Nchi hii ilichezewa sana, au nchi hii itachezewa sana?

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,189
17,157
Hayo maneno manee ya kwanza katika kichwa cha mada hii sio mageni kwetu, na wala sitopenda kuyaandikia kwa kirefu juu yake.

Haya manne niliyoongeza mimi, hata kama yanafanana na yale ya mwanzo, yanatofauti yake.

Kama ni kweli hii nchi "ilichezewa sana"; tulipoyasikia hayo maneno tulielewa nini?

Ni kweli hii nchi ilichezewa sana, na nani? Kuhusu nini? Nini kilifanyika tuache kuchezewa?

Hiyo ilikuwa ni wakati huo.

Sasa tena tunauliza: Hii nchi itachezewa sana?

Kwa nini tukubali kuchezewa tena, wakati tulishasema, tuliwahi kuchezewa!

Kama hatukubali kuchezewa tena, tumejiandaa vipi ili tusichezewe tena?

Au hatuamini kuwa kama nchi tuliwahi kuchezewa; ilikuwa ni uongo tu wa mtu mmoja hata kama alikuwa ni kiongozi?

Tunayo hakika gani kwamba kiongozi wa sasa anajua anayofanya, na kwamba atahakikisha nchi hii haichezewi tena?

Na tukibaini kwamba tunachezewa tena, tunazo njia za kujinasua na kuchezewa huko?
 
imechezewa, inachezewa na itaendelea kuchezewa unless...

"Avengers: EndGame"
Funguka mkuu, hasa hapo penye fumbo zito "Avengers:EndGame". Tumepigwa bao kirahisi hivyo?

Hatuwezi tukanyanyuka tena, maanake unasema "EndGame"!

Huyo aliyetutangazia "Tumechezewa sana"; huu mchezo wa "EndGame" yeye hakuuona kabisa, ili angalau aweke vigingi vya hapa na pale?

Huu mchezo inaonekana ulikuwa wa humo humo ndani; yaani kikulacho kimo nguoni mwako?

Hebu sema jambo mkuu wangu 'IamJackReacher'. Kidogo nikuchanganye na 'Jack Bower'!
 
Na sasa ndio tutachezewa kisawasawa!
Sina sababu ya kupinga unayosema mkuu, ina maana basi tujiandae tu kuchezewa.

Kukwambia ukweli, hata mimi sioni tumaini lolote juu ya kuzuia kuchezewa. Hakuna mwenye ubavu huo kwa hali iliyopo sasa.

Ninaweza pia kukushangaza wewe, na pengine wengi wa wanaJF hapa nikisema kuwa tofauti zozote zilizokuwepo kati ya CCM na CHADEMA hazitakuwepo tena; kama zitaendelea kuwepo hizo zitakuwa ni tofauti ya ulaji tu basi. Kila mtu atapambana apate mkate wenye siagi.
 
Yule mzee ni genius alituchezea kijanja sana huku akisema tumechezewa sana, sasa hivi tutachezeana maana hadi hapa tulipo hamna asejua kucheza sasa ukicheza na Mimi nacheza hivyo tutaendelea kuchezeana " zingua tuzinguane"
 
sasa ukicheza na Mimi nacheza hivyo tutaendelea kuchezeana " zingua tuzinguane"
Nimeipenda sana hii "zingua tuzinguane".

Ila sina uhakika na uwepo wa ujanja huo. Ngoja tuone, ya nini tuandikie mate mkuu 'ortuuro', huku wino upo?
maana hadi hapa tulipo hamna asejua kucheza
Matumaini yako haya unayatoa wapi, au yanatokana na nini?
 
Nimeipenda sana hii "zingua tuzinguane".

Ila sina uhakika na uwepo wa ujanja huo. Ngoja tuone, ya nini tuandikie mate mkuu 'ortuuro', huku wino upo?

Matumaini yako haya unayatoa wapi, au yanatokana na nini?
Sijaona mwaminifu kiasi kwamba hata Mimi nimeanza kuwa na mashaka na yeyote.
 
Sasa unalalamikia nini mkuu, si jadili tu na kuweka maoni yako?
Mkuu nyuzi nyingi kwa sasa zinaponda kila linalofanywa. Ni vema tukaonesha namna bora zaidi ya kufanya jambo au nini kingepaswa kufanyika ili wenye nafasi wapate kujua.

Kebehi au kuponda haviepukiki ila mapokeo yetu yamekua hasi sana mpaka inatia shaka.
 
Jasiri haachi asili.

Sasa kama huyo jasiri ni mpumbafu basi jua atang'ang'ania hicho hicho.
 
Ukimuogopa kila mtu utaishi na nani hapa duniani? tumia akili kuishi na watu usiowaamini badala ya kuwakimbia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom