Hii simu ni pasua kichwa!!

MWAMUNU

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
870
Reaction score
531
Wakuu nina Samsung Galaxy note 4 SM-N910C, balaa la hii simu nimekuwa nikiitumia vizuri tu ila toka juzi ,
Nikiweka laini ya voda hatusikilizani yaani mimi namsikia mwenzangu yeye hanisikii !!
Cha kushangaza nikiweka laini ya Tigo au Airtel tunasikilizana vizuri tu .
Kama kuna mjuzi atupie mautundu hapa maana ishakuwa tabu !!
 
Mkuu nimesha reset mara kadhaa lakini hola !!
 
Naomba ujaribu hii code *#*#4636#*#* kwenye Dialer ya simu yako, (ikikubali) kisha chagua Phone information,, baada ya hapo bonyeza menu ya simu, itakuletea band options weka 'AUTO'

Kingine unatakiwa kujua settings ambazo zipo kwenye Wireless & Network, kuna baadhi ya maeneo mitandao mengine haina 3G (WCDMA) kwa hiyo unashauriwa kuchagua 2G (GSM) only.. au unaweza ukachagua AUTO, ila sikishauri kwa sababu hii itakumalizia chaji ya betri haraka sana.. Tupe feedback kwa msaada zaidi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…