MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Believe me or not, huu utaratibu mpya wa kuanzisha miradi mikubwa na ya mapesa mengi bila kupitia taratibu zilizozoeleka kwa sababu mtu katiba inatoa mwanya huo, kimsingi mambo kama haya hua na mapungufu makubwa sana. Ukianza kufuatilia utakuta matumizi ya pesa zinazotengwa hayaendani na miradi.
Walioanzisha mabunge walikua na maana zao, hii ndio kila mara bajeti nyingi zinapojadiliwa huzuka mabishano makubwa sana baina ya wabunge kukiwa na maana ya kuwepo kwa mapungufu makubwa ndani ya bajeti hizo.Sasa kama mradi unatekelezwa kwa bajeti zilizotengwa kwa maagizo hali itakuaje?
Sasa bunge linapokwepwa na miradi mikubwa inatekelezwa pasipo kulihusisha tufahamu kua lazima kuwepo na mapungufu makubwa tuu, tukumbuke usemi usemao kua "Mali bila daftari hutumika bila habari". Tu nafikiri kufanya hili ni kulisaidia taifa kumbe ni kujitengenezea mazingira ya kulitia hasara. Huwezi kufanya mradi unaochukua muda mrefu kukamilika au usiohitajika kwa haraka kama kitu cha Emergency, hiki kitu si cha kawaida. Hivi ununuzi wa bombardier ni Emergency? Kwenye majanga hata sheria inaruhusu pesa kutolewa kwa emergency ingawa nako kuna taratibu zake.
Nasema ipo siku hawa wanayoyafanya haya watakutwa na hatia za matumizi mabaya ya ofisi au ufisadi. Tunayafurahia haya kwa vile uwezo wetu wa kuhoji huenda unatia mashaka lakini utafika muda haya mambo yatamlaza mtu jela bila kujali umri alionao kwa sababu sheria na vifungu vyake viko wazi. Kutekeleza mambo nje na taratibu za kisheria kwa sababu tu sasa ni zama zingine, ipo siku zama zingine zitafuta sheria katika kufuatilia kama zamazingine nazo zilifuata sheria.