Hii ni aibu, TBC1 yashika nafasi ya mwisho

Status
Not open for further replies.

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746
UMEIPATA HII YA TBC 1 KUSHIKA NAFASI YA MWISHO....!!!!!

TBC1.png​

Kwa hali ya kushangaza, kituo cha television cha matangazo cha tbc 1 kati ya vituo vinne maarufu vya matangazo ya habari nchini Tanzania kimeshika nafasi ya mwisho baada ya kufanyiwa utafiti,

Kwa habari za uhakika ni kwamba kituo kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji wengi ni ITV kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya tatu imeshikwa na Channel 10 na hatimaye TBC1.

Kwa utafiti uliofanya na na TCRA imebainika kuwa ni aibu kama kituo television ambacho ni cha Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma ya vituo binafsi jambo ambalo ni hatari.

Vyanzo vya kuaminika vinadai kuwa TBC1 imefikia hapi baada ya kugundulika inabagua baadhi ya habari ya vyama vya siasa na kutoa habari ya chama kimoja tuu jambo ambalo siyo sahihi katika utashi wa utangazaji na kutofuata uhuru wa kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la habari la Tanzania,

Utafiti umeonyesha kuwa ili chombo cha habri kiweze kuangaliwa na watu wote wa vyama vyote ni lazima chombo cha habari kitoe habari bila kubagua vyama vya siasa maana watazamaji wana misimamo tofauti na itikadi tofauti, na kama chombo cha habari kikiamua kutoa habari kwa chama kimoja cha siasa basi ujue hapo watakaoangali hizo taarifa za habari ni hao hao wa chama kimoja.

Watafiti pia walienda mbali zaidi na kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha utangazaji kuwa ni chombo cha UMMA na kisipende kubagua baadhi ya taarifa za habari za vyama vya siasa kwa misingi ya kuelekezwa na wanasiasa au viongozi wa nchi maana madhara yake ni wananchi kushindwa kuangalia hicho kituo.

Mwisho wake kitashindwa kufanya biashara na hatimaye kutegemea tuu ruzuku serikalini na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara badala ya kukiacha chombo kijiendeshe kwa uhuru. Wametoa mfano kama shirika la habari la Uingereza BBC lingefanya kama TBC inavyofanya basi nayo ingeishia kutazamwa tuu nchini uingereza na tena kwa watu wachache tofauti na ilivyo sasa BBC inatazamwa duniani kote.

Utafiti umeonyesha kuwa hivi vyombo vingine vya habari ITV, Star TV na Channel 10 vimepata watazamaji wengi kwa kuwa havibagui matangazo ya kada tofauti ya vyama vya siasa na hapo ndoo inasababisha waweze kupata watazamaji wa kutosha.

=======

Majibu ya TCRA

Jihadhari na taarifa hii sio ya kweli! TCRA haijafanya utafiti na sio moja ya kazi za Mamlaka! Tunachukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya mtandao.
 
sikumbuki mara ya mwisho niliangalia lini taarifa ya habari ya TBC 1. Wameksa weledi kabisa, najua wanafanya makusudi kutokana na mashinikizo ya watawala ambao wameegemea chama kimoja cha siasa. CCM!
 
mbona tz sekta binafsi ndo zinafanya vizuri kuliko za serikali..hilo sio jambo jipya kbs bongo..shule.hospital.kampuni binafsi zinatoa huduma fresh so sio suala la ajabu xana
 
Jihadhari na taarifa hii sio ya kweli! TCRA haijafanya utafiti na sio moja ya kazi za Mamlaka! Tunachukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya mtandao.
 
kuna msomi mmoja alikua anaongea sana kwenye makongamano kapewa u CEO tbc ndo wale wale wasomi wa tz waganga njaa
 
UMEIPATA HII YA TBC 1 KUSHIKA NAFASI YA MWISHO....!!!!!

View attachment 197797​

Kwa hali ya kushangaza, kituo cha television cha matangazo cha tbc 1 kati ya vituo vinne maarufu vya matangazo ya habari nchini Tanzania kimeshika nafasi ya mwisho baada ya kufanyiwa utafiti,

Kwa habari za uhakika ni kwamba kituo kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji wengi ni ITV kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya tatu imeshikwa na Channel 10 na hatimaye TBC1.

Kwa utafiti uliofanya na na TCRA imebainika kuwa ni aibu kama kituo television ambacho ni cha Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma ya vituo binafsi jambo ambalo ni hatari.

Vyanzo vya kuaminika vinadai kuwa TBC1 imefikia hapi baada ya kugundulika inabagua baadhi ya habari ya vyama vya siasa na kutoa habari ya chama kimoja tuu jambo ambalo siyo sahihi katika utashi wa utangazaji na kutofuata uhuru wa kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la habari la Tanzania,

Utafiti umeonyesha kuwa ili chombo cha habri kiweze kuangaliwa na watu wote wa vyama vyote ni lazima chombo cha habari kitoe habari bila kubagua vyama vya siasa maana watazamaji wana misimamo tofauti na itikadi tofauti, na kama chombo cha habari kikiamua kutoa habari kwa chama kimoja cha siasa basi ujue hapo watakaoangali hizo taarifa za habari ni hao hao wa chama kimoja.

Watafiti pia walienda mbali zaidi na kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha utangazaji kuwa ni chombo cha UMMA na kisipende kubagua baadhi ya taarifa za habari za vyama vya siasa kwa misingi ya kuelekezwa na wanasiasa au viongozi wa nchi maana madhara yake ni wananchi kushindwa kuangalia hicho kituo.

Mwisho wake kitashindwa kufanya biashara na hatimaye kutegemea tuu ruzuku serikalini na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara badala ya kukiacha chombo kijiendeshe kwa uhuru. Wametoa mfano kama shirika la habari la Uingereza BBC lingefanya kama TBC inavyofanya basi nayo ingeishia kutazamwa tuu nchini uingereza na tena kwa watu wachache tofauti na ilivyo sasa BBC inatazamwa duniani kote.

Utafiti umeonyesha kuwa hivi vyombo vingine vya habari ITV, Star TV na Channel 10 vimepata watazamaji wengi kwa kuwa havibagui matangazo ya kada tofauti ya vyama vya siasa na hapo ndoo inasababisha waweze kupata watazamaji wa kutosha.
Clouds TV na utitiri mwingine wa TV haujadukuriwa
 
Jihadhari na taarifa hii sio ya kweli! TCRA haijafanya utafiti na sio moja ya kazi za Mamlaka! Tunachukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya mtandao.
Hongereni sana kumbe mpo humu ndyo maana nikashangaa iweje nyingine hazipo? Japo tbc Haifanyi vizuri lakini hiyo siyo kazi yenu kutoa eti hadi maoni
 
Hivi TBC 1 nacho ni kituo cha Television kwanza picha mbaya sio HD wala 3D
Wanatumia camera za mwaka 2000 niangalia huo ujinga wao kwa kipi
Niacha kuangalia Television zenye ubora niangalia eti TBC si uboya huo
 
Jihadhari na taarifa hii sio ya kweli! TCRA haijafanya utafiti na sio moja ya kazi za Mamlaka! Tunachukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya mtandao.
Afadhari kama TCRA mpo humu, hebu naomba unijibu kuhusu suala la ving'amuzi kurusha Local channel kwa kulipia, haya ndo mambo yenye tija badala ya kukanusha kanusha mtupe ufafanuzi wa kueleweka, wakati mnatuaminisha kuhamia Digitali mlisema hakuna atayelipia local channel Leo hii mmetuachia TBC pekee kuwa ndo Local channel ITV,CHANNEL TEN,AZAM TV ZOTE (1&2) EATV, CLOUDS etc. Hizi zipo nchi gani kama si Local channel?
 
TCRA Wakirudi kukujibu swali lako nidai vocha ya elfu tano kunako PM, mtandao wowote. Nitakupa. Weka link tu ya jibu lao, itatosha kama ushahidi. I swear!
 
UMEIPATA HII YA TBC 1 KUSHIKA NAFASI YA MWISHO....!!!!!

View attachment 197797​

Kwa hali ya kushangaza, kituo cha television cha matangazo cha tbc 1 kati ya vituo vinne maarufu vya matangazo ya habari nchini Tanzania kimeshika nafasi ya mwisho baada ya kufanyiwa utafiti,

Kwa habari za uhakika ni kwamba kituo kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji wengi ni ITV kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya tatu imeshikwa na Channel 10 na hatimaye TBC1.

Kwa utafiti uliofanya na na TCRA imebainika kuwa ni aibu kama kituo television ambacho ni cha Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma ya vituo binafsi jambo ambalo ni hatari.

Vyanzo vya kuaminika vinadai kuwa TBC1 imefikia hapi baada ya kugundulika inabagua baadhi ya habari ya vyama vya siasa na kutoa habari ya chama kimoja tuu jambo ambalo siyo sahihi katika utashi wa utangazaji na kutofuata uhuru wa kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la habari la Tanzania,

Utafiti umeonyesha kuwa ili chombo cha habri kiweze kuangaliwa na watu wote wa vyama vyote ni lazima chombo cha habari kitoe habari bila kubagua vyama vya siasa maana watazamaji wana misimamo tofauti na itikadi tofauti, na kama chombo cha habari kikiamua kutoa habari kwa chama kimoja cha siasa basi ujue hapo watakaoangali hizo taarifa za habari ni hao hao wa chama kimoja.

Watafiti pia walienda mbali zaidi na kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha utangazaji kuwa ni chombo cha UMMA na kisipende kubagua baadhi ya taarifa za habari za vyama vya siasa kwa misingi ya kuelekezwa na wanasiasa au viongozi wa nchi maana madhara yake ni wananchi kushindwa kuangalia hicho kituo.

Mwisho wake kitashindwa kufanya biashara na hatimaye kutegemea tuu ruzuku serikalini na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara badala ya kukiacha chombo kijiendeshe kwa uhuru. Wametoa mfano kama shirika la habari la Uingereza BBC lingefanya kama TBC inavyofanya basi nayo ingeishia kutazamwa tuu nchini uingereza na tena kwa watu wachache tofauti na ilivyo sasa BBC inatazamwa duniani kote.

Utafiti umeonyesha kuwa hivi vyombo vingine vya habari ITV, Star TV na Channel 10 vimepata watazamaji wengi kwa kuwa havibagui matangazo ya kada tofauti ya vyama vya siasa na hapo ndoo inasababisha waweze kupata watazamaji wa kutosha.

Kwa asilimia kubwa ya Watangazaji walionao ambao wanaokimbizana ' kiumri ' na Rais wa Zimbabwe Mzee Mugabe huku mawazo yao sasa yakiwaza tu ' Pensheni ' na ' Presha ' za Kifamilia hasa za Wajukuu, Vitukuu na Vilembwe unategemea ' jipya ' tena hapo Mkuu? Labda subiria tu kuna siku tutakuja kuona Mtangazaji ' anatiririka ' kusoma taarifa ya Habari huku anasinzia na ile Karatasi yake ' Script ' akiitumia kufukuzia ' mbu ' tu pale Studioni.
 
Nmecheka sana mkuu
 
Nakumbuka mgomo mmoja pale revolution square TBC walivyofika tu walitimuliwa wakaondoka bila kuwasha hata camera...kiufupi TBC haipendwi na karibia watu wote wanaohisi hawana share serikalini..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom