Waterloo
JF-Expert Member
- Nov 30, 2010
- 25,356
- 38,908
Wakuu habari,
Jana katika taarifa ya habari ilitangazwa kuwa tayari fedha bilioni 12.5 zimekabidhiwa kwa mahakama kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za mahakama.
Takribani wiki moja imepita sasa tangu rais atoe maelekezo kwa mhimili wa mahakama kuwa wote waliotuhumiwa kuhusika na ukwepaji kodi washughulikiwe na pesa zipatikane kiasi cha Tsh. Trillion moja.
Naungana na mh.rais katika wazo lake la kuwahukumu wote waliohusika na ukwepaji kodi lakini tujiulize, je, majaji au mahakimu wanaweza kutoa hukumu kinyume na matakwa ya rais?
Tayari rais ameshatoa hukumu kinyume na matakwa ya kisheria.
Nachelea kusema kuwa mhimili wa mahakama kwa sasa umeingiliwa na tayari mahakama haiko huru kushughulikia suala hili.
Rais amepitiliza sana kitendo cha kushawishi majaji kutoa hukumu hakikubaliki katika serikali yoyote inayofuata misingi ya haki za kibinadamu na utawala wa sheria.