Hii mitandao ya simu imeshatugeuza shamba la bibi!

Haujalalamika Sukari wala Ngano kupanda bei..., Unalalamikia Kampuni binafsi ?

Uzuri haujalazimishwa na una choice kutafuta alternative..., by the way kabla hatujalaumu mitandao tuangalie Serikali / TCRA wanapiga kodi kiasi gani ? Usijekuta kikulacho ki nguoni mwako...
 
Waafrika badala ya kutafuta suluhisho tunalalamika lalamika Kama mbuzi aliyempoteza mamaye
Hizo ni changamoto kwa wateja lakini ni fursa kwako angalia mbele tafuta suluhisho
Mwaka 2008 nilipanga foleni kuanzia asubui saa 2 asubui hadi saa 10 jioni kulipa ada pale nmb clock tower arusha lakini Sasa hivi haya Mambo hakuna tena kwanini? Kwa sababu watu wameona fursa na kuleta mabadiliko acha kulalamika tumia fursa hiyo
Unafanya kaz mtandao wa simu nn??
 
Ukishakuwa na fikra za kulia lia hauwezi kuona fursa. Kama unaona kupiga simu ni gharama mfuate huyo ndugu yako mkaongee ana kwa ana.
Watu watumie gharama kununua mitambo ya kuunganisha mawasiliano alafu wewe mpuuzi mmoja uje kulia lia gharama ni kubwa? Umeshajiuliza watu wametumia rasilimali kiasi gani kufanikisha Jambo hilo?
Nenda lab fanya tafiti vumbua mbinu yako ya kuwasiliana alafu punguza bei au fanya bure kabisa
Uholanzi inaishi juu ya maji, kuna nchi kila siku barafu imetanda juu ya nchi hao watu Kama wasingekuwa wabunifu na kutafuta suluhu ya matatizo yao wangekua hai kweli? Achane kulia lia tafuteni suluhu Kama hamna ongeza kipato chako kukidhi mahitaji yako.
Ujumbe huu uwafikie wanasiasa na mashabiki wote wa UKAWA!
 
HIvi sisi wateja wa huduma za simu ni nani mtetezi wetu? Kila siku haya makampuni yanatupandishia bei za huduma zao wanavyojisikia na hakuna wa kuwadhibiti!

Mwezi Januari nakumbuka TCRA walitoa ahadi kwa wananchi kuwa wamesikia kilio chetu kuhusu ughali wa gharama za mitandao ya simu na kuitaja tarehe 28 Februari kuwa siku ya kutangaza muarobaini wa tatizo hilo. Mpaka leo tarehe 2 Machi kimyaaaaaaa. Kama hawapo. Mambo kama haya huondoa imani kwa vyombo vyetu.

Sasa kama mtetezi wetu ndio hivyo hatusikii sauti yake, tunafanyaje? Dawa ni kuanza kususia makampuni haya ya kinyonyaji na kuhamia yenye nafuu.

TIGO ndio wamezidi kabisa. Bando la internet walilozoea kuniuzia kwa Tsh. 10,000 GB 7 kwa mwezi, leo wananiuzia GB 2.5 kwa bei hiyo hiyo ya Tshs 10,000 kweli? Inauma na haivumiliki.

Huu ni uhuni na wizi wa wazi kabisa. Huduma yao haijawa bora hivyo kiasi cha kupanda thamani kiasi hicho na kushusha thamani ya pesa yangu mteja.

Wizi wa hali ya juu sana
Tena level ya lami
 
Waafrika badala ya kutafuta suluhisho tunalalamika lalamika Kama mbuzi aliyempoteza mamaye
Hizo ni changamoto kwa wateja lakini ni fursa kwako angalia mbele tafuta suluhisho
Mwaka 2008 nilipanga foleni kuanzia asubui saa 2 asubui hadi saa 10 jioni kulipa ada pale nmb clock tower arusha lakini Sasa hivi haya Mambo hakuna tena kwanini? Kwa sababu watu wameona fursa na kuleta mabadiliko acha kulalamika tumia fursa hiyo
Acha lugha za kihuni na dharau unapojibu hoja ya mtu humu. Wewe unasema ulipanga foleni kwa muda mrefu lakini sasa hayo mambo hayapo. Wewe kama mteja ni nini ulichokifanya hadi huo usumbufu ukaondoka? Si ni hayo makampuni yanayotoa huduma na yenye mitaji yao ndio yametumia fursa kubadili hali?. Huna hoja!!
 
Hawawezi kupandisha bei za vifurushi bila sababu.. itakua wameongezewa kodi au gharama za uendeshaji zimepanda au vyote kwa pamoja.. nahisi serikali imejificha nyuma ya hili. Wakiicha mitandao ikitupiwa lawama na wananchi
Hata mimi naliona hili ndio maana hatusikii kauli ya TCRA kama tulivyoahidiwa ingetoka tarehe 28 Februari.
 
Ukishakuwa na fikra za kulia lia hauwezi kuona fursa. Kama unaona kupiga simu ni gharama mfuate huyo ndugu yako mkaongee ana kwa ana.
Watu watumie gharama kununua mitambo ya kuunganisha mawasiliano alafu wewe mpuuzi mmoja uje kulia lia gharama ni kubwa? Umeshajiuliza watu wametumia rasilimali kiasi gani kufanikisha Jambo hilo?
Nenda lab fanya tafiti vumbua mbinu yako ya kuwasiliana alafu punguza bei au fanya bure kabisa
Uholanzi inaishi juu ya maji, kuna nchi kila siku barafu imetanda juu ya nchi hao watu Kama wasingekuwa wabunifu na kutafuta suluhu ya matatizo yao wangekua hai kweli? Achane kulia lia tafuteni suluhu Kama hamna ongeza kipato chako kukidhi mahitaji yako.
Najizuia tu kukuita fala lakni ulistahili hilo maana unavyoalazimisha kwa nguvu hoja zisizoeleweka utadhani na wewe unamiliki moja ya makampuni ya simu. Pole sana.!
 
Acha lugha za kihuni na dharau unapojibu hoja ya mtu humu. Wewe unasema ulipanga foleni kwa muda mrefu lakini sasa hayo mambo hayapo. Wewe kama mteja ni nini ulichokifanya hadi huo usumbufu ukaondoka? Si ni hayo makampuni yanayotoa huduma na yenye mitaji yao ndio yametumia fursa kubadili hali?. Huna hoja!!
Akirudisha makamasi yake hapa atajiona mjinga sana. Humu siku hizi kuna watu wanajiona wana akili na uwezo sana ila ukiwapa aya mbili wajileleze wanapoteana.
 
Back
Top Bottom