Hii ndiyo sample ya wanafunzi tunaotaka wafaulu!!!... Huu mkoa (Singida)sijapata kuona

vanmedy

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
2,698
1,395
MVULANA mmoja mwanafunzi wa shule
ya Sekondari Chief Senge mkoani Singida
anashikiliwa jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma ya kumlawiti mtoto wa
kiume mwenye umri wa miaka minne.
Mvulana huyo Ibrahim Saidi (17)
anayesoma kidato cha tatu katika
Sekondari hiyo anatuhumiwa kutenda
unyama huo jana majira ya saa 12 jioni katika eneo la Majengo mjini Singida
baada ya kumwita mtoto huyo na
kumwingiza kwenye chumba
alichopanga kisha kumlawiti.
Ni mtoto wa kiume mwenye umri wa
miaka minne akieleza jinsi alivyoshawishiwa na mvulana aliyekuwa
mmoja wa wapangaji katika nyumba
anamoishi kisha kuingiliwa kinyume na
maumbile yake.
Mama mzazi wa mtoto huyo pamoja na
baadhi ya majirani waliokuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo
wanaeleza kilichotokea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida
kamishina msaidizi Geofrey Kamwela
amesema mtuhumiwa amekamatwa na
anatarajiwa kupandishwa kizimbani wakati wowote kujibu shitaka
linalomkabili.
Ingawa hali ya mtoto aliyelawitiwa
inaelezwa kuendelea vizuri baada ya
kutibiwa katika hospitali ya mkoa wa
Singida na kuruhusiwa, lakini ametakiwa kurejea tena kwa uchunguzi zaidi wa afya
yake.
Source: Habari Star TV Tanzania (facebook group)
 
Back
Top Bottom