Hii picha nimeipenda kwasababu ina ujumbe mkubwa kuweza kuelewa muungano kwa tafsiri ya watanganyika

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Hii picha nimeipenda kwasababu ina ujumbe mkubwa kuweza kuelewa Muungano kwa Tafsiri ya Watanganyika.

Muungano wa april 26, 1964 uliojumuisha nchi mbili huru, Jamuhuri ya Tanganyika na Jamuhuri ya watu wa Zanzibar walipo amua kushirikiana/kuunganisha mambo machache (11).

Baada miaka 53 ya Muungano huu, Tanganyika amebakia kuwa ni dereva huku akiwa amekibeba zanzibar. Huenda kiji Zanizbar hiki kimekuwa ni mzigo mzito kiasi kwamba gari Muungano limekwa kwenye gogo (kero za muungano) haliwezi kusonga mbele wala kurudi nyuma..

Kuulinda Muungano huu kwa nguvu zote ni kuwafanya watanzania kuishi bila furaha kama tunavyoelezwa. .
tmp_17881-FB_IMG_14933150666551962008176.jpg
 
Watu wenye mawazo finyu kama hawa ndio sababu kuu iliyomfanya hayati Baba wa Taifa aogope kuingia kwenye Muungano wa Serikali moja baina ya Tanganyika na Zanzibar maana alijua wazi ya kuwa kuna watu ambao watakuja na mawazo finyu kama haya ambayo yatasababisha Muungano huo kuvunjika.
 
Umaskini ukiisha na kero za Muungano zitapungua otherwise kila upande utaona mwenzie ndio kikwazo
 
Watu wenye mawazo finyu kama hawa ndio sababu kuu iliyomfanya hayati Baba wa Taifa aogope kuingia kwenye Muungano wa Serikali moja baina ya Tanganyika na Zanzibar maana alijua wazi ya kuwa kuna watu ambao watakuja na mawazo finyu kama haya ambayo yatasababisha Muungano huo kuvunjika.
HAKI ndio msingi mkuu wa kuondoa migogoro.
 
Hamna watu hawautaki huu muungano kama wazanzibar..nimekaa hapo kikwajun takriban miaka mitatu lakin sijawah kusikia mzanzibar akiongea lolote zuri katika muungano...haraf wenyew wanaisamin sana oman kuliko hata tanganyika mana wanaona huko ndo kwao sio huku tanganyika
.
.
.
Kyenekyaka nkighanile une
 
Watu wenye mawazo finyu kama hawa ndio sababu kuu iliyomfanya hayati Baba wa Taifa aogope kuingia kwenye Muungano wa Serikali moja baina ya Tanganyika na Zanzibar maana alijua wazi ya kuwa kuna watu ambao watakuja na mawazo finyu kama haya ambayo yatasababisha Muungano huo kuvunjika.

Unaweza ukathibitisha mahali popote Baba wa taifa alipoogopa Muungano wa serikali moja??
Kwa uelewa wangu ni kwamba hakutaka serikali tatu akaanzia serikali mbili lengo likiwa serikali moja
 
Unaweza ukathibitisha mahali popote Baba wa taifa alipoogopa Muungano wa serikali moja??
Kwa uelewa wangu ni kwamba hakutaka serikali tatu akaanzia serikali mbili lengo likiwa serikali moja

Sikiliza hapa maneno ya Baba wa Taifa akiongelea kwa nini alikuwa anauogopa Muungano wa Serikali moja baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Back
Top Bottom