Hii ni high frequency hearing loss, au ni nini?

Hii ni high frequency hearing loss, au ni nini?

Duu! Pole sana mkuu, vilema vya ukubwani kiukweli huwa vinatesa sana, alafu hadi mtu uje ujikubali inachukua muda, lakini dawa hapo ni wewe tu kujikubali na kusonga mbele ndipo wengine watakukubali kama ulivyo! Atakaekucheka mpuuze, fanya lile lililo ndani ya uwezo wako na Mungu pia hatokutupa!
 
Hapo kuna Tatizo la Ubongo wako kushindwa kuinterpret unachokisikia na sio tatizo la sikio.. !! May be nerves zinashida au kuna dawa ulitumia zikaathiri mfumo wa Ubongo unaohusiana na speech interpretation.

Je ulichelewa Kuongea ulipokuwa mdogo au ulipata shida kuongea???? Maana watoto huongea wanachokisikia so kama ulichelewa means ulikuwa na shida toka mwanzo.
 
Kuna dawa inaitwa Gink Giloba je ushawahi kuitumia????
Huwa inacontain suppliments muhimu sana ambazo husaidia kuimprove hali kama yako
 
Pole sana mimi nina shida kama yako ila ni sababu ya nerve compression ilianza macho then masikio . Kwa macho natumia miwani nilianza tatizo nikiwa mdogo sana sema hawakujua then 2012 nikaanza hearing loss ndo nagunduliwa na tatizo la nerve 2018 which is too late . Daktari kaniambia nitumie hearing aids zile digital

Apart from that nina tinnitus kutokana na nerve compression yaani inanipa tabu ila najikaza nicopy nayo tatizo haliwezi kutibika

Ushauri: Nenda ENT muhimbili uone watakuambia nini
 
Inauma sana kaka sana sana kipengele cha simu kinakosesha mengi mana kuna watu meseji huwa hawajibu
Pole sana ila hawajakuelewa tu,wakikuelewa lazima wakujibu sababu ndiyo mawasiliano yako.

Kuhusu chuo jitambulishe kwa dean of students yeye atakutambulisha special department nk..

Kuhusu kujifundisha mwenyewe,ukiomba wakuelekeze watakusaidia na notes pia utapewa maana class usikii chochote...

Watu wakijua tatizo lako watakupa ushirikiano mzuri na kukupenda pia.....wa kucheka cheka wapo ila achana nao.
 
Dah! Asante Sana mkuu🙏🙏🙏 Ni ukweli mchungu lakini hamna jinsi inabidi kukabiliana na Hali halisi. Ni kweli baada ya kuendelea kutafuta zaidi na zaidi nimegundua kuwa hakuna tiba specifically kwa tatizo hili wanasema Ni mpaka upate Aina sahihi ya hearing aid.
Pia pole Sana kwa tatizo lako mkuu lakini hatutakiwi kukata tamaa inabidi tupambane Kama tulivyo.
 
Hivi hii ndio Tinnitus ,sikio kupiga kelele!? Mimi sikio moja linaunguruma tu muda wote, nikilala ndio napumzika nalo
Kwanza pole Sana kwa tatizo lako mkuu.
Hapana hii SIO 'tinnitus' sababu sikio halipigi kelele ila tu ndio hivyo unakuwa huelewi mtu anachoongea isipokuwa binafsi mara moja moja Sana nasikia mlio mdogo masikioni, hasa sikio la kushoto nasikia kamlio kadogo ile "tiiiii" halafu baada ya muda kanapotea na Wala hakaumizi.
 
Tupo wengi mkuu. Mi nilishafanyiwa usafishaji zaidi ya mara tatu ila ikabuma. Nikafanya hearing test ndio nikagundua nina excess hearing loss ambayo imesababishwa na kuathirika kwa nerves. Nishatumia dawa kama gentamycene ya drop na vidonge flani hivi walisema ni nerves ila ikabuma bado.

Ni tatizo baya sana ila inabidi tukubali tu. Mimi siongei na simu yaani situmiagi dakika kabisa, mawasiliano yangu ni kwa sms tu.
Siangalii movie bila subtitles, never, Nahisi kukosa body balance hivyo huwa inaniwia vigumu sana michezoni na nishaacha kucheza step kwenye kwaya maana unakuwa kichekesho,

In short, ilivyoeleza ndivyo nilivyo. Cha msingi ni kama alivyosema mdau hapo juu ni kujikubali na kuwa muwazi basi.
Dah! Mkuu kwanza pole Sana, maana wewe mpaka 'vestibular system' yako pia imeathirika mpaka unakosa balance.
Hii issue yako Ni more serious ila Mungu akutie nguvu mkuu🙏🙏🙏
 
Ni kweli mkuu, watu wanajua shida yangu kuanzia wanafunzi Hadi facilitators na kwakweli support huwa naipata.

Ila Kuna limitations hususa Ni linapokuja swala la mafunzo kwa vitendo maana taaluma ninayosomea inahitaji Mimi ndo niwe nawasiliana na watu mara kwa mara na haikwepeki, lakini huwa nakaza hivyo hivyo kibishi bishi.

Asante kwa mchango wako mkuu
 
Hapo kuna Tatizo la Ubongo wako kushindwa kuinterpret unachokisikia na sio tatizo la sikio.. !! May be nerves zinashida au kuna dawa ulitumia zikaathiri mfumo wa Ubongo unaohusiana na speech interpretation.

Je ulichelewa Kuongea ulipokuwa mdogo au ulipata shida kuongea???? Maana watoto huongea wanachokisikia so kama ulichelewa means ulikuwa na shida toka mwanzo.
Hapana bro sikupata shida yoyote kati ya hizo ulizotaja utotoni mwangu, nilikuwa fresh kabisa Yani.
 
Kuna dawa inaitwa Gink Giloba je ushawahi kuitumia?

Huwa inacontain suppliments muhimu sana ambazo husaidia kuimprove hali kama yako
Hapana mkuu, ila niliwahi tumia zile za kuimarisha mishipa ya fahamu kwa muda wa mwezi mzima zinaitwa "Neuroton" lakini wapi tatizo Bado lipo.
 
Pole sana kwa changamoto. Una tatizo kama la mdogo wangu ambaye nae alianza kugundua kua hayupo sawa akiwa 4m 6 kajitahidi kufanya mitihani katika mazingira magum kutokana na comb aliyokua anasoma PCB kumuangusha. Tukaamua kumtafutia chuo cha afya kasoma mwaka wa kwanza tu akafel na kukosa sifa za kuendelea na masomo.

Tumejitahidi sana Ekenywa, Upanga kote tulikwenda bila mafanikio. Majibu ya mwisho niliyoyapata Muhimbili ni kwamba ana tatizo la nerves za usikivu zilishakufa tukashautiwa atumie hearing aid lakin wapi. Kwa sasa amekubali hali na anaendelea na maisha. Inauma sana ila haina namna.
 
Pole sana mimi nina shida kama yako ila ni sababu ya nerve compression ilianza macho then masikio . Kwa macho natumia miwani nilianza tatizo nikiwa mdogo sana sema hawakujua then 2012 nikaanza hearing loss ndo nagunduliwa na tatizo la nerve 2018 which is too late . Daktari kaniambia nitumie hearing aids zile digital

Apart from that nina tinnitus kutokana na nerve compression yaani inanipa tabu ila najikaza nicopy nayo tatizo haliwezi kutibika

Ushauri: Nenda ENT muhimbili uone watakuambia nini
Pole sana mkuu kwa tatizo lako ila hatutakiwi kukata tamaa Mungu Ni mwema atatusaidia na asante Sana kwa ushauri wako
 
Pole sana kwa changamoto. Una tatizo kama la mdogo wangu ambaye nae alianza kugundua kua hayupo sawa akiwa 4m 6 kajitahidi kufanya mitihani katika mazingira magum kutokana na comb aliyokua anasoma PCB kumuangusha. Tukaamua kumtafutia chuo cha afya kasoma mwaka wa kwanza tu akafel na kukosa sifa za kuendelea na masomo. Tumejitahidi sana Ekenywa, Upanga kote tulikwenda bila mafanikio. Majibu ya mwisho niliyoyapata Muhimbili ni kwamba ana tatizo la nerves za usikivu zilishakufa tukashautiwa atumie hearing aid lakin wapi. Kwa sasa amekubali hali na anaendelea na maisha. Inauma sana ila haina namna.
Dah! Poleni Sana mkuu.

Ila hili tatizo la kufa kwa 'nerves' sijui kwanini linatupata Sana vijana wadogo siku hizi.

Kuna haja ya wataalamu kutuelimisha juu ya tatizo hili ili nasi tuje kuwalinda watoto wetu na vizazi vyetu baadaye.

Mpe pole Sana kijana mwenzetu Mungu amtie nguvu hata hivyo amejitahidi Sana kupambana na isingekuwa Hilo tatizo huenda angefika mbali.

Mimi mwenyewe Niko chuo Cha afya na ugumu ninaoupata naujua, Ni ngumu Sana kusurvive ukiwa na matatizo ya Aina hii na unasoma hizi kozi.
 
Kisema kweli mzee omba Mungu tu hilo tatizo halitibiki ni neva kwny ubongo zimekufa mie pia na shida hyo nishaenda huko Ekenywa, Upanga mtaa wa Mindu jwa wahindi wa bei mbaya bila mafanikio..

Hearing aid haziwez kukusaidia sababu sikio lipo vizuri ni mishipa kichwani imezingua ni kama vile mtu anapikua kipofu there is no way jikubali na hali yako na pia kuwa free usifiche ukifika sehemu ni mgeni sema kuwa husikii waangalie watakusaidieje ikitoke watu wame ku diss au kukucheka hujasikia take it easy mzee...

So jikubali Hospital kwa bongo haoa utapoteza pesa labda nje ya nchi
Hii ni kweli Mzee tatizo ni Mishipa ambayo inapeleka taarifa kwenye Ubungo ndio yeye shida hiyo inaweza kutokana na chakula ambvyo ulikuwa unakula au umerithi
 
Hii ni kweli Mzee tatizo ni Mishipa ambayo inapeleka taarifa kwenye Ubungo ndio yeye shida hiyo inaweza kutokana na chakula ambvyo ulikuwa unakula au umerithi
Hata Mimi nilikuwa nahisi hivyo hivyo na watu walipokuwa wananishauri nitumie 'hearing aids' nilikuwa napinga kwa hoja hii hii.
Nilikuwa nahisi kabisa tatizo litakuwa kwenye 'nerves'.

Halafu Kuna kipindi na macho nayo yakaanza kuzingua, nilikuwa siwezi kabisa kusoma hata gazeti yaani nasogeza karibu kabisa na macho na Bado sioni maandishi naona ukungu tu!

Nilipokwenda pale CCBRT wakaniambia Ni 'nerves' zimeisha nguvu ndio maana hata masikio yanazingua. Basi wakanipa dawa fulani (jina limenitoka) ila inafanya kazi ya kuimarisha 'nerves', wakanipa hizo na vidonge vya 'folic acid' nikatumia kwa muda wa miezi mitatu mfululizo, macho yakapata afadhali nikarudi tena wakanipa Tena vidonge vile vile nikatumia kwa miezi mitatu mingine macho yakapona kabisa na mpaka leo yako fresh ila ishu imebaki kwenye masikio.

Sasa Sijui kwa Nini hizi 'nerves' za masikio hazikurudi katika Hali ya kawaida wakati za macho zilikubali.
 
Hata Mimi nilikuwa nahisi hivyo hivyo na watu walipokuwa wananishauri nitumie 'hearing aids' nilikuwa napinga kwa hoja hii hii. Nilikuwa nahisi kabisa tatizo litakuwa kwenye 'nerves'...
Nilisoma pahala kuwa masikio ni tofauti na macho kwny masikio ubongo inabidi utasfiri nini kinongelewa..

Sasa mara nying neva zikifa ubongo unakuwa hauwezi kutfsiri konsonati kwny matamshi mfano mtu akisema KINONDONI hapo ubongo hzio harufi K, N ,D ndio mana wenye tatizo hili huwa wanasikia sauti tu ila hawaelewi nini kinaongelewa sababu konsonati ndio zinachukua sehemu kubwa ya maneno...

Hvo basi ukipewa dawa au mashine inachukua mda sana ubongo kujifunza upya kusikia konsonati na kuzitasfiri ndio mana unakuta hata ukivaa mashine au ukinywa dawa bado tuuu
 
Back
Top Bottom