Hii ni Sera ya Mabenki au BOT?

Hii ni Sera ya Mabenki au BOT?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,860
Reaction score
50,626
Mimi sina hata chembe ya ujuzi wa masuala ya kiuchumi, siyajui kabisa,lakini najua kuna sera ambazo huendesha mambo ya mabenki kwenye nchi zote duniani. Na sera hizo hutungwa au hupitishwa na wanasiasa.

Swali langu ni hili: Hapa Tanzania mtu akienda kukopa mkopo binafsi kwenye taasisi za kifedha hukatwa kiasi fulani cha fedha kama gharama za mkopo. Kwa mfano mtu anakopa milioni Ishirini (20,000,000) basi hukatwa hadi shilingi laki sita(600,000) kama gharama za Mkopo. Hivi hii ni sahihi kweli? Benki inaandika imemkopesha Ml. 20 wakati kiuhalisia mkopoji kaondoka na Ml. 19,400,000. Ni haki kutoza Riba kwa kusema unatoza riba kwenye Ml.20 ya mkopo wakati Mkopaji mwenyewe umempa Ml. 19,400,000?. Nataka kujua kama huu ni utaalam wa kibenki au ni sera za kibenki au ni mfumo uliopo kwa kufuata sera za BOT?
 
Navumilia kuwa mtanzaniaa!!!

haya mambo yapo Tanzania ya Magufuli tuu!!!!
 
Tena huo nduo uwizi wa wazi wa mabenki... wanaita GHARAMA za ku process mkopo... WIZIIIII WIZIIIIIIIIIII kila sekta, Magufuli bado anaya tumbua, atafika huko ktk mabenki muda si mrefu
 
Mimi sina hata chembe ya ujuzi wa masuala ya kiuchumi, siyajui kabisa,lakini najua kuna sera ambazo huendesha mambo ya mabenki kwenye nchi zote duniani. Na sera hizo hutungwa au hupitishwa na wanasiasa.

Swali langu ni hili: Hapa Tanzania mtu akienda kukopa mkopo binafsi kwenye taasisi za kifedha hukatwa kiasi fulani cha fedha kama gharama za mkopo. Kwa mfano mtu anakopa milioni Ishirini (20,000,000) basi hukatwa hadi shilingi laki sita(600,000) kama gharama za Mkopo. Hivi hii ni sahihi kweli? Benki inaandika imemkopesha Ml. 20 wakati kiuhalisia mkopoji kaondoka na Ml. 19,400,000. Ni haki kutoza Riba kwa kusema unatoza riba kwenye Ml.20 ya mkopo wakati Mkopaji mwenyewe umempa Ml. 19,400,000?. Nataka kujua kama huu ni utaalam wa kibenki au ni sera za kibenki au ni mfumo uliopo kwa kufuata sera za BOT?

hata mie hili linanichanganya sana, hizo gharama za mkopo ndo inakuwaje hasa? bado hapo afisa mikopo anataka hongo ya milioni moja. jamaa yangu alikopa benki mil 5 akawa anarejesha laki sita ina maana hadi mkopo kukamilika atakuwa amerejesha 7.2 sasa hiyo riba ni 45% sasa bora nikakope saccos au nikachukue mali kauli dukani kwa mangi.

Hapa tunahitaji riba na tozo elekezi kutoka benki kuu.
 
hiyo 600,000tzs iliyokatwa hapo ni insurance/bima ya mkopo. na baada ya hapo utaanza kulipa down payment ya mwanzo kabisa,kwa makubaliano kila mwezi lazma urudishe kiasi fulani kwa muda waliokupangia kama ni miaka 2 au vinginevyo.
 
hiyo 600,000tzs iliyokatwa hapo ni down payment ya mwanzo kabisa,kwa makubaliano kila mwezi lazma urudishe kiasi fulani kwa muda waliokupangia kama ni miaka 2 au vinginevyo.kwa hiyo kwente hiyo mil.20 downpayment ya kila mwezi ni 600,000tzs kwa miezi/miaka mliokubaliana.

down payment sio hiyo mkuu, down payment inakuwa kwenye "hire purchase" mfano unaponunua nyumba au gari, kwenye "personal loan" tunazungumzia hii "loan processing" fee ndo kitu gani?
 
hiyo 600,000tzs iliyokatwa hapo ni insurance/bima ya mkopo. na baada ya hapo utaanza kulipa down payment ya mwanzo kabisa,kwa makubaliano kila mwezi lazma urudishe kiasi fulani kwa muda waliokupangia kama ni miaka 2 au vinginevyo.
Ndugu yangu kuna tofauti kati ya "Loan Down Payment" na "Loan Processing fee" Deni linabakia pale pale na laki sita umekatwa! Unafanyaje hiyo unayoisema "Loan Down Payment" kabla kuutumia mkopo kwa lengo ulilolikusudia?
 
Moja ,sio bank zote zinafanya hivyo,mfano nenda pale finca hakuna kitu kama hicho,hela unayolipia ni only twenty thousands kwaajili ya form, no more cost...
Bima ya mkopo huwa inalipwa na bank sio na mteja, na haikatwi kwenye mkopo ulioomba, so wanaokata hivyo ni wizi
 
Maisha bila kukopa hayaendi,ila kwa Tanzania kiukweli wakopaji wanakumbana na changamoto nyingi.kwa mfano hili la mtu kukatwa hela maarufu km loan processing ili hali ni wajibu wa benki kutoa mkopo kama sehemu ya biashara.hapa ni lazima tukubari kuwa hii ni sera mbaya chini ya BOT.hebu serikali isimamie hili ili kuwakomboa watu wake.
 
Hapo inategemeana na sera ya bank kwa sababu kuna aina za mikopo mbali mbali kuna mikopo unayo lipa principal na interest per month na kuna mikopo ambayo una lipa interest pale unapo chukua mkopo unalipa kabisa interest alafu return ya kila mwenzi unalipa principal tu sasa kama wewe ni loyal customer inabidi kuongea na loans officer kabla huja chukua mkopo ujue ulipaji unakuwaje interest zinakuwaje lakin most of us watanzania tuna chukua mikopo tukiwa na shida kwahiyo ni vigumu sana kuzingatia mambo kama haya lakin muda wa kulipa ndipo tunapo kumbuka vitu kama hiv lakin unapo fanyiwa evaluation ya mkopo vitu bank inavyo zingatia ni profit liquidity credibility of customer sasa. Kwenye profit lazima kuwe na term of repayment na ndo unapata evaluation ya hicho kitu ulicho uliza ni wajibu wa bank officer ku kwambia kabla hajakupa mkopo
 
KABAYAPAITA hapa kuna hii kitu inatwa "Loan Processing fee" wala haina uhusiano na "Interest" kwani bado riba utakatwa na hiyo uliyokatwa haitaingia kwenye hesabu za mkopo unaolipa!
 
Last edited by a moderator:
KABAYAPAITA hapa kuna hii kitu inatwa "Loan Processing fee" wala haina uhusiano na "Interest" kwani bado riba utakatwa na hiyo uliyokatwa haitaingia kwenye hesabu za mkopo unaolipa!

Allen kwa hili leo tuko pamoja, halafu wakati unaomba mkopo hawakwambii haya makandokando utakutana nayo kwenye mkataba tu, kwa kifupi hili ni jipu na gavana asipolitolea ufafanuzi lazima limlipukie tu.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo inakuwa ninloan processing fees kama.vile gharama za wanasheri na huwa haizidi 2% ya pesa unazoomba.
 
Allen kwa hili leo tuko pamoja, halafu wakati unaomba mkopo hawakwambii haya makandokando utakutana nayo kwenye mkataba tu, kwa kifupi hili ni jipu na gavana asipolitolea ufafanuzi lazima limlipukie tu.
Ha! Ha! Ha! Eddy nashukuru kwa kuwa pamoja katika hili. Kukopesha si ndiyo biashara yenyewe ya mabenki, na wafanyakazi mishahara yao si inatokana na riba inayotozwa kwenye mikopo na kwenye uwekezaji mwingine unaofanywa na Benki, kama kwenye ununuzi wa hati fungani za serikali? Sasa hii "Loan Processing fee" kazi yake ni nini hasa na faida yake kwa mkopaji ni nini?
 
Mabenki Tanzania ni wizi mtupu, serikali ya Magufuli iwamulike na hawa jamani tunaumia
 
hata mie hili linanichanganya sana, hizo gharama za mkopo ndo inakuwaje hasa? bado hapo afisa mikopo anataka hongo ya milioni moja. jamaa yangu alikopa benki mil 5 akawa anarejesha laki sita ina maana hadi mkopo kukamilika atakuwa amerejesha 7.2 sasa hiyo riba ni 45% sasa bora nikakope saccos au nikachukue mali kauli dukani kwa mangi.

Hapa tunahitaji riba na tozo elekezi kutoka benki kuu.

Mkuu umezungumza barabara kabisa,hili la riba na tozo elekezi BOT wanalifumbiaga macho sana.
 
Ngoja tuwekane wazi hapa, unapokopa unakatwa gharama za kuprocess huo mkopo, mfano afisa atahitaji kufika kwa mwajiri wako au sehem yako ya makazi na biashara. Hii hujumuisha pia insurance au bima ya mkopo na gharama zingine ndogo ndogo kama wanasheria and so forth.

Funzo, ukihitaji mfano 20million usikope 20m ongeza japo laki 2 yaani kopa 20,200,000 ili upate pesa kamili.
 
Back
Top Bottom