Crew ya kwanza ya wanasayansi walitua ISS tayari kwa kuanza kazi rasmi lkn wkt huo ilikuwa bado haijamalizika vizuri! ila kwa matumizi ya binadamu ilikuwa salama,ISS imemalizwa kuundwa rasmi mwaka 2011 ikiwa na science labs,vyumba,choo na bafu,sehemu ya mazoezi,jiko n.k..
ISS inatumia solar ili kupata nguvu ya kujiendesha,ambapo solar hizo hutegemea mwanga wa jua ili kupata joto na kulibadili joto hilo ktk mfumo wa umeme,kisha umeme huo huifadhiwa ktk battery tatu kubwa zijulikanazo kama nickel hydrogen battery,hizi hutumika kusambaza umeme hasa pale ISS inapokuwa imekingwa na dunia ama kivuli cha dunia kinakuwa kinapiga ISS hivyo kufanya mwanga wa jua kutokufika vyema..toka dunia mpk ISS ni mile 240,
pia ISS huzunguka dunia kwa dk 90 kwa kasi ya 17,500 mph,kwa kasi hii ISS inaweza toka duniani mpk kwenye mwezi kwenda na kurudi kwa masaa 24.
maisha ktk ISS ni tofauti ukilinganisha na duniani kwani huko ilipo haiathiriwi sana na nguvu ya uvutano ya dunia hivyo vitu huelea! hii pia imekuwa moja kati ya kivutio