"Hii siyo shida?"

"Hii siyo shida?"

Thinker96

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2011
Posts
346
Reaction score
133
Nashukuru Mungu wa Mbinguni, kwa kutufanikisha kufika mwaka huu wa 2026. Ahsante.

Waheshimiwa kitu kinapokuwa adimu ndipo kinapokuwa na thamani na pia kinaondoa migogoro kwa kuwa ni adimu.

Mamlaka ya uongozi hayaruhusiwi kumwazima au mtu mwingine awaye yote kujivika mamlaka ya yako na kuyatumia na wewe ukaacha ni hatari sana. Kwa kuwa yule mwingine kwa kuwa hana nafasi ya kuyajibia pale inapoharibika zaidi ya wewe mwenye nayo hata kama kukuwajibisha utawajibishwa wewe mwenye nayo na si yule aliyeyatumia hata kulaumika utalaumika wewe na kuchukiwa wewe. Na sio yule aliyeyatumia inabidi tujifunze kwa yaliyotokea mafunzo yafike mpaka nafasi ya familia kuwa wewe kama Baba/Mama nafasi yako sio ya kumwazima mtu yeyote yule hasa watoto kwa kudhani unawasaidia. Madhara yake ni makubwa sana kwa wakati ujao maana yakitumika vibaya wa kulaumiwa ni wewe...

Madhara kwa taifa kutokana na watu kujivika nafasi za watu zisizo nafasi zao:-
1) Utekaji umeshamiri ilhali ulikuwepo tokea hata kabla ya uhuru lakini miaka ya hivi karibuni umeshamiri na ilhali kuna kauli zinasubiriwa za kukemea na zitatatoka kwa wakati wake. Suala la kama kukamata inabidi wakati wa yeyote yule kukamatwa washirikishwe wajumbe wa nyumba kumi angalau watu wawili kwa kuwa wakati mwingine huzuka taharuki ya utekaji kumbe ni ukamataji wa polisi wa kawaida na usio wa kawaida.

2) Ubambikiaji wa kesi huu sio yule wa juu ndo anasema mbambikieni ila kwa kuwa watu wamejipa mamlaka wanafanya vitu vinavyomchafua wa juu inabidi likemewe tu na yule wa juu itatosha kabisa kuhusu ushauri wa tume ya haki jiani uzingatiwe.

3)Upendeleo huu kuuelezea naweza inua hisia hasi na sio lengo langu ila upendeleo upo ijulikane hivyo.

4)Saizi kumekuwa na ongezeko la ving'ora na misafara kuliko kipindi chochote kile. Nacho huwa ni kwamba watu wamepata mwanya wa kujigawia mamlaka na kujipachika vinafasi ilmradi mambo yao yaende. Nayo inapandikiza chuki kwa kiwango kikubwa sana kwa kuwa mamlaka sio "scarce" hii hujenga chuki mpaka kwenye vyombo vya ulinzi kwa kuwa moja kwa moja kutakuwa na kauli za "Chukua simu ongea naye", "Unanijua mimi ni nani?" , mzigo wa mkuu na afisa wa chombo akileta fyokofyoko anapishana na ka. Na pia maafisa wa kitengo wamejiweka wazi sana siku hizi ambapo ni hatari kwa usalama wa taifa kwa kuwa idadi yao inaweza kukadirika nadhani mnaelewa zaidi wahusika. Kwa nchi yetu kwa kuwa tupo awamu ya sita na aliyepo hai mstaafu number moja ni mmoja na mawaziri wakuu wastaafu watatu, na wakuu wa vyombo vya usalama,bunge na wengine waliopo kwenye system ving'ora vya viongozi basi nchi nzima si zaidi ya 20, na vingine vibaki kwa fire, ambulance na cash in transit na dharura zingine. Hivyo vingine vipungue kwa kuwa huo mwanya hata waovu huutumia kupitisha uovu wao bila kizuizi ni ushauri tu...
Ninaendelea ila mamlaka ibaki kwa mwenye mamlaka na wengine tuitii mamlaka sio iwe imegawanyika au kuazimwa na wengine yaliyotokea Oktoba.29 hayafurahushi wala hayatasahaulika. Amani ni tunda la Haki tukoke kwenye mjadala wa kati ya yai na kuku nani alitangulia.
 
Back
Top Bottom