Hii kwenu imekaaje

Hii kwenu imekaaje

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,027
Reaction score
20,414
HII TABIA SASA INAKELA WACHA TUSEME TU

Kuna kasumba au Tabia ya walimu wa shule za msingi hasa hizi za Serikali kumejengeka kasumba ya walimu kuwagiza watoto KUNI, MAJI, MAUA n.k kuhusu maji Mimi kwangu sio tatizo Sana maana upatikanaji wake sio mgumu Sana, lakini kuhusu Kuni na vitu vingine ambavyo adimu kuvipata hasa shule za hapa mjini mfano Kalangalala, Nyanza Mseto Geita Kivukoni Mbugani n.k nyie walimu wa hizi shule mtoto unamwagiza kuni Tena unamtishia na adhabu juu hebu tusaidieni nyie wapi kwa hapa Geita kuni zinapopatikana⁉️ mnataka kuwafundisha watoto wetu waanze kuiba?

Leo nimemkuta mtoto wa shule moja wapo hapa mjini kwenye shamba la mtu anaiba miti inayotumika kusapoti mazao shambani🤷 nikamuuliza kwanini anafanya hivyo akasema waliagizwa kuni na Mwalimu na ni lazima kila mtu aende na kuni asipopeleka ataadhibiwa 🙆😳 kitu Cha ajabu kabisa zingekuwa shule za kijijini tungesema wazazi wanamashamba watoto wataenda kuchukua kuni Sasa hizi shule za mjini mnataka watoto waende polini wakakamatwe na watu wa misitu?

Tafuteni nishati mbadala kuliko kusumbua watoto wetu na Mambo ya kuni🤷 walimu pamoja na viongozi mnaohusika na idara hiyo liangalieni hilo swala kwa jicho la tatu maoni yangu.
 
Back
Top Bottom