ABEL MAGEMBE LUGIMBA
Member
- May 22, 2016
- 63
- 59
USHAURI WANGU KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Katika kudhibiti utovu wa nidhamu wa baadhi ya wabunge wanaofanya Fujo mbalimbali Bungeni na kupelekea hadhi ya Bunge kushuka, Kama mwananchi wa kawaida napendekeza yafuatayo yaongezwe katika kanuni za kudumu za Bunge zinazohusu adhabu pindi Mbunge anapofanya makosa yanayoshusha hadhi ya Bunge letu Tukufu :-
1.Adhabu kwa Mbunge anayesimamishwa Bungeni iongezwe mara dufu, kwa kuwa Wabunge wanaosimishwa Bungeni wanapoenda kwa wananchi wamekuwa wanapotosha sana kuhusu sababu za wao kupewa adhabu. Kuhusu suala hili napendekeza yafuatayo yafanyike katika kurekebisha suala hili, nashauri Mbunge asipewe posho pamoja na Mshahara wake ukatwe wote, pia azuiliwe asifanye mkutano wowote ule wa kisiasa Jimboni kwake au sehemu nyingine pamoja na kuzuiliwa kuongea na Vyombo vya habari kwa kipindi chote atakachokuwa anatumikia adhabu yake.
2.Mbunge azuiliwe kufanya shughuli zozote zile za kibunge katika kipindi chote atakachokuwa anatumikia adhabu aliyopewa na Bunge.
3.Wabunge wanaoingia Bungeni na kusign mahudhurio halafu wakatoka bila kufanya kazi yoyote ile wahesabike sawa na watoro au watumishi hewa, hivyo basi hawatakiwi kupewa posho hata kidogo pia wanatakiwa kulipwa nusu ya mishahara yao.
Yakifanyika haya naamin heshima ya Bunge itarudi.Adhabu yoyote ile malengo yake huwa ni kubadilisha tabia ya mtu na sio kumkomoa.Ahsanteni
By Abel Magembe Lugimba.