Elections 2010 Hii ni kweli kabisa

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Jana nimemsikiliza vizuri sana mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama cha CUF kuna baadhi ya tafiti zimenikuna na kwa kweli kwa kiasi kikubwa sana zimenifumbua macho na kuona kujua kila ninachokiona sasa hivi ni drama aidha iliyo planiwa kwa makusudi au kwa kutokujua.

Profesa amesema chama chake ndio kinachofuatia kwa kura kwenye uchaguzi wa maka jana wa serikali za mitaa na hakuna chombo cha habari chochote kinachosema hili au kuwahi kulisema hili. Anaongeza kusema vyombo vya habari vya Tanzania huwa wanaamua nani wampigie debe na akatolea mfano vyombo vya habari vilivyokuwa vikiipa nguvu CCJ lakini hajui mwisho wake ulikuwa vipi!

Amesema waandishi wa habari wao wanachagua nani wakumkampenia tena kwa nguvu zao lakini ni wananchi ndio wataamua nani wa kumpigia ikifika siku ya uchaguzi.


Wadau mnazikumbuka ripoti za CCJ? Hazifanani na chama fulani? je sio plani za chama tawala? fungueni macho.
 
prof. haonyeshi nia ya dhati kuwakomboa watanzania.
anatembea kabeba uprof. wake kuwa no.1, anajikuta yupo ndani ya kujadili u-profesa dhidi ya u-dr. kapoteza dira.
 
Kweli kaka, jana alitumia muda mwingi kuelezeaPhD yake ikilinganishwa na DR ya Slaa....eti anasema tofauti iliyopo kati ya yeye na Slaa ni kama tofauti kati Ml. Kilimanjaro na Kichuguu....ameshindwa kutueleza jinsi wasifu huo utakavyowasaidia wa-tz kuondokana na umaskini badala yake analeta story za kujiona yeye ni bora kuliko Dr. Slaa na JK.....eti kwa sababu ya PhD yake ya Economics..... Very blunderous prof...shame
prof. haonyeshi nia ya dhati kuwakomboa watanzania.
anatembea kabeba uprof. wake kuwa no.1, anajikuta yupo ndani ya kujadili u-profesa dhidi ya u-dr. kapoteza dira.
 
prof. haonyeshi nia ya dhati kuwakomboa watanzania.
anatembea kabeba uprof. wake kuwa no.1, anajikuta yupo ndani ya kujadili u-profesa dhidi ya u-dr. kapoteza dira.

Anaetembea kwa kutumia barabara na anaeruka hewani yupi ana nia ya dhati kuwakomboa watanzania?
 
Ni kweli kabisa tofauti ya Slaa na Lipumba ,yaani Lipumba anakuwa ni mlima kilimanjaro na huyo Slaa ndio kichuguu ,Slaa amna kitu tunamponda Kikwete kuwa tumepotea njia sasa kumchagua Slaa sio itakuwa tu kupotea njia bali hata muelekeo wa tunapoelekea utakuwa hau[o .kumchagua Slaa ni kupanda mkenge !!! Take care ,jamani tumemchagua Kikwete 2005 imekuwa kama tumeingia kisimani na mkifanya utumbo safari hii kumchagua Slaa itakuwa tumetumbukia bahari ,ndio itakuwa imekwenda Tanzania arijojo ,Slaa mdini na mkabila ,let us see !!!Tatizo hashindi.
 
Back
Top Bottom