Mu7
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 1,549
- 1,804
HIvi sisi wateja wa huduma za simu ni nani mtetezi wetu? Kila siku haya makampuni yanatupandishia bei za huduma zao wanavyojisikia na hakuna wa kuwadhibiti!
Mwezi Januari nakumbuka TCRA walitoa ahadi kwa wananchi kuwa wamesikia kilio chetu kuhusu ughali wa gharama za mitandao ya simu na kuitaja tarehe 28 Februari kuwa siku ya kutangaza muarobaini wa tatizo hilo. Mpaka leo tarehe 2 Machi kimyaaaaaaa. Kama hawapo. Mambo kama haya huondoa imani kwa vyombo vyetu.
Sasa kama mtetezi wetu ndio hivyo hatusikii sauti yake, tunafanyaje? Dawa ni kuanza kususia makampuni haya ya kinyonyaji na kuhamia yenye nafuu.
TIGO ndio wamezidi kabisa. Bando la internet walilozoea kuniuzia kwa Tsh. 10,000 GB 7 kwa mwezi, leo wananiuzia GB 2.5 kwa bei hiyo hiyo ya Tshs 10,000 kweli? Inauma na haivumiliki.
Huu ni uhuni na wizi wa wazi kabisa. Huduma yao haijawa bora hivyo kiasi cha kupanda thamani kiasi hicho na kushusha thamani ya pesa yangu mteja.