Hii sheria ya Mkongo wa baba na mama imetungwa ili kumzuia Katumbi kugombea Urais

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Msitunge sheria zenu kutaka kuzuia Moise Katumbi kugombea Urais
Siku zote mlikuwa kimya baada ya kusikia Moise Katumbi anataka kugombea Urais ndipo wanajifanya kulalamika na sheria zao za kibaguzi eti ili uwe Rais ni lazima uwe mkongomani wa baba na mama, huu ni ubaguzi

Kuwa mkongomani wa baba na mama sio sababu. Mobutu alikuwa mkongo wa baba na mama ni nini alitufanyia Kongo

Kama tupo katika matatizo makubwa ni kwasababu ya hawa wanaoitwa wakongo halisi

Kipindi Moise Katumbi anapambana kumtoa Kabila madarakani wote wanaojiita leo wakongo wa baba na mama si mlikuwa kimya Katumbi pekee yake alipambana na Kabila mpaka kufikia hatua ya kufukuzwa nchini wote mlikuwa kimya

Halafu leo wanakuja kuibuka eti sisi ndo wakongo halisi baada ya kuokota madaraka

Antoine Tshisekedi si alishindwa kumtoa Kabila madarakani yeye mkongo wa baba na mama

Tunachokitaka kwetu ni maendeleo tu huo ukongo wa baba na mama pelekeni kwenye makabila yenu sio kwenye nchi hii
 
Waafrika sisi ni wabaguzi sana na tunabaguana. Ila utasikia waafriak wenzetu waliozamia mbele huku tunataka wawe masenator, wagombee uraisi watambulike serikalini hadi jeshini ila sisi utasikia huyu jamaa si mtanzania baba yake mkimbizi, huyu mhindi.
 
Ya Wacongoman tuwaachie wacongoman.
Wenyewe tuna yetu makubwa zaidi yanatushinda.
 
Laana ya ubaguzi ni mbaya sana, utakuta hata wakongo wenyewe wanabaguana. Hiyo nchi inahitaji akili kubwa bila kujali mtoto wa nani. Mbona Obama mtoto wa baba Africa alifanya vizuri kwa wamarekani. La sivyo mtabaki kupigana miaka mia tano ijayo. Nilijua wakongo mmejivuza kumbe bado.
 
Sio wakongo tu, hii dhana ya baba na mama ni ubaguzi na silaha unaotumiwa na wenye madaraka kuwadhibiti wapinzani wao hii ni kwa Africa kote

Ila ni ujinga sana, maendeleo hailetwi na watu wa asili pekee yao, sisi Africans kwa ujinga wetu hatuoni haya, USA maraisa wengi sio asili pale kwani tunawazidi nn?

Katumbi anafaa DRC ila kwa vile dhambi ya ubaguzi tulio rithishwa na ujinga ujinga hakika watamsumbua sana
 
Luambo MakiadiMsitunge sheria zenu kutaka kuzuia Moise Katumbi kugombea Urais
Siku zote mlikuwa kimya baada ya kusikia Moise Katumbi anataka kugombea Urais ndipo wanajifanya kulalamika na sheria zao za kibaguzi eti ili uwe Rais ni lazima uwe mkongomani wa baba na mama, huu ni ubaguzi

Kuwa mkongomani wa baba na mama sio sababu. Mobutu alikuwa mkongo wa baba na mama ni nini alitufanyia Kongo

Kama tupo katika matatizo makubwa ni kwasababu ya hawa wanaoitwa wakongo halisi

Kipindi Moise Katumbi anapambana kumtoa Kabila madarakani wote wanaojiita leo wakongo wa baba na mama si mlikuwa kimya Katumbi pekee yake alipambana na Kabila mpaka kufikia hatua ya kufukuzwa nchini wote mlikuwa kimya

Halafu leo wanakuja kuibuka eti sisi ndo wakongo halisi baada ya kuokota madaraka

Antoine Tshisekedi si alishindwa kumtoa Kabila madarakani yeye mkongo wa baba na mama

Tunachokitaka kwetu ni maendeleo tu huo ukongo wa baba na mama pelekeni kwenye makabila yenu sio kwenye nchi hii
"Ndeko ya basi yo yo yo. Balingaka basi ya ndeko mibali te", Mpo na nini o yo yo yo. - Franco Luambo Makiadi.

Bandeko ni dada na Ndeko ni kaka hivyo naiweka kaka kwanini wamchukia mke ya kaka yako.
 
Hii kitu imenikumbusha kipindi Salim Ahmed Salim alipotaka kugombea uraisi Tanzania.
 
Back
Top Bottom