Hii Nayo Mpya!

Hii Nayo Mpya!

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
2,085
Reaction score
45
Nimetoka nilikotoka jioni hii, sasa nilipokaribia sehemu ninayokaa nikakutana na jamaa mmoja barabarani lakini anakuwa hajatulia anatembea hapa na pale, huku akiongea na simu kwa jazba na kufoka.

"Wewe mwanamke huishi vituko, usitake kunichanganya, hueleweki kabisa, nimeshindwa kukusoma, kama vipi bwana mie nitapisha wengine!"

Huyu jamaa sijawahi kumwona wala simjui, ghafla "Brother hebu shika hii simu ongea na huyu mwanamke". Nikasema aahhaa, hapa wamenitegea mtego wanataka kunipora! Lakini nikajiuliza anipore mtaani, na kuna watu kibao nawafahamu nawaona na wao wananiona!

Nikamwambia aisee mie sikufahamu wala huyo mwanamke simfahamu, niongee naye nini? Jamaa, akaniambia samahani sana, yaani samahani, naomba tu unisikilize kaka, wala usinielewe vibaya, hapa nilipo nimechanganyikiwa, huyu mwanamke ataniua bure!

Nikamwambia mwanamke mwenyewe yuko wapi? Akasema yupo hapahapa Dar. Nikamwambia hebu nipe maelezo kidogo kuna nini? Akaniambia wewe ongea naye kaka!

Bahati nzuri watu wakawa wamejaa wametuzunguka kiaina, hapo sasa nikasema huyu huenda ana shida kweli na hawa watu wote tena majirani, haiwezi kuwa ni mtego.

Kuna mtu mmoja akasema weka loud speaker, faster jamaa kaiweka, hapo simu ipo on muda wote!

Mazungumzo yakaanza.

Mimi: Dada habari yako, za wapi?

Yeye: Nzuri, kwani hajakwambia nipo wapi (jamaa akadakia, achana naye yupo Dar).

Mimi: Ok, hakuna shida. Sasa mbona jamaa analalamika kuhusu wewe shemeji yangu, kulikoni?

Yeye: Kuna mambo anafanya, nikimwuuliza kwa nini, badala ya kunipa maelezo yeye anaishia tu kuniambia umenichoka! (Jamaa kadakia, mambo gani?)

Mimi: (Nikasema eeenhh, kuna ujanja dada kajifunza Jf ndio anamsumbulia jamaa nini?) Mambo gani dada, wewe sema tu usisite!

Yeye: Huyo kweli ni mchumba wangu, na ameahidi kunioa ingawa hajawa muwazi atanioa lini, lakini tangu tumekuwa wachumba sasa ni miaka 2, yaani jamani mtu kila kitu ninachomwomba, hasa hela ananipa, ina maana hayo ndio maisha yake halisi au?

Mimi: Kivipi dada hebu toa basi maelezo, kwani kuna shida gani mchumba wako kukupa kila unachotaka? (Jamaa yake, "huyu mwanamke mwehu nakuambia aisee", nikamwambia tulia mkuu, acha niongee naye kama ulivyotaka, wewe sikiliza).

Yeye: Ninachojua katika hali ya kawaida mtu haiwezekani siku zote awe vizuri, kila nikimwomba hela hata katika mazingira ambayo nadhani hana au hawezi kunipa, utashangaa ananiuliza sh ngapi, then anatuma au ananipa, saa nyingine hata haulizi ni kwa ajili ya nini? Mtu gani ambaye hakwami hata siku moja, mie hiyo tabia na maisha yake sijapenda (Kwa mbali nikaanza kuona kama kuna logic fulani anataka kuijenga, lakini nikajisemea ngoja niendelee kumhoji. Nikajiuliza anaogopa anadhani jamaa yake labda ni Freemason nini?, Watu wameguna huyu dada vipi, wengine wakaanza kusambaa na kufanya kelele, nikawaambia tulieni jamani).

Mimi: Sasa dada kama ana uwezo wa kukusaidia wewe unataka asikupe?

Yeye: Mie sisemi asinipe, lakini awe na kiasi. Ina maana yeye hana mipango na hela yake, ipoipo tu, nikimwomb, yeye ni kunipa! Miaka 2 yeye hajakwama au hata kuchelewa kunipa hela. Kwanza maisha anayonifundisha au anayotaka kuniaminisha sio! Nimejifunza maisha ya kupata na kukosa, maisha ya kujinyima na kuvumilia, maisha ya raha na shida. Maisha anayonionyesha sidhani kama ni halisia, hata kama ni halisia yananipa wasiwasi! Kwa nini asiwe na mipango na hela (Jamaa kwa hasira, "mipango gani, huyu mwanamke kichaa aisee", nikamwambia naomba tulia mkuu).

Mimi: Kama unachohitaji unapata, sioni kama kuna shida kivile, cha msingi basi umshauri namna ya kuzitumia hizo hela na jinsi ambavyo wewe unataka awe anakuhudumia. Sasa wasiwasi wako uko wapi?

Yeye: Mie naona kama ananipumbaza tu na hela zake, hana mpango wa kunioa wala nini! (Nikasema hapa sasa patamu).

Mimi: Sasa dada angekuwa anakunyima hela au hakupi mara zote ungeamini ndio atakuoa?

Yeye: Sijapendezwa na hiyo tabia yake ya kutumia hela kama kitu cha kunivutia. Kwa sababu kila nikimwuuliza unanioa lini, anaishia kuniambia kwa kejeli, unakimbilia ndoa ili iweje mbona kila kitu nakupa! (Nikasema ok, huyu sasa kakutana na lara 1 hataki entertainment za hela, mmmhhh, kama vile ana akili). Tumezuliana ugomvi kwa sababu yeye hataki kuelewa ninachomwambia, anadhani hela yake itamwezesha kufanya kila kitu.

Mimi: Dada mie nimekuelewa, hata jamaa yako anasikia, naomba tu nendeni taratibu elewaneni, kama ni habari ya ndoa mkubaliane, naamini itawezekana.

Yeye:

Baada ya kumaliza, dada akakata simu, jamaa akaanza, "ndio nini sasa ameongea!" akataka ampigie tena, nikamwambia mkuu acha, ngoja tuongee kidogo mimi na wewe.

Nikamwambia mkuu, tatizo mbona dogo, shida hapa nimeona shemeji anataka umhakikishie swala la ndoa!

Jamaa akajibu, nimemwambia nitamwoa shida yake nini? Mie nikamwambia, yeye anaona kama unampumbaza kwa kumpa hela na vitu vingine ili asahau kuhusu lini mtafunga ndoa.

Nikamwambia sasa fanya hivi: Mwambie shemeji kwamba unamwoa lini, yaani kama ni mwakani mwezi wa kwanza au mwaka ujao mwezi fulani, ikiwezekana na tarehe, basi hizi shida zote hazitakuwepo, ni jambo dogo tu mkuu!

Jamaa akauliza, wewe unadhani shida yake ni ndoa?

Mie nikamjibu, ndio, sidhani kama kuna jingine! Au wewe hauko tayari kumwoa? Akasema huyu kwanza ni sawa na mke wangu, mie nisimwoe kwa nini? (Mie nikajiuliza sasa tatizo nini?).

Nikamwambia mmeshawahi kukutana? Akajibu, juzi alikuwepo ameondoka, anakuja kila leo!

Nikamwambia, aisee wewe mwambie wazi utamwoa lini, haya matatizo yote yataisha. Kwa heri mkuu acha nifike nyumbani. Nikawa nimemwacha jamaa. Kidogo akawa ananikimbilia, akaniambia mkuu samahani kuna kitu, nimesahau kukuuliza! Nikamwuuliza, nini?

Akaniambia unajua kuna message sometimes huyu mwanamke ananitumia sizielewi, ndio mambo yake ya kutaka ugomvi, soma hii sasa, anamaanisha nini! (Kuifungua, mbona message ni ya kiingereza na kama vile inaeleweka!).

Kuisoma, imeandikwa "You are my number one, you are the star!". (Nikawa na wasiwasi kwamba jamaa huenda hajui hata neno moja la kiinglish). Nikapiga moyo konde nikamwuuliza, wewe umeielewaje?

Jamaa, "Asiniletee usenge, kuna message zake huwa za ajabu ajabu, mojawapo ni hii, ananiambia mimi ni namba moja ina maana huyu mwanamke ana wanaume wengine kabisa".

Karibu nicheke nivunjike mbavu, ila nikasema hiki kicheko nitakibana, bahati mbaya tumebaki wawili, kama kungekuwa na kundi la watu kama ilivyokuwa mwanzoni ningecheka mpaka basi!

Nikamwambia taratibu, mkuu, hiyo mbona haimaanishi hivyo, anakusifia tu mkuu kwamba wewe ndio wewe hakuna mwingine!

Yaani kuna mazungumzo fulani tuliendelea kuyafanya hapo katika harakati za kuelimishana, dah, nikasema mie sicheki ng'o ingawa kicheko kilikuwa kimefika pomoni. Nimelazimisha kumwacha, nilivyofungua tu mlango nikaingia ndani fasta na kuanza kucheka!

Nimejiuliza maswali huyu jamaa swala mbona kama linaeleweka na dogo? Kama yeye yuko tayari kumwoa kwa nini asitamke? Nilivyoona ni kama vile yuko tayari kumwoa ila uelewa wake wa mambo nina wasiwasi nao ndio maana anagombana na mchumba wake!

Dah, kumbe mtu anaweza kuwa yupo vizuri mambo mengine lakini kama hamwezi kuelewana kwa sababu ya akili yake ni majanga!
 
Last edited by a moderator:
mnasoma shule gani.? Msizofundishwa ku samare..
 
Ahsante sana haya tuambie hadithi yako inatufundisha nini?
 
hihihiii hii kali mwanzoni nilitaka nikupashe kwamba mbona kila siku simplicity una umbea wa watu, nikasema wacha tu noisome hii ..... kufika katikati nimecheka sana, jamaa hana confidence ni hilo tu.
 
unauwezo wa ku summarize content yako kwa ufupi....
data wewe sasa hivi najua huwezi kusoma kwa sababu picha ya Wasira ITV bado ipo kichwani!
 
Last edited by a moderator:
maskini huyo kaka anampenda dada ila haoni kama ndoa ni muhimu kama hakuna kipingamizi angemuoa tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom