Hii ni sawa au napigwa

Hii ni sawa au napigwa

Ambrose Koller

Senior Member
Joined
Oct 13, 2024
Posts
102
Reaction score
85
Fundi kanitumia hii bajeti ya kuchimba shimo la choo, wataalamu wa ujenzi hii iko sawa?
 

Attachments

  • Screenshot_20250622-200958_Gallery.jpg
    Screenshot_20250622-200958_Gallery.jpg
    158.5 KB · Views: 21
Kama huo mkeka uliandaliwa hiyo tarehe kwenye hicho kikaratasi itabidi u-update!

Gharama lazima zimeongezeka mahali.
 
Daah 😀
Embu muamini fundi wako mkuu acha mambo ya kiwaki, hata akila hapo atakula shingapi?

Hapo inabidi umuilize tena huenda ikatakiwa uongeze pesa.

Quotation yenyewe ya mwaka jana gharama zishapanda dolla imeongeza bei za vifaa haiwezi kubaki vile vile.
 
Kwanini kuna 400,000 kujaza kifusi kwenye nyumba?

Vilevile kujenga tofali 400 kwa 250,000 ni gharama kubwa. Kuchimba shimo la kawaida 180,000 inatosha.

Nondo 15 ni nyingi mno. Shimo la kawaida nondo 5-8 zinatosha, hasahasa kama anachanganya na mesh kama hapo.

Kwa makadirio, shimo halitakiwi kuzidi 1.2 mil gharama zote.
 
Hapo unapigwa mchana kweupe, tafuta angalau mafundi watatu au wanne kila mmoja akafanye tathmini kwa muda wake, kisha wakupe hesabu, hapo utalinganisha sasa, ilq huyo achana nae
 
Unapigwa mkuu, shimo pamoja na kujenga vile visivyojaa haizidi 1.3m
Pitia hii page uone bei na maelezo

 
Gharama ya kujaza kifusi kwenye vyumba vya vyoo uongo

Chumba cha darasa hujazwa kwa TZS. 150K - 250K sembuse vyumba vya vyoo vya size ya kawaida aisee 😂
 
Ni sawa simenti inatakiwa kali ili isipikutike mapema, mimi nilitumia 1.6 m ujenzi kwa kupanga mawe v shape upana juu ni 15ft urefu kwende chini 13ft
 
Fundi kanitumia hii bajeti ya kuchimba shimo la choo, wataalamu wa ujenzi hii iko sawa?
Hapo kipengele kipo kwenye namba 6 na namba 10...lakini kwenye namba 6 kama ananunua lora zima la wire mesh zitabaki nyingi mno! Na kama ananunua kwa elfu 2 kama wanavyouza angenunua Wire mesh pc 5 tu ambayo ni kama elfu 10 tu...Yeye kaandika waya meshi 2 tsh 34000

Na namba 10 kuhusu mbao ya 1*8 inauzwa elfu 6- 8 sio elfi 10! Pengine ni nje ya mji lakini hata huko haiwezi kuwa hivyo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom