Hii ndiyo ilikuwa 'thread' iliyomtoa Mzee Mohamed Said Knock out na kupoteza umaarufu?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,514
Nakumbuka kwenye jukwaa la historia kipindi cha nyuma ndugu yangu huyu mzee Mohamed Said alikuwa akijikumbia watu wengi sana katika kila bandiko lake katika jukwaa la historia ungeweza kukuta watu wakisoma mpaka pages 50+. lakini kwa sasa hali imekuwa mbaya sana.

Ni kama watu wamemwacha mzee huyu peke yake akiwa mnyonge na mwenye huzuni. Nimekuwa nikiwaza sana nini kilitokea? na katika kutafuta tafuta kwangu nikakutana na bandiko hili ambalo kwa kiasi kikubwa lilikuwa lenye madhara makubwa sana kwa mzee wangu huyu.

Ni bandiko ambalo watu waliokuwa wamenyamaza muda mrefu sana waliamua kutanabaisha yaliyomo ndani yao kwa maswali magumu na mepesi yenye ugumu kujibiwa na mzee wangu na mwishowe kumwacha akiwa katika hali hii mpaka hii leo.

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nimesikitika sana kwa sasa Maisha anayoishi mzee Mohamed Said yamekuwa ni ya mashaka,hofu na unyonge kutokana na kuwa mambo ambayo alikuwa anayaandika wadau waliamua kuya reveal uhalisia na kumpa changamoto kubwa sana ambayo hakuwahi itarajia. Watu wengi wakiwemo akina Nguruvi3 ,Mag3 na Mzee Mwanakijiji walimiminika nondo na uchambuzi yakinifu wakisadifu yaliyokuwepo kwenye maandiko ya mzee said mohamed.

FaizaFoxy alijitahidi sana kumsupport mzee wangu lakini bahati mbaya haya mambo kwa yeye yalikuwa juu ya uwezo wake hivyo akajikuta ni kama kamwachia mzee wangu peke yake na yeye kukaa kutafuta hoja za kitoto kwenye majadiliano ya watu wazima[/USER]hili lilikuwa ni pigo kali sana kwa mzee wangu ambaye toka kipindi hicho amekuwa akijitahidi kurudisha imani ya watu pasipo mafanikio. wafuasi wa mohamed said alikuwepo pia Mdondoaji na faiza foxy huyu alionesha dhahiri shahiri kwenye mjadala kuwa hakuwa akielewa kinachojadiliwa isipokuwa kudandia dandia vijimaneno na kutaka kuvifanya ni ajenda... alionesha kushindwa kwa kiasi kikubwa sababu alikuwa akisukumwa na mahaba,hisia na mipasho kuliko kuendesha mjadala kisomi.

Mkandara nilimtaja kimakosa katika kutetea alichokuwa akiandika mohamed said...mkandara alikuwa akiwasilisha mawazo yake kama mtu msomi, mtu huru asiyefungamana na upande wowote isipokuwa kwenye ukweli tu. kwa hili naomba ndugu yangu anisamehe.

nimesikitika kuwa huu ndo umekuwa mwisho wa mzee mohamed said... sikutegemea kuwa kuna watu walikuwa siku zote wamemwacha hivyo apande juu sana ili mwishowe wakija kumwangusha anguko lake liwe la kishindo kikubwa sana. nmesikitika sana kwa hili akina Nguruvi3, Mag3 , Mzee Mwanakijiji tukio ambalo mmelifanya katika thread hiyo ni la kikatili na lenye kuhuzunisha sana. nmeufuatilia mjadala mzima..haikupaswa mumuaibishe mzee wangu huyu kwa kumfanya kazi yoooote aliyofanya ionekane takataka mbele ya wasomi.
 
History ya mzee ime egemea kwenye udini. Kabla ya kumtaja mzee tambaza ya paswa kuwa tambua wazee wengine. Ana jenga hoja utafikili wazee wa gerezani pekee ndio wa mepigania Uhuru jambo ambalo si la kweli. Wa kimdharau Julius na kumuita wa kuja
 
Napitia clip za Nabii Sheikh Hamza Issa hapa akikiri njia, kweli na uzima
 
licha ya yote tukubali mzee yupo vizuri sanaaa, ku base kwenye hisia za kidini ndiko kunakomuharibia sana.
 
Ana udini sana mimi hata mada zake sisomi tena. Kila kitu waislamu wanaonewa wanaonewa kwani hao waislamu wao ni watoto wakubali kuonewa na kuchonganishwa.

Ila hizo pipo tatu Nguruvi3.Mag3.Mwanakijiji naxikubali mnooo zikitoa hoja
 
mzee mohamed said ni hazina kubwa sana hapa JF
Japo anamapungufu yake madogo(kutanguliza udini kwa kila jambo)
ila apewe heshima yake Kama mwanahistoria nguli kuwahi kutokea Tz, hii tabia ya sisi watoto wa jf kizazi kipya kutoa comments za hovyo kwa wazee wa JF sio njema sana
 
Back
Top Bottom