HumbleBoy98
JF-Expert Member
- Aug 30, 2020
- 387
- 396
- Thread starter
- #41
Dah, hii kitu inaweza ikawa kweli aisee. Halafu jinsi ulivyoeleza Happ ndio hivyo hivyo nilivyo! Pia Kuna pahala nilisoma wanasema wenye tatizo hili wanahitaji Aina fulani ya 'hearing aids' ambazo zenyewe zina 'amplify' sauti zenye frequency kubwa (sauti ndogo) bila kuongeza ukubwa wa sauti zile za kawaida. Hivyo kukusaidia kuelewa Yale matamshi.Nilisoma pahala kuwa masikio ni tofauti na macho kwny masikio ubongo inabidi utasfiri nini kinongelewa..
Sasa mara nying neva zikifa ubongo unakuwa hauwezi kutfsiri konsonati kwny matamshi mfano mtu akisema KINONDONI hapo ubongo hzio harufi K, N ,D ndio mana wenye tatizo hili huwa wanasikia sauti tu ila hawaelewi nini kinaongelewa sababu konsonati ndio zinachukua sehemu kubwa ya maneno...
Hvo basi ukipewa dawa au mashine inachukua mda sana ubongo kujifunza upya kusikia konsonati na kuzitasfiri ndio mana unakuta hata ukivaa mashine au ukinywa dawa bado tuuu
Ila kwa hapa bongo sidhani Kama zitakuwepo na Kama zipo Basi hiyo Bei yake nadhani itakuwa ghali mno! Maana hizi nilizonunuaga pale mindu upanga kwa wahindi Ni za kawaida tu ila Bei yake Sasa!