Hii siyo Fair Dada zangu tutakuja kuuana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii siyo Fair Dada zangu tutakuja kuuana.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by GAZETI, Apr 6, 2012.

 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni jambo muhimu ambalo litanusuru mambo mengi, kwa siku kadhaa nimekuwa nikimfuatilia dada fulani ambaye kanihakikishia kuwa yuko free, si hivyo tu pia kanihakikishia kuwa yuko tayari kuwa na mimi. Nimejipanga kadri ya uwezo wangu kupeleka barua ndo ananiambia kuwa samahani nimechumbiwa. Baada ya kuchunguza nimegundua ni kweli kachumbiwa na jamaa mmoja ambaye anaishi Dubai toka mwaka jana mwezi wa nne. Huu sio ustaarabu bora kuwa wawazi, ndani ya miezi minne niko na matumaini kumbe najivunia garasa. SI TABIA NZURI kuweni wazi, ona sasa wiki nzima sina raha nashindwa hata kufanya kazi zangu kwa ufanisi.
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Jina la jamaa alikuwa Dubai ni nani tu? Nipe hint naomba ..
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Pole. . .

  Siku nyingine jaribu hata kumchunguza mtu kidogo bila kumshirikisha yeye binafsi.
   
 4. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Yeah man! Yani its about time mtu kushout out! Yani sijui wanakuwa hawana uhakika na wanataka more options? Au unakuta wameudhiwa na wanaatempt kulipiza? Kweli dada zetu acheni kabisa kucheza hii sick game!
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  unahisi umevamiwa??

  Teh teh teh.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  It goes both ways. . .
  Au ndo hufahamu kua wapo wanaume wanaoacha mke na watoto nyumbani alafu wanaenda kudanganya vibinti.kua wanataka ndoa nao? We mwenyewe uliachia moyo kwa rafiki. . .WHY?
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  ndio utie akili......
  ndani ya miezi minne unatangaza ndoa......
  nani alikwambia huwa tunataka kuolewa haraka haraka.....
  au mnadhani huwa na sisi hatuhitaji kuwachunguza.....
  next time usirudie......ni kosa kubwa sana kushobokea ndoa mapema.....
  pole lakini.....itapita utazoea....ndio maisha......
   
 8. serio

  serio JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  poleh.... we learn thru mistakes
   
 9. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Mwehhhh lazima ni double check ati ..
  Huku porini si unajua tena ...
   
 10. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Preta, unamaanisha kuwa miezi minne ni michache. Kwa upeo wangu
  kama umeshindwa kufanya Investigation ndani ya miezi 4 hata miaka
  miwili huwezi pia.
   
 11. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Naomba mnisamehe nashindwa kureply kwa wakati kwani
  huku niliko NETWORK ya Airtel inasumbua. Lakinini niko pamoja
  nanyi katika huu wakati ambao naona umekuwa mgumu ajabu!
   
 12. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ni kweli it goes bothways ila wewe unamaanisha tulifumbie hili jambo macho kwa sababu hiyo? kamwe! huko kwingine mtu atakujaanzisha thread tusubiri, sasa hivi tulijadili lililoko mezani.
  BTW kama umesoma story yangu toka mwanzo sikudanganya na hao wasichana wawili wanajuana, na kila mtu anajua position yake na ya mwenzie in my life!
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  The point is, acha kukandia mmoja as if yeye pekee ndie anaehusika kwenye maswala kama hayo.

  Hehehe. .
  Kila mmoja angekua anajua huyu ambae ndo unamuita mchumba asingejua juzi juzi tu(source thread yako ya vipi akurudishe moyoni) kwamba ulifall kwa rafikiyo. Angekua anajua tangu unaanza kufall hivyo na wewe ndio wale wale. Anza kujirekebisha kabla ya kukandia wengine.
   
 14. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu,ila kama unaona miezi minne ni mingi basi usishangae kwa lililokukuta. Yaani miezi minne tu halafu unaenda kuchumbia???!!!kazi ipo....kumbe ndio maana hizi ndoa hazidumu.
  Bado nimepigwa na butwaa ina maana ndani ya miezi minne umeshamjua vizuri sana na mmeshatumia muda mwingi pamoja hata kulala nae kwa siku kadhaa ujue mkilala na kuamka pamoja inakuaje duuuhhh aiseeee mie nimepitwa na wakati mwenzenu.
   
 15. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ungetaka kumega tu isingekuwa issue (pamoja na kwamba tayari ana mchumba) ila na wewe ulipoonyesha seriousness ya kwenda kwenye next level akaona uta-complicate mambo..
   
 16. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lizzy mpenzi umeamkaje? Hebu nitupie huo uzi naona ulinipita maana naona unampiga marungu mtu hapa....lol
   
 17. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Mbona wewe mgumu wa kuelewa na mwepesi wa kusahau?
  Nasema hata kama it goes both ways, HATUTOLIFUMBIA MACHO HILI LA UPANDE MMOJA. kama wewe unaona upande wa pili nako kuna shida-ANZISHA THREAD YAKO, HATUNA KINYONGO TUTACHANGIA...mwenyewe si unajua mtu anaona kwake vizuri zaidi?

  About me: ingekuwa vyema ukaelewa, KAMA UNGEJUA KILA MTU ALIWAZALO JUU YAKO, YOU WOULDN'T WITHSTAND LIFE.
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahahaha Yummy mwambie akwambie mwenyewe bana sitaki kusutwa.
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ndani ya miezi 4 unapeleka barua! Ningekuwa mimi ningekukatalia hata kama sina mchumba.
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Siona haja ya kufanya hivyo kwasababu sio mhanga. . .Ila nashangaa mtu kama wewe ambae ni wa upande wa pili, ambae ameshashiriki kuingiza wadada wawili chaka akikandia mwenzie kana kwamba yeye ni msafi sana.

  Hehehe. . .I personally au unaongelea generally? Binafsi kwa namna ambavyo nipo straight na watu wengine. . . hamna kinachoweza kunifanya nishindwe kukabiliana na maisha kisa mawazo ya watu wengine juu yangu.
   
Loading...