Hii ndiyo chanjo unayotakiwa kutumia

bernard10

JF-Expert Member
Apr 2, 2021
410
731
Chanjo ni maandalizi ya kibaolojia yanayolenga kuchochea uwezo wa mwili kajitengenezea antibodies na immunity(kinga) zinazosaidia kukabiliana na ugonjwa husika bila yenyewe (chanjo) kusababisha ugonjwa.faida za chanjo Ni nyingi ukiacha yamuhimu kabisa ambayo nikuokoa maisha ya watu faida nyingine nikutengeneza pesa nyingi kwa watengenezaji na faida nyingine nyingi za kiuchumia na kijamii.

SIFA ZA CHANJO UNAYOTAKIWA KUTUMIA KISAYANSI
mwanasayansi msomi au mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na Mimi zifuatazo Ni sifa za chanjo watanzania waafrika au watu mahali popote duniani tunatakiwa kuzitumia kwafaida yetu kiafya.

1. USALAMA(chanjo yoyote inatakiwa kuwa salama kwamaana haitakiwi yenyewe iwe chanzo Cha magonjwa au kifo).

2. ULINZI DHIDI YA MAGONJWA HUSIKA.(chanjo yoyote ili iitwe chanjo lazima iwe na uwezo wakumlinda mtumiaji dhidi ya ugonjwa au magonjwa husika).

3. UWEZO WAKUFANYA KAZI MUDA MREFU; chanjo yoyote lazima iwe na uwezo wakumlinda mtumiaji kwa muda mrefu miaka 40, 50 au zaidi bila kumletea madhara kiafya yamuda mrefu au mfupi.

4. UWEZO WAKUSABABISHA AU KUCHOCHEA UTENGENEZAJI WA(T-cells); ambazo nimuhimu katika ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa.

5. ZISIWE na MADHARA KABISA KAMA KIFO N.K
Kama yatakuwepo basi ni madogomadogo na kwamuda mfupi.

6. GHARAMA STAHIMILIVU au ZAKAWAIDA (gharama zinategemeana na watengenezaji na sababu nyingine lakini chamuhimu zisiwe zakibiashara zaidi kuzidi lengo madhubuti lakuokoa maisha ya watu.

7. UWEZO WAKUSTAHIMILI MABADILIKO YA KIBAOLOJIA NA KIJIOGRAFIA.


Hizi ni baadhi ya sifa chache za muhimu ambazo chanjo yoyote salama inatakiwa iwe nazo.je chanjo ulizowahi kutumia zina sifa hizo?? Au Chanjo ya Covid19 ambayo ndiyo habari ya mjini inazo hizo sifa?? Kama inazo basi nashauri tuzitumie kwa usalama wa Afya zetu nakuacha kufuata mikumbo au mihemko.Asante.
 
Umesahau sifa moja;
~ inatakiwa ifanyiwe majaribia siyo chini ya miaka miwili mpaka miaka kumi. Hii hudhihirisha ubora, na ufanyakazi wake kulingana na watu tofauti tofauti kulingana na mtengenezaji atakavyochagua
 
Ilitakiwa ufikie kwenye conclusion.

Chanjo dhidi ya Covid 19, kufuatana na taarifa za kitaalam, zina vigezo sawia zaidi hata ya hivyo ulivyoeleza, na zimehusisha majaribio mengi zaidi kabla ya kuruhusiwa kuanza kutumika, kuliko chanjo yoyote. Na wanaeleza iliwezekana vipi kwa muda mfupi.
 
Umesahau sifa moja;
~ inatakiwa ifanyiwe majaribia siyo chini ya miaka miwili mpaka miaka kumi. Hii hudhihirisha ubora, na ufanyakazi wake kulingana na watu tofauti tofauti kulingana na mtengenezaji atakavyochagua
Hayo majaribio kufanyika miaka miwili au kumi Nani alikwambia?
 
Hayo majaribio kufanyika miaka miwili au kumi Nani alikwambia?
Watu mbona povu linawatoka au Kuna maslahi mnayo kwenye hizo chanjo but lengo langu siyo kubeza mtu au watengeneza chanjo to speak the truth ingekuwa vizuri u base kwenye points
 
Watu mbona povu linawatoka au Kuna maslahi mnayo kwenye hizo chanjo but lengo langu siyo kubeza mtu au watengeneza chanjo to speak the truth ingekuwa vizuri u base kwenye points
Usione wivu watu kufaidi kutokana na Akili zao.Waliotengeneza chanjo watapiga pesa.Hiyo Ni faida ya kuwa na Akili.Watapiga pesa yes.Na kwa vile sisi tupo vizuri kwenye uchambuzi wacha wajanja watumie vichwa vyao kutengeneza faida.

Sisi Kama hatutaki kutengeneza tiba wao watatengeneza.Wanatumia Akili na pesa nyingi,Akili zao na pesa zao Lazima tulipie.
 
Back
Top Bottom