hii ni vita: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hii ni vita:

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by cheusimangala, Mar 29, 2010.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mtoto magath alikatwa mikono na mtu asiejulikana kwa madai kuwa viganja vyake vina michoro ya utajiri,


  Tanzania ni nchi inayojulikana kama moja ya nchi zenye amani na utulivu ulimwenguni,
  ni kweli namshukuru Mungu kwamba hatuna vita ya mabomu wala mitutu ya bunduki lkn nimekaa nikatafakari hasa baada ya kuumia sana roho yangu juu ya unyama aliofanyiwa mtoto Magath nikajikuta nikijiambia kuwa kuna VITA KALI vita mbaya ya IMANI ZA KISHIRIKINA.
  Hii ni vita tuliyoridhi kwani imani hizi tumezaliwa tukazikuta, imani hizi hazijaanza jana lkn kinachonisikitisha pamoja na kwamba elimu imewafikia wengi lkn bado elimu haijasaidia kufuta imani hizi na kasi ya vita hii inayoendelea kumwaga damu nyingi za watanzania inazidi kuongezeka.
  Ushirikina wa tanzania naufananisha na ukoloni,sbb unakuja ktk sura tofauti tofauti,mfano kuna wakati waganga wetu wa kienyeji walidai vichwa vya watu wenye upara vina uwezo wa kumfanya mtu awe tajiri na kama mna kumbuka damu nyingi za watu wa aina hii ilimwagika bila hatia.
  Hivi sasa ni zamu ya kuwawinda Albino,eti viungo vyao vina uwezo wa kumfanya mtu awe tajiri,na sote tunajua ni kiasi gani vita hii imemwaga damu za ndugu zetu hawa na hatujui itaendelea kumwagika kwa kiasi na muda gani.
  Sijasahau jinsi vita hii ilivyomwaga damu nyingi ya wazee waliouliwa eti kwa sababu wana macho mekundu, na waganga wetu walisema watu wenye macho mekundu ni wachawi na kwa vile tunayaamini sana mabo haya tuliwaua bila huruma wazee wetu wenye macho mekundu.
  Nadhani kila mtu ameshaskia kuhusu waganga waliokamatwa na ndoo zilizojaa mafuta ya binadamu waliowaua na kuwabanika kisha kukinga mafuta hayo ili wayatumie ktk shughuli za kishirikina.
  Kuna watanzania wengi sana wamefariki kizembe sbb badala ya kupelekwa /kwenda hospitali waliishia kwa waganga wa kienyeji kwa imani kuwa wamelogwa/kutupiwa jini na mwishowe kufa kumbe wengine walikuwa na malaria tu.
  Kisa cha huyu mtoto ndio kimenisukuma kuandika haya,watu wamemkata huyu malaika mikono yake na kuichukua eti sbb wanaamini inaonesha njia za utajiri,napenda sana watoto na kisa hiki kimeniliza kama niliyefiwa.
  Kutokana na ushirikina wetu kuja ktk sura tofauti tofauti,najihisi kupata hofu sbb najiuliza je ni watu wa aina gani watakaofuatiwa kuwindwa na kuuliwa wakiamika kuwa ni chanzo cha utajiri?
  Kama mtu sio mtanzania atahisi ni vichaa watu wanaoua albino,wazee wenye macho mekundu,au kama huyu mtoto nk lkn sio vichaa ni watanzania wenye akili tmamu na wengine wamesoma.
  Kinachonishangaa ni kwamba,sisi tunaoutafuta utajiri kwa hadi kuwawinda wenzetu kama digidigi na kuwaua kikatili bila huruma mbona ndio nchi maskini ya kutupwa?
  Kwa nini wenzetu walioachana na imani hizi za kishetani nchi zao ni tajiri?
  Sina idadi ya watu waliokufa tanzania kwa sbb ya imani za kishirikina lkn najua ni wengi sana,ukizingatia wengi wao hata magazeti hawaandikwi!
  Hatuwezi kuendelea iwapo watanzania tutaendelea kuutafuta utajiri kwa namna hii.
  Mimi naona hili ni moja ya tatizo kubwa nchini kwetu hivyo kama zinavyofanyika kampeni za kutokomeza malaria au kama zinavyorumika nguvu kuhamasisha kilimo kwanza nadhani ingeanzishwa kampeni ya nguvu itakayosaidia kufuta imani hizi nchini mwetu.
  Asanteni!
   
 2. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Haya mambo ya kishrikiana ni hatari kwani kila siku wanaibua jipya utasikia sijui ukiafanya hivi utakuwa tajiri wakati ni udanganyifu mtupu lakini wanaoniudhi zaidi ni wale wanaodanganyika na huu upuuzi
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  heri mwenye kutafuta mali kwa hekima za ki Mungu, maana hata akipata atakuwa na amani nayo, lipi jema kuwa fukara wa mali uwe rafiki wa Mungu, ama awe na mali nyingi ulizozipata kwa mikono ya shetani na uwe adui wa Mungu, mpenzi mwanajamii tafadhari chukua japo sekunde kufikiri kabla ya kutenda uovu.
   
Loading...