Hii SMART Partnership ikoje?

Hii SMART Partnership ikoje?

MchunguZI

Platinum Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,048
Reaction score
2,240
Ni mkutano mkubwa tunaoambiwa unaanza hapa TZ lakini naona kumbe si mkutano wa kwanza kufanyika na Tz kushiriki. Ilikuwaje kwamba kwa miaka yote ya nyuma haukusikika kama ilivyo sasa hivi? Tena hapo nyuma umefanyika Uganda na hata hatukuwa na mbinu zozote za kuongeza ushiriki wetu.

Naweka imani kwamba huenda hauna manufaa sana kama inavyojaribu kuonyeshwa na wanasiasa wetu.

Nategemea usiwe na manufaa sana maana si kawaida kwa viongozi wetu afrika (bila ya wazungu) kuendesha mikutano ya manufaa. Hata wakialikana, si rahisi kufika ktk bara hili labda waambiwe watakutana Paris kujadili matatizo ya Kongo.

Lakini kikubwa pia nakiona hapa kwetu. Naona kila mtu anajitokeza TBC kueleza umuhimu wa Smart Partnership. Ni mashindano ya kujionyesha kwamba mimi nahusika na ni muhimu. Naweza kutabiri kwamba hakuna faida tutakayoipata ktk mipango yetu.

Baada ya mkutano huu, wanaoshikilia tenda mbali mbali za mkutano huu watalaumiana kwa kuzulumiana na kutumia pesa vibaya na huenda kutia hasara.

Hata hivyo yupo wa kuendesha mkutano wa mafanikio? Ngoja tusubiri maelezo na hotuba zisizokuwa na umbile la binadamu.

Btw. Kagame anakuja, au ……………….?
 
Back
Top Bottom