Hii kwetu Wanaume wote

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Unasikia mwanaume anasema Mbona mama Fulani au mke wa fulani, ikifika jioni anapendeza? Hayo ni Maneno ya wanaume Wengi kwa wake zao.

Vichekesho Kweli* : unatarajia kuvuna wakati hujapanda? Mnatarajia vielee nakati hujaviunda? Hivi ni Lini umemnunulia Mkeo ivyo ambavyo akivaa (Mkiwa ndani) atapendeza?

Wewe ukisha nunua roba la mchele, mafuta, unga, na mkaa unahisi ndio Ushamaliza, Halafu eti unamlaumu mke hapendezi. Kubwa zaidi unarudi kwako bila ya taarifa, sasa ajipambe saa ngapi?

Hembu mume jijengee mazowea Kabla hujatoka kazini mpigie Simu mwenza wako Mwambie mke wangu kipenzi, my sweety, my love, mama watoto wangu saivi ndio natoka kazini baada ya mda Fulani ivi nitakuwa nishafika nyumbani. Uone ukirudi kama hujamkuta mke kesha oga, kajipamba, ananukia na anapendeza kwa ajili yako. Ugonjwa wakujitakia hau ambiwi pole.

Wanaume tubadilike, andaa mazingira ya mke kupendeza alafu kama ajajipamba na vitu vipo ndio uanze mlaumu.
 
Kwahiyo unataka kumwambia mwanamke kuwa unarudi home ili apate muda wa kuaga madanga yake sio.. mwanaume unatakiwa timetable yako iwehaieleweki
 
Back
Top Bottom