Mama kubwa hiyo inaweza kuwa moja ya mikakati mnayoweza kuitumia kuongeza uungwaji mkono wa chama chenu na inaweza kuwasaidia KIDOGO kwenye uchaguzi ujao. Inabidi muelekeze nguvu zenu kwenye kudai katiba mpya itakayoandaa mazingira yanayotoa fursa sawa kwa vyama vyote. Kwa sasa hamuwezi kuishinda CCM ambayo inatumia dola kubaki madarakani.
CCM wana tume ya uchaguzi, wana wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi wa halmashauri za miji na wako chini ya ofisi ya waziri mkuu, wana polisi, wana usalama wa taifa, na wana uhakika wa kuwatumia mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambao wote ni makada wa CCM lakini wanagharimiwa na serikali kuwakampenia CCM. kumkukeni kuwa wakuu wa mikoa na wilaya, ambao ni makada wa CCM, ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa maeneo yao. Kwa kutumia kofia hiyo wanaweza kabisa kutoa maelekezo kwa maofisa wa polisi, usalama wa taifa na jeshi kuhusu kuwasaidia kweye uchaguzi.
Mfumo wa sasa wa kikatiba na kisheria uliandaliwa na Hayati Nyerere kuhakikisha kuwa CCM Inatawala milele. Msipofanikiwa kuubadilisha mfumo huo ili kuwapa fursa sawa na CCM, kamwe hamuwezi kushinda uchaguzi nchi hii. Mtapata majimbo machache ambayo wananchi wake wameamka kisiasa na wanauwezo wa kudai na kusimamia haki zao. Huku kwingine mtaishia kuyasikia kwenye redio tu.