Hakikwanza
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 4,034
- 1,003
Kwanza kwa heshima kubwa nikupongeze Mh Nape kwa kuunda kamati ndogo ili iweze kuja na uhalisia wa nini kilitokea ofisi za Clouds. Kwamba hii kamati izihoji pande zote mbili ili kuupata ukweli wa kilichotokea pale Clouds. Ninashukuru sana kwa kuwa umetumia njia bora za kiongozi, kusikiliza kwanza pande zote zinazo husika kwenye mgogoro. Lakini imenisikitisha sana kwa mkuu wa mkoa kwa kuikwepa hii kamati teule iliyoundwa na waziri mwenye dhamana. Hii ni dharau kubwa sana inayoonyeshwa na RC kwa waziri. Pole sana waziri na kamati yako kwa kudharauliwa hivyo.