Hii nchi haina uhamiaji?

Hii nchi haina uhamiaji?

miley

Member
Joined
Aug 2, 2013
Posts
87
Reaction score
14
Kwanini Dar imefurika wahamiaji toka Malawi? kuna nini wanakimbia kuja Tanzania kuja kuchimba mchanga Mbezi Juu na kulala kwenye chumba kimoja watu 20? Serikali ya mtaa inaona lakini wamefumba macho au wana vibali?

Hii italeta shida wakati wa uchaguzi mkuu. Nawaomba wahusika na hili waliangalie kabla shida haijaingia.
 
Watanzania wakiwa ugenini wanateseka sana, ila sisi tunakumbatia wahamiaji wa kiholela.

Anza wew kureport kwa mamlaka husika
 
Na raia wa Burundi wapo wengi Sana nchini,wanauza machungwa,embe,kahawa wakijifanya wanatoka Kigoma,pua Kuna wachina,pale airport kwenye mgahawa wa framingo wamejaa wadosi ambao hukaa nchini kimagumashi..
 
Mnatoa taarifa rasmi huko Uhamiaji au mnaishia kulalamika na kulaumu tu hapa JF? Huu ugonjwa wa kulalamika na kulaumu bila kuchukua hatua kwa Watanzania, sijui utaisha lini? Hata katika kuchagua viongozi wa ngazi mbalimbali inakuwa hivyo tu. Hatujiandikishi na hata tukifanikiwa kujiandikisha, hatupigi kura. Halafu wakichaguliwa viongozi wabovu tunakuwa wa kwanza kulalamika.

Ukiona tatizo usiishie kalalamika na kulaumu tu. Uwe sehemu ya suluhisho la tatizo hilo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom