Hii ni hatari hata noti zetu tunachakachua

nguluvisonzo

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
515
71
Najisikia vibaya sana kutokana na hali halisi ya Taifa letu,kuna vitu vingi sana vinasikitisha na tumeviona,wototo kufukiwa katika kaburi moja,dowans,IPTL,EPA,makalio ya wachina n.k.
Lakini hili la NOTI ZINAZOTUMIKA KAMA FEDHA HALALI KWA MALIPO HALALI KUCHUJA RANGI HII NI KALI.Jamani wekundu wa msimbazi mpya inachuja rangi hata ukiweka katika karatasi nyeupe ukawa kama unafuta juu ya hiyo karatasi utaona rangi nyekundu ikibaki,hivi hawa benki kuu na gavanor wao wakoje,kila mahala wizi wizi tu tufanyeje ? labda katiba mpya iwe na kipengele cha atakaye hujumu ucumi,iba mali ya umma,atakayesababisha hasara kwa taifa kwa taaluma yake(daktari,mwanasheria,engeneer,n.k)wanyongwe shingo mpaka kufa hadharani kila mtanzania akishuhudia ndipo hatutakuwa na mambo haya.
noti zetu ni dhaifu jamani, kulikoni BOT mtueleze nani kazitengeneza na alipataje tenda hiyo ya kutuharibia fedha yetu.
BOT bado kuna ufisadi Mkwere kapelekewa sample akawasifu, kumbe bomu kubwa alikuwa analitegua ni hatari sana, awashikishe adabu wahusika kwani wanamshushia hadhi kila kukicha.
 
Juzi zimekamatwa feki kariakoo nilitegemea watatangaza kwenye vyombo vya habari lakn nimeona kimya anyway sijui
 
kwani hata jina hii nchi inaitwaje?
a) Jamhuri ya muungano wa tanganyika, unguja na pemba.
b)jamhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar

au

c)Jamhuri ya muungano wa tanzania ---uchakachuzi huu (neno 'muungano' ktk nchi ambayo mnasema imeshakuwa moja linatoka wapi na kwa nini liendelee kutumika badala ya kusema tu Jamhuri ya Tanzania ikiwa kuna muungano wa kweli)

unchakachuaji hapa TZ ulianza siku nyingi sana, now we are at the breaking point.
 
Aisee nina elfu kumi hapa....nimechukua karatasi jeupe nimesugua, rangi imebaki kweli!!!......dah, kazi tunayo.
 
Na noti feki zimezagaa kibao zinatokea Arusha, juzi kapigwa jamaa 2mil Tegeta
 
khaaa yaani kila kitu ifanyacho serikali ya ccm mnapinga mengine tukubali tuu hata kama ni feki!

kwa sababu hatuna namna kwa sasa. bora tuwe kama zimbabwe au somalia tutumie dola au sarafu za nchi jirani....
 
Ukichunguza sana utagundua hata viongozi wetu ni feki ndio maana hawana uchungu na nchi yetu
 
Fuatilia history ya ujio wa izo note mpya ndo utajua kuwa una serikali makini au lah!
 
khaaa yaani kila kitu ifanyacho serikali ya ccm mnapinga mengine tukubali tuu hata kama ni feki!

we ndo kabisa bendera hufuata upepo, utabaki na mtizamo wako hasi yaani kwa vile kimetokana na serikali hata kama ni feki tukubali tu mmmm na wasiwasi na na ww mayb ukapimwe upya mirembe.kama ww ni kijana lazima uamke utete liliojema na sio feki.
 
Back
Top Bottom