lord atkin
Senior Member
- Sep 30, 2018
- 197
- 683
Mwanzoni ilikuwa Wapangaji wa nyumba na ofisi Kwa ajili ya biashara tu (commercial/business) ndiyo waliokuwa wakitakiwa kulipa withholding tax ya asilimia kumi (10%) TRA. Kifungu Cha 82(2)(a) Cha The Income tax Act RE 2019 kiliweka wazi kuwa mtu asilipishwe withholding tax ya pango la jengo au nyumba kama halitumii Kwa biashara. Hivyo Wapangaji wa fremu za maduka, maofisi na biashara zinginezo tu ndiyo waliotakiwa kulipa Kodi ya withholding tax ya 10% TRA.
Bunge letu tukufu kupitia sheria ya fedha ya 2022, (The Finance Act, 2022) Kwa busara zake liliifanyia marekebisho sheria ya Kodi yaani The Income Tax Act R.E 2019 na kufuta kifungu Cha 82(2)(a) kilichokuwa kimetoa maelekezo kuwa wanaopaswa kulipa Kodi ya withholding tax ya 10% ya pango ni wale tu wanaopanga nyumba Kwa madhumuni ya biashara.
Kufuatia marekebisho haya ya sheria Sasa ni Kila mpangaji hata wale wanaopanga nyumba Kwa ajili ya makazi binafsi (residences) wanatakiwa kulipa asilimia 10 ya Kodi ya nyumba ya Kila mwezi TRA kama withholding tax na utaratibu uliotolewa na TRA ni kwamba wanapaswa kulipa wapangaji na kuwapelekea risiti wenye nyumba kuwa asilimia 10 imekwisha lipwa TRA.
Marekebisho haya ya sheria yameanza kufanya kazi July 2022 pamoja na bajeti ya Serikali. Hivyo ni wajibu wetu kama wananchi kuiunga mkono Serikali yetu sikivu Kwa kuchangia mapato na kutii sheria bila shuruti.
Alamsiki
View attachment tz-act-2022-1-publication-document.pdf
Soma kifungu kilichobadilishwa hapa chini
Kabla ya madiliko hapa chini