Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nje ya Bunge hakuna Upinzani na nje ya Dodoma, hakuna vyama vya upinzani. Hii ni kauli ambayo ninaweza kuisema kwa ujasiri mkubwa na ninasema hivyo kwa kumaanisha.
Ni nani aliona harakati za vyama vya upinzani kabla ya Bunge la Bajeti? Ni kiongozi gani wa Upinzani alidiriki kupaza sauti nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Ni kikao gani cha chama cha upinzani kiliwahi kufanyika nje ya kipindi cha Bunge la Bajeti?
Baada ya Bunge la Bajeti kuanza, ni dhahiri kwamba Wapinzani wamepata ajenda za kuongea kwenye public. Sote tumeshuhudia jinsi suala la uhaba wa sukari lilivyowatoa mapovu wabunge wa upinzani wakidhani kuwa CCM italegeza kamba yake na kuruhusu mfumo wa zamani uendeleee. Wapiiii. Magufuli ameendelea kukaza buti na soon ajenda hiyo imeshasahaulika.
Kupitia vyombo vyao vya habari ikiwemo Mwananchi Digital, viongozi wa upinzani wanauza sura kwa sasa. Kila wanachosema wanataka kisemwe na kiandikwe kwenye media zao. Lengo ni kuulaghai umma kuwa wanachokisema ndicho wanamaanisha kumbe wapiiii! Ni ulaghai tu wa kisiasa unafanyika. CHADEMA kwa upande wao wamediriki mpaka kuhamisha vikao vya Kamati Kuu kutoka Dar es Salaam hado Dodoma kwa lengo tu la kuteka hisiasa za Watanzania. Kuna wakati pia Lowasa alisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa lengo la kuweka mikakati yake ijapokuwa hakufanikiwa.
Hizi ni hulka za wapinzani wa Tanzania. Mihemko yao inaishia Bungeni tu kwani nje ya Bunge wanajua kuwa hakuna anayewaunga mkono