Hii ndio Kauli ya Asia baada ya kushindwa ukonga

Mwaka mpya

JF-Expert Member
Jun 12, 2016
213
221
Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa (CHADEMA) Jimbo la Ukonga Asia Msangi ametoa kauli yake ya kwanza kuwa alitegemea kushindwa uchaguzi huo ikiwa ni saa chache tangu Msimamizi Mkuu wa uchaguzi wa Jimbo hilo kumtangaza Mwita Waitara kuwa mshindi wa jimbo hilo kwa kura 77795.

Akizungumza na www.eatv.tv Asia Msangi ameeleza alipokea taarifa kuwa angeshindwa uchaguzi huo kutoka kwa wapiga kura wake kwa kile alichokidai kuhujumiwa katika baadhi ya vituo vya kura ikiwemo kuzuiliwa kwa mawakala wake huku zoezi la kupiga kura likiwa linaendelea.

“…ulimwengu wote umeona mambo yaliyofanyika Ukonga, kwa sababu hata kabla ya uchaguzi nilipokea taarifa kuwa Asia hutoshinda.., wameamua kumuweka yeye (Waitara) ndio mbunge wacha wamuweke lakini Ukonga wameona anaewafaa ni nani? . wengi walinipigia simu kwamba hawapigi kura kwa sababu mawakala wangu waliwasumbua tangu saa 12 asubuhi.”

Uchaguzi huo ulihusisha wagombea 14 akiwemo Murshidi kabilinga (NRA) aliyepata kura 6, Kimosa Mohamed (UMD) kura 16, Rajabu Rashindi (NLD) kura 16, Mbwana Kibanda (UPDP) kura 17, Ngubi Ramadhani (ADC) kura 17, Kuzenga Faustine (UDP) kura 23, Kiambo Richard (CCK) kura 74, Nelbert Obatia wa NCCR-Mageuzi kura 27, Kisena Lucas (SAU) kura 40, Rehema Nasoro Chama cha Wakulima 91, Salama Masoud (CUF) kura 405, Asia Msangi wa CHADEMA kura 8676 na Mwita Waitara wa CCM kura 77795.

Kwa mujibu Msimamizi wa Mkuu wa uchaguzi jimbo hilo lilikuwa na wapiga kura 300,609 lakini waliojitekeza ni wapiga kura 88,270 tu ambao ni sawa na asilimia 29 ya wapiga kura waliojiandikisha.
CHADEMA%2B2%2BPIC0.jpg
 
Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa (CHADEMA) Jimbo la Ukonga Asia Msangi ametoa kauli yake ya kwanza kuwa alitegemea kushindwa uchaguzi huo ikiwa ni saa chache tangu Msimamizi Mkuu wa uchaguzi wa Jimbo hilo kumtangaza Mwita Waitara kuwa mshindi wa jimbo hilo kwa kura 77795.

Akizungumza na www.eatv.tv Asia Msangi ameeleza alipokea taarifa kuwa angeshindwa uchaguzi huo kutoka kwa wapiga kura wake kwa kile alichokidai kuhujumiwa katika baadhi ya vituo vya kura ikiwemo kuzuiliwa kwa mawakala wake huku zoezi la kupiga kura likiwa linaendelea.

“…ulimwengu wote umeona mambo yaliyofanyika Ukonga, kwa sababu hata kabla ya uchaguzi nilipokea taarifa kuwa Asia hutoshinda.., wameamua kumuweka yeye (Waitara) ndio mbunge wacha wamuweke lakini Ukonga wameona anaewafaa ni nani? . wengi walinipigia simu kwamba hawapigi kura kwa sababu mawakala wangu waliwasumbua tangu saa 12 asubuhi.”

Uchaguzi huo ulihusisha wagombea 14 akiwemo Murshidi kabilinga (NRA) aliyepata kura 6, Kimosa Mohamed (UMD) kura 16, Rajabu Rashindi (NLD) kura 16, Mbwana Kibanda (UPDP) kura 17, Ngubi Ramadhani (ADC) kura 17, Kuzenga Faustine (UDP) kura 23, Kiambo Richard (CCK) kura 74, Nelbert Obatia wa NCCR-Mageuzi kura 27, Kisena Lucas (SAU) kura 40, Rehema Nasoro Chama cha Wakulima 91, Salama Masoud (CUF) kura 405, Asia Msangi wa CHADEMA kura 8676 na Mwita Waitara wa CCM kura 77795.

Kwa mujibu Msimamizi wa Mkuu wa uchaguzi jimbo hilo lilikuwa na wapiga kura 300,609 lakini waliojitekeza ni wapiga kura 88,270 tu ambao ni sawa na asilimia 29 ya wapiga kura waliojiandikisha.View attachment 868997
Hakuna ustaarabu mzuri kama kukubali kushindwa ili uweze kufanya tathmini na kuweka mikakati ya ushindi kwenye chaguzi zijazo. Tatizo kubwa kwenye demokrasia changa ni hili la kulalamika wanaposhindwa.
Algore alijezewe mizengwe mingi na republican kwenye uchaguzi lakini mwisho wa siku alikubali kushindwa na kwenye uchaguzi uliofuata democrats walishinda. CHEZA MUZIKI NA ACHA KULALAMIKA
 
Chaguzi za marudio Huwa hazina watu wengi Pia ujue wengi walijiandikisha ili wawe Na kitambulisho tu wakienda benki nk wengi hawakuchukua kwa ajili ya kupigia kura.
Pamoja na yote hayo inajidhirisha wazi kuwa tupo tired sana
 
KWANI KULEWA NDIO KIPAUMBELE CHAKE HADI M UMHUSISHE NAYO, mwache atafute hela mume atakuja tu
 
Chaguzi za marudio Huwa hazina watu wengi Pia ujue wengi walijiandikisha ili wawe Na kitambulisho tu wakienda benki nk wengi hawakuchukua kwa ajili ya kupigia kura.
Hivi kauli hii inasadifu na uhalisia wa waliojitokeza Monduli?
 
Chadrama chama la wapigaji, walikua wanamtafutia nafasi m_chagadema mwenzao. Akagombee huko kwao
 
Back
Top Bottom