Hii mikasa inanipata mimi pekee?

Kuna msemo unasema usilalamuke kwakuwa umeinguzwa shimo! Mradi uhai, unamikono, macho, akili, vyeti. Pambana mwanangu, piga moyo konde tafuta vyako, huo unyonge unauonyesha ndiyo ushindi wa huyo ndugu yako. Tafuta kazi pengine huku unafanya jitihada za kudai haki yako.
 

Hapo kwenye fungu la kumi ndio siri ya mafanikio yangu ilipo. Huwezi amini nikitoa 10% huwa naona maajabu ya Mungu. Napata baraka na pesa nyingi inaingia.
Ni sawa na Kulipa Kodi ya serikali. Usipolipa unaweza fungiwa biashara
 
Mtu anapata ajira pumbavu moja linatokea (kama lenyewe lilisoma vile) eti subiri uende chuo ili uende jeshini ukiwa na degree kabisa (my foot!). Kana kwamba hiyo ajira kaihifadhi kabatini vile na wewe ukamuamini.
 
Kaka katika kitu nilichojifunza usije mkategemea ndugu akutoe kimaisha. Utaumia sana man, mi mwenyewe nimesha experience ishu kama hiyo, ndugu yuko position nzuri serikalini lakin hakusaidii kwa lolote.
itisha kikao cha wana ukooo...
Au fungua kesi ya madai...

Usiache haki yako ipotee hivi hivi
 
Pole kwa changamoto hizo,lakini hayo ndio maisha na hapo ndipo pa kujifunza, wewe bado kijana, tena wa kiume, komaa tu, yote hayo yanapita na yatakuwa historia. Ushauri wangu;

1) Mkabili tena huyo ndugu yako, kwa heshima na unyenyekevu (kwa mara ya mwisho) mwambie kwamba una hali ngumu na una uhitaji sana wa fedha zakom, hivyo ni muhimu sana kwa sasa akupatie haki yako, akikupatia ni vema, lakini akigoma, basi achana naye, usisimamie tena biashara yake na umwambie ukweli kwamba hutaweza kuendelea kusimamia biashara yake wakati maisha yako yanakuwa magumu kila siku, na kwamba yote unamwachie Mungu. Usimtukane wala usimuambie maneno yoyote makali au mabaya. Usihangaike na kumshitaki popote, wala usifungue kesi ya madai, haitakusaidia na utapoteza muda na hutalipwa chako, wewe mshitakie Mungu, kisha endelea na maisha yako. Kwa maneno mengine ni kwamba, amekupa au hajakupa fedha zako, umeshajifunza vya hivyo, achana naye sasa!

2) Kuhusu kuoa - usikimbilie kuoa au kutaka na kuishi na mwanamke wakati maisha yako hayako sawa, kuwa mkweli kwa nafsi yako, kwamba unahitaji kujipanga upya. Kuna raha gani kuishi na mtu kwenye mazingira ya matatizo? Tena sio mkeo? Muambie ukweli huyo mwanamke wako kwamba, kwa sasa maisha/mambo yako hayako sawa na hutaki yeye aendelee kupata shida akiwa na wewe, wakati anaweza kuishi maisha bora huko nje. Mpe uhuru wa yeye kuondoka, kuendelea na maisha yake ili wewe ujipange na maisha yako. Akiamua kubaki ili mle vumbi wote pamoja, poa, maana hayo ndio mapenzi, lakini huo utakuwa uamuzi wake na utakuweka wewe huru ukiwa na amani. Ila ukila bingo na mambo yako yakinyooka huko mbeleni (Nina hakika yatakunyookea) utambue kwamba uda deni kwa huyo mwanamke - usije kujifanya mjanja, kumsaliti na mambo kama hayo.

3) Tatizo ni wewe, inabidi ubadilike hasa unavyotazama mambo na kuwalaumu wengine kwa makosa yako mwenyewe, kwa maamuzi mabovu uliyoyafanya mwenywe siku za nyuma. Kwanini uliacha kazi yako mwenyewe ya kufundisha na kuja kusimamia shughuli ya ndugu yako? Maana yake ni kwamba uliacha kujitegemea mwenyewe na ukarudi kumtegemea mtu mwingine (Kosa kubwa!), yaani maisha/hatima yako yote ulimuachia mtu mwingine na yeye hana sababu ya kuangalia maisha yako, anayepaswa kuangalia maisha yako ni wewe na sio yeye. Kwa mfano, ungebaki na kazi yako ya kufundisha na ukaendelea na biashara yako, leo ungekuwa wapi? Bila shaka mbali sana! Kwa mtazamo wangu ni kwamba huyo ndugu yako sio tatizo kwako, hiyo biashara yako kudorora nayo sio tatizo, hata kuishi maisha magumu nako sio tatizo kivile. Ni mungu au ulimwengu unakufundisha, kwamba badilisha maisha yako, anza upya, bado kijana, tena umesoma, anza kulitazama tatizo lako kama lako na pambana nalo na kama wewe, acha kulaumu wengine. Angalia ulipojikwalia na sio ulipoangukia. Tatizo liko akilini mwako, kwamba 'matatizo yangu haya, yanasababishwa na fulani', Huyo ndugu yako mtoe kabisa akilini mwako. Chukulia kila kilichotokea ni shule kwako. Ni Mungu na Ulimwengu unakupa fursa nyingine huku ukiwa umepata funzo kubwa la maisha.

Kila la heri
 
hahahahaaa kweli aisee ,unajua binadamu tunapimwa padogo sana inawezekana kutokukupa mshahara ni kipimo chake cha imani kwako
 
Kuna wanawake wengine ni nux hawaolewi nyota zenu hazienfani tafakari
 
Msamehe na uendelee na mipango mingine ya kutafuta pesa
Million 3 ni kidogo sana ukilinganisha na muda/pesa utakayoitumia ili upate haki yako kwenye vyombo vya sheria, pia kuuharibu kabisa uhusiano wenu coz hamna kitakachobadili kuwa huyo ni kaka yako, atakuwa kaka yako milele
MUACHIE MUNGU HE WILL DEAL WITH HIM
 
Haki hai ombwi bali ina daiwa,minakushauri kama vipi kinukishe kwa ndugu na marafiki zake,muwekeeee mabango kila mahali kuwa una mdai na hataki kukulipa,mtanganze kwa watu wanao mfahamu na wasiomfahamu,hakikisha mpaka wafanyakazi wenzake wajue una mdai ila hataki kukulipa ana nia ya kukudhulumu,mtangazeeeeee kila mahali aisee! Mpaka ajutie tabia yake ya udhulumati,halafu jitahidi uache kufanya kazi kwake kafanye shughuli zingine huku ukiendelea kumtangaza kila mahali mpaka akulipe dadeki.
 
Masahibu madogo tu hayo. Pambana kiume yatapita. Mi nilijua bonge la ishu.
 
wazi mkuu!!
 
ahsante ndugu
 
Huwa naona huruma sana kwa kijana anaejituma na kutafuta maisha halafu mtu anamuharibia pole sana. Usikate tamaa
 
Ushauri mzuri Sana. Mkuu tafuta MTU mkumbwa kama uncle aongee naye.

Mkuu I wish you well, keep going we are all coming in from the cold, from difficulties. That is our lives. Blessings and best wishes.
 
Ushauri mzuri Sana. Mkuu yachts MTU mkumbwa kama uncle


Mkuu I wish you well, keep going we are all coming in from the cold, from difficulties. That is our lives. Blessings and best wishes.
thankiu comrade!! I swear to fight till the grave takes me off!! tuombe uzima.
 
Me nianze kukulaumu kwamba uliona mwezi wa kwanza unapita hulipwi wa pili wa tatu na ww umeng'ang'ana na kukaa kimya wakati makubaliano ni mlipane!!!

Kuna watu wana makubwa zaidi ya hilo na wanapojikwaa huendelea mbele wanasahau ya nyuma sasa najua kuna ulichojishauri tayari pamoja na hilo angalia fursa ulizoambiwa na wachangiaji hapo juu usonge mbele tena bahati yako unacho hata cha kuanzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…