Hii ni hatari!

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Wiki iliyopita katika msikiti mmoja maarufu hapa Arusha kilitokea kituko cha mwaka. Wakati waumini wakiwa wameinama katika kuabudu, muumini mmoja alijisahau kuzima simu yake ya mkononi mara ikaanza kuita. Mlio wa simu hiyo ulikuwa ni wimbo wa Rose Mhando "Nibembeleze Nibebe...nipeleke mbinguni kwa Baba"! Hebu niambie kilichotokea baada ya ibada... Muumini huyo alipaa kipigo cha mbwa mwizi hadi alipookolewa na polisi.

Read more: Hii ni hatari! - FotoBaraza.Me
 
Nashindwa kuelewa walimpiga kwasababu ni muislamu anaependa kwaya au walidhani ni mkristo kaingia msikitini kwao??Ajabu kweli...hata uhuru wakujichagulia ringtone hamna!
 
Nashindwa kuelewa walimpiga kwasababu ni muislamu anaependa kwaya au walidhani ni mkristo kaingia msikitini kwao??Ajabu kweli...hata uhuru wakujichagulia ringtone hamna!

hv kuna uhuru wa kujichagulia ring tune kwenye katiba?au ni mambo ya udini yameinguia hapo na alikua ni ustaadh huyo
 
hv kuna uhuru wa kujichagulia ring tune kwenye katiba?au ni mambo ya udini yameinguia hapo na alikua ni ustaadh huyo

Sasa simu yako ringtone uchaguliwe na dini!Mbona kazi ipo...sijaona sababu yakumpiga mtu hapo!
 
Nashindwa kuelewa walimpiga kwasababu ni muislamu anaependa kwaya au walidhani ni mkristo kaingia msikitini kwao??Ajabu kweli...hata uhuru wakujichagulia ringtone hamna!

hata kwa sababu hizo, haihalalishi kipigo, sikuhizi hata wanyama hawapigani sembuse watu kwenye nyumba za ibada wanaendekeza unyama?. Shame upon them.
 
Nashindwa kuelewa walimpiga kwasababu ni muislamu anaependa kwaya au walidhani ni mkristo kaingia msikitini kwao??Ajabu kweli...hata uhuru wakujichagulia ringtone hamna!

Swali zuri sana hilo Lizzy.
Lakini bila ya shaka walifikiri kuna Mkristo kaingia msikitini kwao.
 
msikitini zima simu period

Amepigwa kwasababu ameleta nuisance msikitini siyo kwasababu ya mlio wake

Ukimya wakati wa ibada ndio nidhamu kwa Muumba

Unaweza kufanya utani sokoni kwenu sio kwa Muumba wa Mbingu ok

Halali yake, ningekuwepo ningemuongezea ili wakati anaenda msikitini ajiandae kwa utulivu bravo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom