Hii ni moja ya njia ya kudumisha mahusiano

Hii ni moja ya njia ya kudumisha mahusiano

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
Habari wanajanvi.

Kuna vitu vingi sana vya kufanya ili kudumisha ama kuhuisha mahusiano, hasa hasa mapenzi na kitu kizuri ni kuwa utatumia ile style huku mjini tunasema "flow with the beats", yaani njia ya kudumisha uhusiano ziko applicable kutokana nanyinyi wenyewe mlivojiweka!

Zawadi,hii ni moja ya tool muhimu sana katika kudumisha mahusiano,mpe zawadi toa zawadi. Hapa katika zawadi kuna ushauri naomba niwape dada zangu, kuna siri ndogo tu kama ukijaribu inaweza kukusaidia.

Kwa kawaida wanaume baadhi, nimesema baadhi tu bila kujalisha kipato, tu wazito wa kununua baadhi ya vitu. Hivi vitu unaweza wewe mdada ukavitumia kuchanga karata zako vizuri kwa kisingizio cha zawadi, kujali na kupenda.

Wanaume wengi tu wagumu wa kununua vitu vifuatavyo kwa matumizi yetu ya nyumbani ama ofisini:

1. Shuka za kujifunika
2. Taulo
3. Mafuta
4. Kiwi
5. Singlet
6. Pichu
7. Saa ya mkononi
8. Kioo cha chumbani
9. Mikoba ya ofisini ama computer
10. Mafuta ya kupaka
11. Computer mouse
13. Neck tye nk

Unachotakiwa kufanya, jaribu kumchunguza yule anaekuhusu, inaweza isiwe vyote hivo hapo juu, lakini akawa na kimoja jipe jukumu la kuhakikisha huyo mtu wako haishiwi nacho.

La muhimu zingatia kuwa, usinunue alimradi umenunua nunua kwa maana halisi ya zawadi kwa mpenzi. mfano kwa mwanaume m'kazi. Mtumiaji wa computer mnunulie mouse ya elfu 50 japo Muhindi alikuonyesha mouse za elfu 5, elfu 10 elfu 20. Usinunue soksi Karume sokoni, pair inauzwa elfu 1 kamnunulie maduka makubwa pair hata 2, lakini za ubora wa juu.

Baada ya muda, utaona matokeo
 
Sijakubali hata kidogo,yaani Computer mouse inauzwa elfu tano,mimi nikanunue ya elfu ya hamsini? Duuh hayo maigizo ya mapenzi sijayakubali hata kidogo,tafakari tena mada yako. Maisha ya sasa ni ya manati halafu bado mtu anajaribu ku-complicate?
 
Juzi wangu nimemuuliza nikupe zawadi gani akanijibu ''Kuwa na wewe tu tayari nimeridhika''....
 
Ukipewa mouse ya 50elfu basi jiandae kuombwa murano. Hakuna free lunch hapa duniani
 
Mkuu jiangalie mouse ya buku kumi si inakutosha?
 
Juzi wangu nimemuuliza nikupe zawadi gani akanijibu ''Kuwa na wewe tu tayari nimeridhika''....

huyo hana lolote zaidi ya kuzuga hakuna asiyependa zawadi mkuu hapo anakibalaguza tu
 
slim5 unataka nikununulie ya elfu hamsini ukachape nayo bakora ofisini??? na mimi utaniletea nini
 
Last edited by a moderator:
Mwee! Hata Ununue Nini Mtu Asieridhika Hata Umpe Zawadi Ya Moyo Wako Kama Umeandikiwa Kupigwa Chini Utapigwa Tuu, FOLLOW YOUR HEART ONLY
 
Nani kasema hayo? Ile kuwa nae tu ni zawadi tosha hakuitaji mouse wala nini.
nikakunulie boxer kwani hajui umuhimu wa kuvaa boxer
 
Sijakubali hata kidogo,yaani Computer mouse inauzwa elfu tano,mimi nikanunue ya elfu ya hamsini? Duuh hayo maigizo ya mapenzi sijayakubali hata kidogo,tafakari tena mada yako. Maisha ya sasa ni ya manati halafu bado mtu anajaribu ku-complicate?

Hufai kuwa rais, hutaweza kuhonga japo tarafa
 
Back
Top Bottom