Hii picha inakufundisha nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii picha inakufundisha nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chenge, Oct 31, 2012.

 1. Chenge

  Chenge JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Pichani ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda (wa Kwanza Kushoto) akiwa pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Bwana Christopher Ole Sendeka (Wa pili kushoto), Aliyekuwa Mkuu wa Mikoa Mbalimbali hapa Nchini, Bwana Ditopile Ukiwaona Mzuzuri (wa tatu kushoto) na wa mwanzo upande wa kulia ni Kijana wa Mjini William Vangimembe Lukuvi.

  Picha hii ilipigwa Miaka ya 80 wakati huo Vijana hawa wakiwa ni Viongozi wa Jumuia ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi.


  [​IMG]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akionekana katika Sare zake za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).Picha hii inatajwa kupigwa Mwanzoni mwa Miaka ya 80 wakati huo Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Jeshini.

  [​IMG]
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anne Simamba Makinda katika Kivazi chake na Namna alivyotengeneza nywele zake.Picha hii ilipigwa Mwaka 1994 wakati Mama Anne Semamba Makinda akiwa ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

  [​IMG]
  Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania, Waziri wa Zamani wa Fedha, Mfanyabiashara na Mkulima Mashuhuri, Mchunga Mbuzi aliyebobea, Fundi Viatu aliyepata Elimu kwa Msaada wa Chama cha Ushirika, Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA na Mmoja wa Viongozi Madhubuti wa Taifa hili, Mzee Edwin Mtei.Picha hii ilipigwa Mwezi Aprili Mwaka 1974 wakati Bwana Edwin Mtei alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

  [​IMG]
  Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Maarufu zaidi kama "Rais wa Mbeya", Mwanaharakati wa Utetezi wa Haki za Wanamuziki na Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Kughani wa Kitanzania Bwana Joseph Mbilinyi "Mr 2/Too Proud/Sugu" (Katikati mwenye Kofia) akiwa na Maswahiba zake miaka kadhaa Nyuma.

  [​IMG]
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamaoja na Mwadhama Kardinali Laurean Rugambwa, Picha hii ilipigwa katikati ya miaka ya 90.

  [​IMG]
  Bibi Titi Mohammed. Hii ilipigwa Mwaka 1957 wakati Bibi Titi Mohammed akiwa anahutubia Wananchi katika moja ya mikutano ya Chama cha TANU.

  [​IMG]
  Waziri Mkuu wa Zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr, Salim Ahmed Salim.

  Picha hii ilipigwa Mwaka 1970 wakati Dr. Salim Ahmed Salim akiwa katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kujitambulisha kama Balozi Mpya Mteule wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

  [​IMG]
  Mbaraka Mwinshehe Mwaruka japo Vijana wenzie wa Zamani walipenda kumuita majina Mbalimbali kulingana na Umahiri wake katika Kutunga, kuimba na Kupiga Gitaa akiwa katika Bendi ya Morogoro Jazz mpaka alipounda Bendi yake ya Super Volcano.

  Haijalishi ulizaliwa enzi za uhai wake au baada ya kifo chake, jambo moja ambalo wote tunafanana ni kwamba ukisikia muziki wake sio
  ajabu utatikisa kichwa, kutabasamu, kucheza au kurukaruka.

  Alifariki kwa ajali ya gari Nchini Kenya tarehe 13 Januari mwaka 1979, kifo chake kikichangiwa zaidi na kuvuja damu nyingi na asipatikane wa kumchangia damu ili kuokoa maisha yake pale hospitalini Mombasa.

  Pichani ni Mbaraka Mwinshehe akimvisha Pete ya Ndoa mke wake, Amney Shadad, Hiyo ilikuwa tarehe 17/3/1972 Mjini Morogoro.


  [​IMG]

  Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa anazungumza na Mfalme wa Muziki wa Pop Duniani na Mwanamuziki Mashuhuri wa Marekani, Marehemu Michael Joseph Jackson Ikulu Jijini Dar es salaam. Picha hii ilipigwa Mwaka 1992 wakati Mfalme huyu wa muziki wa Pop wa Marekani, hayati Michael Jackson alipoitembelea Tanzania na kufanya Kitendo cha Kiungwana kwa kufika katika Shule Maalum ya Watoto Yatima na wenye Mtindio wa Ubongo iliyopo Sinza, Jijini Dar es salaam. Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani hadi anakufa 2009, alifika nchini akiwa Balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Balozi Ahmed Hassan Diria.

  [​IMG]
  Meya wa wa Kwanza Mweusi wa Jiji la Dar es salaam, sheikh Amri Abedi Kaluta (wa Nne Kulia) akimtambulisha Mume wa Malikia waUingereza ambaye pia ni Bwana Jumbe wa Edinburg (Duke of Edinburg) Prince Philip (wa Pili kulia Mwenye Sare za Jeshi) kwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania na Kardinali wa Kwanza Mwafrika Duniani, Mwadhama Laurean Rugambwa (wa Kwanza kulia). Pamoja na Kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam Sheikh Amri Abedi Kaluta pia alikuwa Kiongozi Mkubwa wa Kidini wa Waislam hapa Nchini Tanzania.  [​IMG]

  Hii itolee maelezo   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  WALIKUWA HAWAJUI KUWA LEO WANGEKUWA NI CHUKIZO KWA KILA MTANZANIA (isipokuwa kwa wanafiki tu)
   
 3. M

  Masterproud JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 14, 2012
  Messages: 443
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  They were good by then
   
 4. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Picha ya wezi mchana kweupe!
   
 5. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,926
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  INANIFUNDISHA KUA NI WATU WALIOKAWA NA MISSION NA VISION NJEMA KWA SIASA ZA NCHI HII JAPO SASA UFISADI WA BAADHI YA WALAFI WA CHAMA CHAO UMEWAONDOLEA HESHIMA MOJA KWA MOJA KWENYE JAMIII
  PIA INANIFUNDISHA KUA WATU KAMA SLAA NA MBOWE WAMEDANDIA KATIKA VITU AMBAVYO WALA HAWAKUWAHI KUVIFANYA KATIKA MAISHA YAO
  NA KIVYOVYOTE VILE HAWASTAHILI KUFANYWA KUA NI MFANO WA MATUMAINI YA TANZANIA TUITAKAYO
  WAPO WENGI WA KUWAFANYA VIONGOZI WA NCHI HII LAKINI SIO NJAA KALI NA WAZANDIKI KAMA HAWA WAASISI WA M4C YA MZEE MTEI
  :dance:
   
 6. mauro

  mauro Senior Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hilo buti la Mizengo Pinda sijui alitembea kwa miguu tokea sumbawanga hadi dodoma mbona lina vumbi ni kama halijaonja kiwi miaka 2 ?Duh kweli mtoto wa mkulima.
   
 7. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Inatufundisha kuwa ufisadi wa CCM umetoka mbali.
   
 8. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Hivi Pinda amewahi kuwa kijana!!???
   
 9. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,967
  Trophy Points: 280
  Inatufundisha ukiwa kijana lazima uzeeke.
   
 10. charger

  charger JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Inatufundisha kuwa magamba yalikua yanalipa enzi hizo.
   
 11. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,967
  Trophy Points: 280
  Kweli Pinda ametoka mbali!
   
 12. D

  Dopodopo Kadopo Senior Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inatufundisha kuwa mwalimu alikuwa kiumbe dhaifu kama binadamu wengine. Hasa Kama aliweza kufanya kazi na watu wa uwezo huu.
   
 13. C

  CHAKA CHUWA Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli enzi hizo mwalimu alikuwapo ilikuwa ccm ya kweli full nidhamu sio sasa genge la wahuni tu
   
 14. LEARNED BROTHER

  LEARNED BROTHER JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 322
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  hahahahahahaaaa, jibu lako limenifanya nicheke sana, duh!
   
 15. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inanifundisha kuwa shetani wa miaka semanini leo hii ndio waziri mkuu wangu.Majambazi yalianza zamani kupanga ushetani na leo yanatekeleza mikakati hiyo...Mungu yapoteze haya maibilisi
   
 16. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu, nami nimejiuliza sana maana hata hapo alikuwa kakomaa sura ka mtu mzima, ama alikuwa anaogopa kamera?
  Labda Mkuu Chenge atupatie picha ya Pinda akiwa kijana.
   
 17. S

  Shembago JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inatufundisha kumbe kuna KUFA! Dito alikuwepo sasa hatunaye! Hivyo usitoe Roho za watu kwa kutaka madarka jua ipo siku utakufa tu!!
   
 18. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  now i know why uvccm wanauana na kupigana hadharani.
   
 19. bysange

  bysange JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 4,378
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Inanifundisha kuwa mikakati ya ufisadi ilianza kupangwa toka mbali.
   
 20. M

  Msemakweli Daima Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni jambo baya sana kuwa kibaraka, na hasa kibaraka wa kikundi cha watu kinachofuja maslahi ya watu wengi, tunaheshimu historia ya wanasiasa na viongozi wetu walioko kwenye madaraka sasa hivi, lakini hiyo haiwanyimi watu wengine nafasi ya kutoa mawazo yao na kuleta ukombozi, wakati wa ukoloni walikuwepo watu kama wewe ambao walimtukuza mkoloni na kumuona Nyerere na wapiganaji wengine wa TANU hawana maana, tafadhali usiuze uhuru wako kwa makombo unayokula toka kwa mafisadi wachache, heshimu jitihada za ukombozi, na kwa taarifa yako vita ya ukombozi itazidi kukua pamoja na njaa yenu nyinyi vibaraka wachache, TANZANIA NI LAZIMA IKOMBOLEWE.
   
Loading...