Hii ndio safari ya matumaini

Hii ndio safari ya matumaini

budget

Member
Joined
Feb 23, 2015
Posts
42
Reaction score
27
"HII NDIO SAFARI YA MATUMAINI"

Tarehe 30/5/2015 Mh Edward Ngoyai Lowassa alizindua rasmi safari Ya Matumaini kwenye Uwanja wa Shekhe Amri Abeid uliojaa maelfu ya Watanzania waliokuwa na Shauku ya kuona Safari hii ikiianza rasmi baada ya kuwekewa vikwazo mbalimbali.

Safari iliyoanza miaka saba nyuma,nakumbuka Mwanzo Wa Safari hii tarehe 7/2/2008 Jioni ya siku ambayo Mh Edward Lowassa alipojiuzulu kwa kutimiza Dhana ya Kuwajibika kwa Serikali yake,Chama chake na Watanzania aliokuwa anawaongoza kutokana na Makosa YA Watendaji waliokuwa chini yake.

"Wana Monduli tunashukuru kwa Heshima ya kumchagua na kuendelea kuwa na Imani nA Mh Edward Lowassa,sasa tunaomba tuwape kazi ya Kumtunza na Kumuombea kwa Mungu awe na afya njema,jukumu la kumuingiza Edward Ikulu mwaka 2015 tutalifanya sisi Marafiki zake tukishirikiana na Watanzania nchi nzima,tutawaeleza ukweli kuhusu Sakata la Richmond,Edward Lowassa hausiki kwa namna yeyote,lazima tuhakikishe Watanzania wanaujuwa ukweli"

Moja ya kauli za kishujaa zilizotolewa usiku wa safari ya Matumaimi 1/1/2014.

"Hii ndio Safari ya Matumaini"

Tukio la kujaa kwa Uwanja wa Shekhe Amri Abeid na wengine kukosa nafasi na kulazimika kubaki nje,Mamia ya Watanzania kufuatilia kwenye Vyombo vya Habari imedhihirisha Imani na mapenzi ya Watanzania kwa Mh Edward Lowassa.

"Hii ndio safari ya Matumaini"

Licha ya Propaganda,kashfa za Uongo na uzushi wa aina Mbalimbali ulionezwa na unaonezwa na maadui na wapinzani wenye chuki wa Mh Lowassa kwa Watanzania lakini bado Watanzania hawa hawa waliendelea kuwa nA Imani,Matumaini na Upendo kwa kiongozi wao Mh Edward Lowassa.

Watanzania hawa hawa Maelfu kwa Maelfu wanaujuwa ukweli, wanajuwa wapo wasiolitakia mema Taifa hili,Wanajuwa udhaifu wa Viongozi wa Taifa hili Kiuongozi,Wanajuwa Uwezo Edward Lowassa Kiuongozi, Wanajuwa Maono ya Edward Lowassa kwa Taifa lake,Wanaijuwa Dhamira ya Edward ni Kuwakomboa Watanzania kuondokana na Umaskini nA Wanafahamu Kiu na Ndoto ya Edward katika kuwaletea Wananchi wa Tanzania Maendeleo.

"Hii ndio Safari ya Matumaimi"

Wingi ule wa Watu ndani ya Uwanja wa Shekhe Amri Abeid Umetoa Majawabu ya Watanzania Kwa Maadui wa Edward Lowassa,Umejibu na Kuonesha Upendo Wa dhati na wa Kweli wa Watanzania kwa Kiongozi wanayemtaka na waliyemsubiri kwa Muda Mrefu.

Wingi Ule Uliwadhihirishia na kutoa majawabu ya dhana zao wanazojaribu kuzijenga Nappe Nwuye,January Makamba,Mangula,Prof Mwandosya,Bernard Membe na wale wote wanodhani Lowassa hununua watu,Umati ule haukuvutwa na pesa bali ni Mapenzi yao wenyewe Watanzania kwa Edward Lowassa wakiamini ndio Kiongozi anayefaa kuliongoza taifa hili kwa miaka mitano ijayo,Watanzania wa sasa hawaitaji pesa kumjuwa kiongozi bora,Watanzania wa sasa wanamjuwa Kiongozi bora wanayemtaka.

Watanzania wanajuwa Edward Lowassa hana pesa ya kuwanunua Watanzania wote.

Watanzania wa sasa Wanajuwa Umati ule ni Wa Watanzania wenye Mapenzi,Upendo na Imani na Edward Lowassa naye.

Edward Ngoyai Lowassa ana Marafiki wengi kila Mkoa,Wilaya,Kata,Vijiji,Mtaa na Shina ndani ya Nchi hii.

Turejee hii kauli"Umati huu unanikbusha enzi za Tanu,Enzi za Baba wa Taifa alipokuwa anaenda au kurudi kutoka Marekani kudai uhuru"

"Hii ndio safari ya Matumaini"

Mimia ya Watanzania walikubali kuachana na shughuli zao,kutembea umbali mrefu na kulala njiani kwenye magari ili kuungana na Mh Edward Lowassa katika uzinduzi wa Safari ya Matumaini.

Nilishangazwa na Uwepo wa Bibi Mzee wa Miaka 92 Kutoka Mkoani Tabora ambaye naye hakutaka kukosa Safari Hii YA Matumaini.

Bibi huyu alinielezea kuja kwake ni kutokana na Kuoteshwa kuwa Rais wa awamu ya 5 wa Taifa hili atakuwa ni Mh Edward Lowassa.

"Hii ndio Safari ya Matumaini"

Wapo waliolala njiani,wapo waliolala ndani ya Uwanja baada ya kukosa sehemu za kulala kutokana na kujaa kwa nyumba za Wageni licha kuwa nA baridi na Manyunyu ya Mvua na wapo waliolala nje ya Mji wa Arusha, Kilimanjaro, Babati na Manyara; hii yote ni kuhakikisha wanamuunga Mkono Edward Lowassa katika safari ya Matumaini.

"Hii ndio Safari ya Matumaini"

Njiani Askari wa barabarani waliungana na Umati wa Watanzania waliokuwa njiani kuelekea Arusha kutoka Mikoani kwa kuwatakia Safari njema na wengine kutoa salamu zao za Safari ya Matumaini kwa Mh Edward Lowassa.

"Hii ndio Safari ya Matumaini"

Wingi wa Viongozi wa Dini, Vyombo vya Habari,Wingi wa WaNec,Wajumbe wa Halmashauri kuu,Wenyeviti wa chama wa Mkao,Wilaya,Viongozi Wastaafu,Wabunge,Wajumbe wa Kamati kuu nA Viongozi wa Wengi wa Jumuia ya Vijana wa chama,Wazee maarufu na Wasanii Mbalimbali,hii inaonyesha nguvu ya Upendo na Ushawishi aliyonayo Mh Edward Lowassa kwa Watanzania.

"Hii ndio Safari ya Matumaini"

Naikumbuka hii kauli ya Mzee Mmoja ndani YA Uwanja "Siamini kama pesa yake ndio imeujaza huu uwanja, Lowassa hana pesa za kuupa umati wote huu, kuna namna nyingine lakini sio pesa kama wanavyodai na hii ni Arusha tu, hapa si pana watu wa CAHDEMA hapa leo, imekuaje? Kwa umati huu, huyu ndiye rais wa tano wa Tanzania hamna kipingamizi wamuache tu"

Mwingine"Huyu Jamaa anasubiri kuapishwa tu"

"Hii ndio safari ya Matumaini"

Hotuba ya Safari ya Matumaini,Moja hotuba nzuri iliyoandaliwa kitalaamu na iliyofanyiwa utafiti wa kutosha Inchi nzima,Hotuba iliyotoa majawabu ya Changamoto nyingi zinazowakabili Watanzania kwa miaka Mitano Ijayo,Hotuba iliyotoa dira ya Mtanzania,hotuba iliyokidhi matakwa ya Mtanzania, hotuba inayoonyesha Matumaini kwa Mtanzania aliyekatika lindo la Ufukara na umaskini kwa Muda Mrefu.

Hotuba iliyozingatia Makundi ya Watanzania wa aina zote,Hotuba iliyotoa Matumaini kwa Vijana,Wakulima,Walimu,Mama lishe,Bodaboda,Wahudumu wa afya,wachimbaji wadogowadogo Wa madini n.k

"Hii ndio Safari ya Matumaini"

Vijana maarufu na wenye ushawishi wa kundi kubwa la Marafiki Wa Lowassa wanajulikana kama 4UMOVEMENT FRIENDS OF LOWASSA,walitokwa na machozi ya furaha kuona Mwitikio mkubwa wa Watanzania walioungana nao kwa Kiongozi wanayempigania Kiongozi wanAyeamini ndiye aliyebeba Matumaini yao.

Vijana hawa waliifanya kazi kubwa ya kuelelezea ni kwanini Vijana na Wazee wana Imani na Edward Lowassa,ni Kwa nini Edward Lowassa ndio jawabu na suluhisho la matatizo ya Watanzania,hakika wana haki ya kutokwa na Machozi ya Furaha kwa Matokeo mazuri YA Kazi yao waliyoifanya kwa shida na dhiki,milima kwa mabonde lakini yote ni Katika kumkomboa Mtanzania kuondokana na Umaskini kupitia Edward Ngoyai Lowassa.

"Hii ndio Safari ya Matumaini"

Katika Safari hii ya Matumaini Edward amepitia Vikwazo vingi,wapo waliojaribu kupanga njama za kumuua,wapo waliotaka kuona akikatwa jina na Vikao vya Chama,wapo wanaotamani ardhi immeze Edward Lowassa,wapo Wanaotamani Chama kifute uanachama wa Edward,wapo wanaotamani Watanzania wamgeuke Edward Lowassa.

Lakini naomba kuwaambia Edward Lowassa ni chaguo la Mungu kwa Watanzania,Edward Lowassa ni Dhahabu lazima ipite kwenye Moto.

"Hata Yesu wa Nazareti alisulubiwa kabla ya kuja kuwakomboa wana wa Israel"

"Hii ndio Safari ya Matumaini"

Safari yeyote haikosi Vikwazo na Safari yeyote haikosi Wasindikizaji, tusitishwe na utitiri wa Watangaza Nia na Tusijawe na Chuki Tuwafurahie kwa maana ndio wanaomsindikiza Edward Lowassa katika safari yake ya Matumaini kuelekea Ikulu tarehe 25 Mwezi wa 10 mwaka huu 2015.

"Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, sauti ya umma ni sauti ya Mungu"

"Edward Ngoyai Lowassa ni wengi , ni sauti ya umma, ni sauti ya Mungu"

"Lowassa ni chaguo la Mungu kwa Watanzania"

"Hamna anayeweza kuzuia Mafuriko kwa Mikono"

Mti wenye Matunda siku zote hupigwa Mawe,hivyo katika Safari hii ya Matumaini tutakutana na Vikwazo vingi, tusirudi nyuma na tusikate tamaa, mapambano yaendelee mbele kwa mbele.

"Edward Ngoyai Lowassa atakuwa Rais wa 5 WA Tanzania kupitia Chama cha MapinduzI ( CCM)"

"Edward Lowassa atakuwa wa Mwisho kuhama ndani ya CCM"

"Kama humtaki Edward Lowassa ndani ya CCM basi hama wewe".

Na Askofu Gwajima anasema hivi"Kama humpendi Edward Lowassa uende ukalambe Ndimu"

"Uende ukalambe.nini........?"

HII NDIO SAFARI YA MATUMAINI

Kaa tayari kungojea Sehemu ya Pili ya Safari ya Matumaini!!!

Salaaaaaam!
Kachero Mbobezi
4umovement

 
Tunataka 'Safari ya UHAKIKA' sio 'Safari ya MATUMAINI'. Masuala ya kuishi kwa matumaini waachieni wagonjwa wa UKIMWI.

Tanzania ni tajiri kwa raslimari nyingi sana, tunataka UHAKIKA/UTHABITI wa UONGOZI tu.
 
Lowasa ni rais anaesubiri kuapishwa October
 
Mwalimu Nyerere alisema "Hapa hatumchagui mtu maarufu ,tunamchagua mtu safi na huyu si safi ambaye hapo alimlenga Lowasa. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine wanasema aah ni tuhuma tu.

Samueli Sitta]Yusufu Makamba ]mnasisima hapa mnasema ni tuhuma ,tuhuma tu. Lakini mtakumbuka mke wa kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha ,akasema mke wa kaisari hapaswi hata kutuhumiwa.

Na sisi hapa mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa. Wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope ndio nimuombee kura, hapana kabisa. Huyu mimi namjua si msafi na nchi nzima inajua siyo msafi. Hafai kuwa mgombea wetu" Mwl.Julius Nyerere, NEC Dodoma ,Juni 1995.

Nimeona niandike hayo maneno hapa kwani yana faida kubwa sana kwa Watanzania wanaiotakia mema nchi yetu. Nyerere hayupo duniani tena lakini maneno yake na wosia wake utaendelea kudumu daima.

CCM lazima mtambue IKULU SIYO PANGO LA MAFISADI . CCM lazima mtambue IKULU SIYO WODI YA WAGONJWA. CCM lazima mtambue Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Watanzania wanataka mabadiliko, wakiyakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM, sasa ni wakati muafaka kwa Watanzania kutafuta mabadiliko nje ya CCM.
 
Toen hiz habari maana leo nimeota zaidi ya wabunge 150 waliokuwa pamoja na Lowasa wakimsaliti nakukirudia chama, nimeota Lowasa akikatwa jina mchana kweupe
 
Sasa mwambie mzee aseme,kama yeye sio mnufaika wa iliyokuwa RICHMOND,ni nani aliyekuwa ananufaika nayo

Tunajua yeye alitolewa kafara,sasa asizunguke zunguke tu aseme,ajitoe tu aseme,hata kama atachukiwa yeye aseme tu,sisi wananchi tutamuona ni shujaa wetu

Lakini hivyo anavyoendelea kukataa sio yeye lakini mwenyewe hasemi(kwa sababu RICHMOND ilikuwapo,sio nadharia ile)
 
Ni hatari sana kuishi kwa matumaini kuliko uhalisia.... Mpoto aliwahi kuimba akasema Life is a Performance and not a Rehearsal
 
Nape ameshaandaa rungu tayari kwa kuua panya
 
Ingekuwa china hyu El angekuwa marehemu nw tungewaza mambo mengne kabsa ya maendeleo...Endeleeni na matumain yenu
 
Huyo aliyebuni hii kauli mbiu,ndiye aliyemmaliza mamvi,Hata kampeni hazijaanza,kauli mbiu imeshaanza kushambuliwa,kampeni zikianza itakuwaje?
 
Huyo aliyebuni hii kauli mbiu,ndiye aliyemmaliza mamvi,Hata kampeni hazijaanza,kauli mbiu imeshaanza kushambuliwa,kampeni zikianza itakuwaje?

Kauli mbiu huwa ni ya chama sio mgombea
 
Nakupongeza sana Kachero Mbobezi kwa makala nzuri iliyojaa ukweli na hoja kuhusu harakati za Lowasa kuwa Rais wa Tanzania. Wapinzani wa Lowasa wanayo hoja moja tu dhidi yake - Richmond. Hoja hii ni dhaifu sababu Lowasa hajawahi kuhojiwa na taasisi inayojitegemea (kamati ya bunge ni political platform) kama PCCB, Mahakama au Tume ya Maadili ya Uongozi n.k. Kwa hiyo watu wa 4umovement mkiweza kuipangua mapema kwa hoja na kuonesha takwimu kuhusu waliosababisha hasara kwa taifa mtakuwa mmewaziba midomo wapinzani wa kiongozi huyu. Taifa limeshuhudia vituko na "uadilifu" wa Mwakyembe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya Richmond, kwa kipindi kifupi katika Wizara ya Uchukuzi huko TPA, TRC n.k. mpaka akaletwa Sitta aliyekuwa Spika wakati wa Richmond aje asafishe uozo wa Mwakyembe! Wakati mwingine sarakasi za serikali ya CCM zinatisha.

Ni kichekesho cha mwaka kumuona mtu kama Sumaye, ambaye chini ya usimamizi wake ameliingiza taifa katika hasara ya matrilioni kwa kuuza nyumba za serikali na NBC kwa bei poa eti naye ni mpiganaji dhidi ya ufisadi! Kwa zaidi ya miaka minne mfululizo CAG ameanika ufisadi wa matrilioni TAMISEMI, UJENZI, MAMBO YA NJE, n.k. bila hatua za msingi kuchukuliwa dhidi ya wahusika. Hoja yangu hapa ni kwamba CCM hasa akina Nape na Mangulla wasitumie hoja nyepesi ya Richmond kumhujumu Lowassa eti ni fisadi. Angalau Lowasa alionesha mfano kwa kuwatimua City Water katika kipindi kifupi akiwa Prime Minister!

Makala kama hizi za Kachelo Mbobezi ni vema zisiishie Jamii Forum sababu watanzania wanalishwa kasumba ya kipuuzi eti fisadi katika nchi hii ni Lowasa kutokana na Richmond! Toeni ufafanuzi katika media zote na wafikie makundi ya vijana hasa vyuoni. Tengenezeni credible "game plan" ili kumuuza kwa umma Lowasa amabaye mpaka sasa he is by far the strongest front runner katika mbio za President wa Tanzania. Tukio la Arusha ni la kihistoria na CCM hawana sababu ya kuhangaika kumtafuta mgombea URAIS - Tayari wananchi na viongozi wamemaliza kazi hiyo.
 
Lowasa ni rais anaesubiri kuapishwa October

Maamuzi.JPG
:confused2:
 
mi nawambia nyie mliokula hela za yule mzee atawalaan sanaa...lile lilikuwa tamasha la mziki sio kutangaza nia....kwani sisi ni wagonjwa mpaka aatuambie safari ya matumaini?!! yeye ndio mgonjwa anayeishi kwa matumaini..sasa ugonjwa wake asituambukize watanzania 45 mil....
 
Back
Top Bottom