barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,865
Hii hali ya Bunge kutokuonyweshwa "Live" kuna hatari ya kuwa na tabia ya Wabunge "kulishwa" sana maneno kwa maslahi ya watu fulani.Hii ni sehemu ya mchango wa Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa juu ya utawala bora katika Bunge la 11
===========================================
Mchango kwa Bajeti ya Wizara ya Tamisemi, Utawala bora na Utumishi leo bungeni
1. Utawala Bora
Mheshimiwa Spika, nianze na utawala bora. Utawala bora ni kuongoza nchi kwa ufanisi na tija, kwa uwazi, uadilifu na uwajibikaji, kwa kushirikisha watu, na kwa kufuata utawala wa sheria. Niweke records sawasawa - miezi michache tangu Rais Magufuli aingie madarakani, tayari serikali imeshapoteza sifa zote za msingi za utawala bora.
• Kama ilivyosemwa kwenye hotuba ya Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani, leo serikali inafanya kazi kienyeji-enyeji bila hata kuwa na muongozo rasmi wa utendaji kwa wizara (instrument), kinyume kabisa na utawala wa sheria unavyotaka;
• Tulikuwa na Bunge la "live" sasa tuna Bunge la gizani; na badala ya kuvijengea uwezo vyombo vya habari ili vifanye kazi zake kwa ufanisi zaidi, serikali hii inayopenda kusifiwa bila kukosolewa imezidi kuminya uhuru wa vyombo vya habari na kulifuta kabisa Gazeti la Mawio
. Serikali ya Awamu ya Nne pamoja na udhaifu wake wote, bado haikufikia uwoga wa kuzuia Bunge lisiwe live. Vitendo hivi ni kinyume kabisa na dhana ya “Uwazi” na ambayo ndiyo sharti la msingi la utawala bora.
• Serikali hii inapata wapi uhalali wa kutuletea bajeti ya Utawala Bora, wakati tayari imeshaonyesha jeuri ya kupangua matumizi ya bajeti bila ridhaa ya Bunge? Tunajadili na kupitisha bajeti ili iweje wakati tayari Rais (Serikali) alishajipa mamlaka ya kuhamisha mafungu?
Mheshimiwa Spika, mbwembwe za “Kutumbua Majipu” na “Kauli za Hapa Kazi Tu” sio vigezo vya msingi vya “Uadilifu”. Duniani kote, kigezo cha kwanza na cha msingi kabisa cha uadilifu ni “Uwazi”. Serikali inayohofia uwazi ni serikali isiyojiamini na serikali isiyojiamini ni serikali isiyo na uadilifu.Serikali isiyofuata utawala wa sheria na isiyoheshimu kikamilifu hadhi na madaraka ya Bunge la wananchi katika kupanga na kutumia bajeti kama ilivyopitishwa, ni serikali iliyo kinyume kabisa na utawala bora. Ni bahati mbaya kuwa kinyume cha utawala bora ni udikteta. Siioni busara ya Bunge hili kupitisha bajeti ya Serikali yenye vijinasaba vya kidikteta.
Mheshimiwa Spika, utawala bora hautaki bajeti – bajeti si hitaji la msingi la kujenga utawala bora. Utawala bora unataka Utashi na Utayari wa Kisiasa ndipo uweze kustawi - It takes political consciousness and political will for the good governance to prevail. Siungi mkono Bajeti hii. Hatuwezi kujenga utawala bora na serikali inayokandamiza vyombo vya habari, inayoingilia hadhi na madaraka ya Bunge, na inayominya uhuru wa wananchi wa kupata habari katika namna waipendayo na iliyo muafaka zaidi kwao. Serikali inayotaka Bunge lijadili na kupitisha Bajeti ya Utawala Bora, wakati yenyewe haijali wala kuiheshimu misingi ya utawala bora, ni serikali inayojipanga kufuja na kuchezea fedha za wananchi bila huruma. Sipo tayari kubariki ufisadi wa aina hiyo. Serikali ya namna hiyo sio tu ni Jipu linalohitaji kutumbuliwa bali ni mithili ya Kansa inayohitaji kupigwa mionzi.
Mheshimiwa Spika, kwa miaka mingi Bunge limeidhinisha mabilioni ya shilingi kwaajili ya serikali kutekeleza programu mbalimbali na kuimarisha vyombo vinavyohusika na utawala bora. Lakini pamoja na pesa zote hizo, bado Tanzania imebaki nyuma sana katika kutimiza misingi ya utawala bora, ikiwa na mapungufu mengi. Nitaje baadhi;
• Bado huduma kwenye taasisi nyingi za umma zimekuwa zikitolewa chini ya ubora.
• Kumekuwa na matumizi mabaya ya vyombo vya dola hasa jeshi la polisi dhidi ya wananchi wasio na hatia na vyama vya upinzani na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
• Bado rushwa imetamalaki kwenye ofisi nyingi za umma.
• Hakuna Tume huru wala za haki za uchaguzi
• Bado ni marufuku kwa matokeo ya Rais kupingwa mahakamani hata kama alishinda kwa kuiba kura
• Hakuna uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari na Sheria zetu zimempa Waziri mwenye dhamana madaraka ya kimungu ya kukifungia au kukifuatilia mbali chombo chochote cha habari kwa kadri atakavyoona inafaa
• Hakuna mfumo mzuri na wenye nguvu wa kusimamiana baina ya mihimili na idara za serikali “checks and balances” wala mgawanyo wa madaraka “separation of power” unaofanya kazi kama inavyotakiwa. Kumekuwa na usiri katika utendaji wa mhimili wa serikali hasa katika uingiaji wa mikataba mikubwa ya uwekezaji na kudhohofisha wajibu wa Bunge wa kuisimamia na kuishauri serikali kwa niaba ya wananchi.
• Bado mahakama zetu hazipo huru vya kutosha kibajeti na kimaamuzi hasa kwenye uteuzi wa majaji – ni Rais ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ya uteuzi na sio Tume ya Mahakama
• Bado hakuna fursa sawa kwa Watanzania wote kupata haki zao kwenye vyombo vya kisheria. Watanzania masikini au wa kipato cha chini wanakandamizwa au kupoteza haki zao kwasababu ya kutomudu gharama za kufungua kesi au kufuatilia haki zao kwenye vya kisheria.
• Bado wananchi hawashirikishwi kikamilifu kwenye michakato ya maamuzi ya kimaendeleo na kidemokrasia kwenye maeneo yao.
Mheshimiwa Spika, kutopiga hatua kwenye utawala bora kunatokana na serikali kutokuwa na utayari wala utashi wa kutosha wa kujenga utawala bora. Kwa muda mrefu serikali imetengewe fedha nyingi lakini iliishia kufanya mambo madogo-madogo na yasiyo na tija sana katika kuimarisha utawala bora. Msingi wa kuondoa mapungufu mengi ya kiutawala ni kuandika katiba mpya na kufuta sheria zote kandamizi. Naionya serikali isifanye mchezo na utawala bora.
Udikteta ni ghali sana kuliko utawala bora. Nachukua fursa hii – kwa mara nyingine tena - kuitaka serikali ya Rais Magufuli kuturejesha haraka kwenye mchakato wa kupata katiba mpya. Serikali iache “kupotezea kwenye majipu” katiba mpya na iliyo bora ndiyo msingi wa maendeleo endelevu. Ni katiba mpya itakayosaidia kutumbuliwa kwa majipu mengi zaidi tena bila kubagua lipi litumbuliwe na lipi lisitumbuliwe; ni katiba mpya bora ndiyo itakayotupa fursa ya kusimika mifumo imara ya kisheria na kiutawala ya kudhibiti ufisadi na kuimarisha mfumo wa kusimamiana “checks and balances” utakaoleta matokeo makubwa ya uwajibikaji na huduma nzuri kwa wananchi. Naitaka Serikali itangaze kwenye Bunge hili ni lini hasa itaturejesha kwenye mchakato wa katiba mpya.
Niliwahi kusema na leo narudia tena;“Insanity is keeping doing the same thing in the same way …and expecting different results