WISE 2012
JF-Expert Member
- Mar 13, 2012
- 634
- 460
Tumia dakika chache kufanya uamuzi na siku nyingi kufanya utafiti.Wanaume wengi wanaongoza kwa kuhonga huwa na mkono mfupi wa kuhudumia familia zao pamoja na kuwajali wazazi wao.
Ni kazi rahisi kumkuta mwanaume anakunywa pombe bar ya Tsh 200,000/- kwa usiku mmoja na mama yake mzazi ana pair mbili za kitenge bila kusahau wazazi hawana uwezo hata wa kununua Kg ya nyama,ila ni kazi rahisi sana kumpangia mwanamke kimada chumba na kumnunulia gari kimada wakati familia yako inalalia mihogo ama viporo
Nitajie mtu anayemtolea Mungu fungu la kumi ambaye hana mafanikio katika maisha yake ? Nionyeshe kijana yeyote ambaye huwatumia wazazi wake pesa za matumizi ya nyumbani ambaye hajastawi katika maisha bora na yenye tija ?Kila palipo na baraka ya wazazi pana hazina ya mafanikio daima.
Jitahidi mara nyingi kuwapa wazazi faraja ili wakunenee maneno yenye baraka na hazina ya furaha yako katika maisha yako.Manung'uniko huleta laana katika maisha ya mwandamu na maneno ya baraka huleta mafanikio katika maisha .Ni wakati sahihi wa kuwapa faraja wazazi wetu kwa upendo na asilimia chache ya tukipatacho ili maisha yetu yawe na baraka.
Mama unaweza ukamtumia doti mbili za khanga na akakuombea dua na baraka kwa mwenyezi Mungu ila unaweza kumnunulia kimada wako Iphone 6 na akakuomba tena umnunulie na airtime pamoja na Brazilian Wig,sababu wamejaa laana na ndio wanaovunja ndoa za watu kila uchwao.
Kama upo kwenye ndoa basi hakikisha unapata baraka toka kwa mwanamke bora ambaye ni mkeo sababu yeye ndio kila kitu katika maisha yako kisha unapata baraka za wazazi sababu ndio nguzo bora ya maisha yako.
One of the greatest titles in the world is parent, and one of the biggest blessings in the world is to have parents to call mom and dad