Nakupongeza sana Kachero Mbobezi kwa makala nzuri iliyojaa ukweli na hoja kuhusu harakati za Lowasa kuwa Rais wa Tanzania. Wapinzani wa Lowasa wanayo hoja moja tu dhidi yake - Richmond. Hoja hii ni dhaifu sababu Lowasa hajawahi kuhojiwa na taasisi inayojitegemea (kamati ya bunge ni political platform) kama PCCB, Mahakama au Tume ya Maadili ya Uongozi n.k. Kwa hiyo watu wa 4umovement mkiweza kuipangua mapema kwa hoja na kuonesha takwimu kuhusu waliosababisha hasara kwa taifa mtakuwa mmewaziba midomo wapinzani wa kiongozi huyu. Taifa limeshuhudia vituko na "uadilifu" wa Mwakyembe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya Richmond, kwa kipindi kifupi katika Wizara ya Uchukuzi huko TPA, TRC n.k. mpaka akaletwa Sitta aliyekuwa Spika wakati wa Richmond aje asafishe uozo wa Mwakyembe! Wakati mwingine sarakasi za serikali ya CCM zinatisha.
Ni kichekesho cha mwaka kumuona mtu kama Sumaye, ambaye chini ya usimamizi wake ameliingiza taifa katika hasara ya matrilioni kwa kuuza nyumba za serikali na NBC kwa bei poa eti naye ni mpiganaji dhidi ya ufisadi! Kwa zaidi ya miaka minne mfululizo CAG ameanika ufisadi wa matrilioni TAMISEMI, UJENZI, MAMBO YA NJE, n.k. bila hatua za msingi kuchukuliwa dhidi ya wahusika. Hoja yangu hapa ni kwamba CCM hasa akina Nape na Mangulla wasitumie hoja nyepesi ya Richmond kumhujumu Lowassa eti ni fisadi. Angalau Lowasa alionesha mfano kwa kuwatimua City Water katika kipindi kifupi akiwa Prime Minister!
Makala kama hizi za Kachelo Mbobezi ni vema zisiishie Jamii Forum sababu watanzania wanalishwa kasumba ya kipuuzi eti fisadi katika nchi hii ni Lowasa kutokana na Richmond! Toeni ufafanuzi katika media zote na wafikie makundi ya vijana hasa vyuoni. Tengenezeni credible "game plan" ili kumuuza kwa umma Lowasa amabaye mpaka sasa he is by far the strongest front runner katika mbio za President wa Tanzania. Tukio la Arusha ni la kihistoria na CCM hawana sababu ya kuhangaika kumtafuta mgombea URAIS - Tayari wananchi na viongozi wamemaliza kazi hiyo.