Hii kwangu ni ndoa ya mwaka

Hii kwangu ni ndoa ya mwaka

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,502
Reaction score
6,444
Habari JF?

Katika pitapita za huku na kule kupambana na maisha yetu haya, nilijikuta nimekutana na familia moja ambayo daah!! Walinivutia sana lakini walinifanya nijifunze kitu ambacho nanyi kupitia JF mnaweza kujifunza au kutoa shuhuda kama zipo ndoa zingine za namna hii achilia zile za vijijini.

Jamaa ana wake wawili, mkubwa na mdogo ila hao wake zake wanavyoishi ni zaidi ya mtu na ndugu yake!! Wanapendana to the maximum. Wanaishi nyumba moja waliyoijenga pamoja kwa nguvu ya wote watatu yaani wake wawili na mume, master bed rooms mbili yaan ya mke mkubwa na mdogo na vyumba vingine vya watoto huku wakishea sebule yao nzuri!!

Kilichonishangaza zaidi ni vijana (mume ana 36 na mke mmoja 30 mwingine 28) wasomi wa bachelors wenye watoto watatu mke mkubwa wawili na mdogo mmoja huku jamaa akijitapa kuwa wanakula ujana watoto wametosha!!

Nilimuuliza jamaa mara kadhaa umewapa nini hawa mabinti mpaka kupendana hivi kiasi cha kukaa pamoja sebuleni wakichezea smart phones zao pamoja wakiwa na furaha tele? Jibu lake lilikuwa ni kuwaelewesha na kuwajali wote kwa namna moja!!

Niliwauliza wake wenyewe kama wako poa? (huku wamekaa kwenye love siti yao mume katikati) wakanijibu ni zaidi ya poa na wanafurahia maisha ya pamoja kiasi kwamba mchana kila mmoja anapokuwa kazini wanamisiana sanaaaa!!

Hamgombani? "Tugombanie nini sasa na mume ni wetu sote na zamu ya kulala inajulikana kwa kila mmoja, zaidi tuna amani ya moyo sana kwa maisha haya tunapika pamoja, kustorisha pamoja yaani ni bonge la kampani watu hawajui tu. Si unajua visirani vya wanaume? hata siku jamaa akija na visirani vyake sisi tunafarijiana kwa story kama hivi au mmoja wetu akisafiri basi anajua mume wake yupo kwenye mikono salama ya mke mwingine. Kikubwa ni kuepuka maneno ya watu tuu"

Mabinti wa siku hizi, wasomi wetu na mapenzi ya siku hizi yalivyo!! Ni mwanamke gani atakubali kuolewa mitala?? Tena wanaishi mjini kabisaaa na kila mmoja ana kazi yake

Yote tisa kumi kuishi nyumba moja mnashea miundombinu pamoja kwa wanawake wa kibongo ni ishu!

Salute kwa hii ndoa, wanawake kwa waume wa JF tujifunze kumbe MITALA si ugomvi. Sikujua hilo japo sina maana ya kuleta mabadiliko.....!!!
 
Pamoja na hayo yooote,wape muda kidogo tu utasikia mambo ya ajabu na hata kwa waganga wataendeana,tena jamaa akiyumba tu kiuchumi ndio balaa kabisa.

Hii wanaiweza sana Waarabu(sio wote) kutokana na Uwezo wa kiuchumi walio nao na pia kutokana na sheria kali ndani ya dini na nchi zao.

Time will tell,
 
Hii mbona inawezekana, sema tu labda wote mume na wake zake wawe wachaMungu hapo ndo wataishi ivi.
Maana siku hizi unakuta watu hususan wake wenza wanagombana sababu kubwa ni kutokunshiba Mungu, na baadhi ya wanaume nao pia wanakosa kutenda haki kwa wake zake kwa usawa, mfano akimpa bi mkubwa kanga basi na bi mdogo vile vile ampatie, na huyu akila nyama na mwenzake vile vile hapo ndo mtakapo anza kuona raha ya uke wenza.
 
Mkuu wanandoa wote ni wabongo kabisa? just curious
 
sawa wanakula ujana, ujana ukiisha je,wasije wakagawana hadi sakafu!
 
Bora achelewe kurudi..lakini arudi.maswala ya siku mbili kwangu mbili kwa mwingine hapana..tena ndio ukute wake wa4 unakaa siku kumi humuoni mwenzio.

Mungu niepushie.
 
haiwezekani hii kwa kweli,hao wanawake ni unique kwa kweli
 
Back
Top Bottom