Hii ni Hatari sana!!!!

Mangaline

JF-Expert Member
May 19, 2012
1,045
221
Taarifa ya Habari ITV, ya saa mbili, imeonesha mgogoro wa ardhi, ambapo polisi walipambana na raia, wakati raia wakitumia silaha za jadi (Mishale) katika kupambana na polisi. Polisi wameshinda.

Tatizo hapa si kushinda wala kushindwa kwa polisi, bali ni hatua ambayo wananchi wamefikia, ya kuthubutu kurusha mishale katika jitihada za kujihami dhidi ya nguvu za dola. Kama hatua imefikia hapo, basi ipo haja ya polisi kupunguza matumizi ya nguvu, na kujaribu mbinu mbadala, kwani kukuza nia hiyo ya wananchi, kutasababisha kukua kwa matumizi ya nguvu ya umma dhidi ya dola, kitu ambacho kitakuwa hatari sana kwa utawala.

Ikumbukwe kuwa polisi hao familia zao ziko uraiani. Hii ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom