Hii ni anti virus nzuri kwa simu

Hii ni anti virus nzuri kwa simu

King Octavian

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2011
Posts
403
Reaction score
353
habar ya humu wana science...naomba msaada wa kuelekezwa ni antivirus gani ni nzuri kuweka kwenye simu zinazotumia operating system ya Android? maana ninatumia avast lakini naona haisaidii lolote..msaada wa maelekezo ninauhitaji kutoka kwenu wataam
 
Huna sababu ya kuweka antivirus kwenye android device yako simply because haitokusaidia chochote zaidi ya kukulia battery maana itakua inarun kwenye background muda wote na kufanya simu kwenda slow... afu kuna muda itadetect software yako ya kawaida kama virus which unakuta si kweli, sanasana itakusumbua kuconnect kwenye network to some apps etc....
Kama unadownload softwares kutoka Google Play store huna haja ya kuhofia malware maana hawana software zenye virus kwenye store, ila kama unapenda kudownload cracked softwares basi hapo ndo kuna probability flani ndogo sana ya kukutana na malware
 
Asante mkuu, wasi wasi wangu mpaka kuhitaji strong antivirus ni kwamba huwa naingia kwenye sites ambazo siziamini sana kwa usalama wa simu yangu, huwa nadownload movies, nodownload photos au audio files..je siwez kubeba na virus huko maana ni nje ya playstore
 
Tumia Lookout ni nzuri mimu natumia nikidownload chochote inascan
 
Huna ulazma sana wa kutumia antivirus coz sio rahs kuinstall malware from trusted sources such as play store.
Benefit ya hizi app inakuja kwenye operations kama backup na anti-theft, mfano kukupa uwezo wa kuformat device ikitokea ikaibiwa.
 
Hapo haiwezekani, virus vinaingia pale ambapo una install app yenye virusi.
Pia uwezekano wa kupata hizo app ni mdogo mno ukidownload kutoka play store yenyewe, since kuna 'mabaunsa' wa google wanaoscan hzo apps.
 
Hapo haiwezekani, virus vinaingia pale ambapo unainstall app yenye virusu.

ahaaa kama ndivyo ilivyo basi nimekupata mkuu, ila katika pitapita zangu ninamojifunza funza nimewahi sikia kuwa kuna baadhi ya ya websites zina virus hivyo kama ukidownload video ama ukadownload photos au tu kuzitembelea wale virusi wanaingia kwenye device yako bt hii nili iexperience kwenye PC
 
Yes, ni kweli kwenye PC inawezekana. Mfumo wa ufanyaji kazi wa android devices na PC una utofauti. Kwenye PC, commands znaweza zikawa automatically executed kupitia autoruns na vitu kama hivyo.
 
Hapo haiwezekani, virus vinaingia pale ambapo una install app yenye virusi.
Pia uwezekano wa kupata hizo app ni mdogo mno ukidownload kutoka play store yenyewe, since kuna 'mabaunsa' wa google wanaoscan hzo apps.

Umechanganya na MAC app store nn! Playstore ndo ocean ya malware, spyware na taka zote kwene droid devices.
 
siku hizi watu wanataka hela, malware hawaji tena kama mfumo wa virusi kuharibu mpangilio wa simu bali wanakuja kama spyware kuiba data zako na pia wanakuja kama adware kukuekea matangazo kila eneo.

na google mwenyewe ndio kiongozi wa kuiba data hivyo usishangae kwanini loophole nyingi hazizibwi kwenye android.

na kusema playstore ipo safe si kweli kuna malware kibao mule na wengine ni majina makubwa tu na wanajulikana. mfano app kama chrome inataka always microphone iwe on ya kazi gani? kuna uhusiano gani kati ya browser na microphone?

kuna app kama camera 360 hii ni camera ila always ipo online busy kabisa inatransfer data. kama huamini na unayo kwenye simu nenda setting halafu apps halafu running apps icheki utakuta camera 360 inarun. sasa jiulize kuna haja gan camera iwe active 24hrs kila ukiifunga inajifungua chini kwa chini.

android inabaki simu ya kuchezea tu kama unafanya vitu vya maana tafuta closed system kama ios au wp ufanye mambo yako ya maana ukitaka games na movies rudi android.
 
Duh! kwa hiyo chief mkwawa unaniambiaje hapo nimekuelewa vzr lakini sijakupata kuhusu tatizo langu
 
Duh! kwa hiyo chief mkwawa unaniambiaje hapo nimekuelewa vzr lakini sijakupata kuhusu tatizo langu

hakuna haja ya kuwa na ant virus inabidi tu mwenyewe uwe unaangalia tabia za za apps zako zinavyobehave.

ni ngumu kugundua kwa siku moja ila baada ya muda utazoea.

mfano unaona matangazo yanakuja kwenye notification hapo utajua una adware kwenye simu yako. utahold lile tangazo then itakuja app info utaclick utajua ni app gani inakuletea lile tangazo then un install.

same kwenye apps nyengine ukiona tu simu imekua na tabia ya ajabu ajabu toka ueke app fulani basi itoe hio ndio njia nzuri.
 
Asante mkuu nimekupata na hiyo kitu unayosema nime iexperience mara nyingi kwenye simu hii, dah umetisha kaka
 
Kwa adware aisee google ndio njia yao ya kupata pesa, kucollect personal data zako na kuzitumia kusambaza matangazo. Ila ulichosema chief mkwawa ni sahihi kabisa. Zipo apps za ajabu ajabu sana.
 
Back
Top Bottom