Hii ndio CCM ya Kinana: Nape-Mwanza, Mwigulu-Moro, Mboni-Arusha na Makonda-Geita

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Hakika hiki ndicho chama cha mapinduzi ninachokifahamu. Kipo kila sehemu na viongozi wake wanawajibika..kuanzia kwenye Chama Chanyewe mpaka kwa jumuiya zake. Jana tumepata taarifa juu ya muendelezo wa ziara za Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo kutokana na ziara hiyo Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Tandahimba alijiunga na CCM.

Leo viongozi wa Chama, katibu wa Uenezi ndg Nape yupo Nyamagana mwanza kumpokea aliyekuwa kiongozi wa Chadema na Rais wa Chuo kikuu cha SAUT Ndg Dova Mcheshi.

Wakati hayo yakiendelea Naibu Katibu Mkuu bara ndugu Mwigulu nchemba yeye yupo katika mkutano wa Hadhara katika Mji wa Morogoro.

Lakini pia viongozi wa jumuiya ya Vijana hawako nyuma kwani Makamu Mwenyekiti wa UVCCM ndg Mboni Mhita alikuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika jiji la Arusha na Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa jumuiya hiyo Ndg Makonda Paul yupo Mkoani Geita akihutubia umma wa watanzania kuwaeleza wananchi hatua iliyofikiwa na CCM katika kuisimamia Serikali katika utekelezaji wa Ilani yake.

Kama hiyo haitoshi nae Mbunge wa Chalinze Ndugu Ridhwan Kikwete yupo Mkoani Morogoro akizungumza na wanavyuo wa mkoa huo.

Hii ndio CCM, najua ikifika 2015 watasema kuna makontena ya kura yameingizwa kutokea Rwanda. Hawa jamaa sometimes hawako serious kabisa..kuna ombwe kubwa la uongozi katika vyama vya upinzani hapa nchini.
 
Attachments

  • IMG-20140608-WA0018.jpg
    IMG-20140608-WA0018.jpg
    65.4 KB · Views: 1,173
  • IMG-20140608-WA0017.jpg
    IMG-20140608-WA0017.jpg
    81.8 KB · Views: 1,110
  • IMG-20140608-WA0004.jpg
    IMG-20140608-WA0004.jpg
    48.3 KB · Views: 1,032
  • IMG-20140608-WA0010.jpg
    IMG-20140608-WA0010.jpg
    44.2 KB · Views: 1,015
  • IMG-20140608-WA0024.jpg
    IMG-20140608-WA0024.jpg
    128.7 KB · Views: 1,024
Hii yote ni presha ya Ukawa Chezea UKAWA.

CCM haifanyi kazi zake kwa presha..ni chama chenye historia ya kupanga na kuratibu mipango yake kwa ustadi wa hali ya juu.

UKAWA haina tofauti na operesheni sangara, M4C na nyinginezo, ni tukio tu kama matukio mengine yakiisha muda wake litaondoka.
 
CCM ni chama cha kilaghai! By the way, yale maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?
 
Mtaruka ruka sana magamba ila mwisho wenu umewadia,no way out you have to surrender!
 
CCM haifanyi kazi zake kwa presha..ni chama chenye historia ya kupanga na kuratibu mipango yake kwa ustadi wa hali ya juu.

UKAWA haina tofauti na operesheni sangara, M4C na nyinginezo, ni tukio tu kama matukio mengine yakiisha muda wake litaondoka.

Mkubali moto wa UKAWA kwenu,kwani unawafanya vizuri? Kazi mnayo,tena kubwa kweli kweli.
 
Mimi naomba kuwauliza CCM... Mnawauzia wananchi products zipi? Maisha bora? Ukuaji wa Uchumi? Ujangili? Ufisadi? Maisha magumu? Rushwa? Mishahara Duni? Elimu Duni? Afya bora?... Mna nini hasa ya kuwauzia wananchi?... I'm curious ...
 
Baambie, hakijibu haya maswali najiunga na ccm.
 
Wala haitumii nguvu kubwa kama chadema kuitisha mikutano, wala haihitajiki majina makubwa mkutanoni, hata ukisimamisha nembo tu ya ccm watu wanajaa! Ukawa mjinyonge tuuu!.
 
Mimi naomba kuwauliza CCM... Mnawauzia wananchi products zipi? Maisha bora? Ukuaji wa Uchumi? Ujangili? Ufisadi? Maisha magumu? Rushwa? Mishahara Duni? Elimu Duni? Afya bora?... Mna nini hasa ya kuwauzia wananchi?... I'm curious ...

kamakonda kanabamiza kale. hee
 
Mimi naomba kuwauliza CCM... Mnawauzia wananchi products zipi? Maisha bora? Ukuaji wa Uchumi? Ujangili? Ufisadi? Maisha magumu? Rushwa? Mishahara Duni? Elimu Duni? Afya bora?... Mna nini hasa ya kuwauzia wananchi?... I'm curious ...

Siku hizi nacho ni chama cha upinzani kina lalamikia serekali.
 
Siku hizi nacho ni chama cha upinzani kina lalamikia serekali.

What? sijaelewa Mkuu... Ngoja tupate majibu kutoka kwa wahusika! Nape ataweza kutusaidia juu ya products zao wanazo wauzia wananchi...kama wanalalamika itakuwa wanakosea sana maana serikali iliyoko madarakani ni yao na Mkuu wa nchi ndiye Mwenyekiti wa CCM ...
 
Mtaruka ruka sana magamba ila mwisho wenu umewadia,no way out you have to surrender!

Hayo Maneno ya Mwisho wa CCM umewadia walianza kusema Wifi zako 1995 Wakati wa Mrema, 2000 wakati wa Lipumba, 2005 wakati wa Mbowe,2010 Wakati wa Slaa na yanaendelea kusemwa tena inavokaribia 2015, na mara zote tukisema kuwa hizo ni ndoto za Mlinzi wa Usiku mnabisha yetu macho.

Ikifika 2015 Mbowe atamtapeli tena Slaa agombee Urais huku akijua hawezi kushinda ili yeye Mbowe apate tena fursa ya kuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni ili aendelee kutafuna Vitafunwa kwa kuwa Slaa hatokuwa Mbunge hivo hawezi kufikiriwa kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni.
 
samahani Tandale One.

CCM hakuna ubishi kwa ccm ni chama kubwa hapa nchini lakini ni lazima tufike mahal tuwe wazi kwamba vyama vya upinzani kwa kiwango kikubwa vimefanya Sasa walau mambo yanakwenda!

kubwa hapa tuombe uzima tu hivi vyama viendelee kuwepo ili kuitia presha ccm ili iwatumikie wananchi nasio kulala!
 
Wakati UKAWA wamejikita kwenye kuwaelezea wananchi matatizo yao, CCM inapita kona hadi kona kuhakikisha matatizo ya wananchi yanaendelea kutatuliwa kwa haraka iwezekenavyo. Hatukatai Changamoto zipo pia hazijashindwa kupatiwa majibu.
 
Back
Top Bottom