa.
Kuna mtu niliwahi kumuambia "Sio vizuri mkiwa na mtu wewe uko busy na simu" Dah jibu nililo pewa acha tu.
Wana JF hivi mnaionaje hii iko poa au mimi tu.
Nawasilisha hoja.
karibuni
Kwanini usiinuke, huyo hajakuheshimu hata kidogo au you're too boring. Mimi siwezi, naondokaga hata kama namuheshimu labda ni mkubwa, ni kheri kumwambia nitarudi baada when you're free