Hii kwangu imekuwa changamoto kubwa. Hata natamani kukimbia home

Mimi nimekaa na wadudu Hadi wamekuwa.part of me..Mende, gecko and the like..Mama hataki madawa yakuulia wadudu anasema sumu..

Nge nimeua sana, tandu and the like.. nyoka Mama alikua anaua tukishirikiana
Japo siku nyingi sijakutana na nyoka.. Alhamdulilah.

Wadudu hawanipi shida Sanaa labda kunguni
 
labda aliwakimbiza huko Changanyikeni
 
 

Mungu Ashukuriwe, mie mwenyewe nishaua nge na tandu sana... Kuna siku zamani huko nipo kama 14 yrs niliua 3 snakes in a day kwa time tofauti tofauti.... alipokuja kuonekana wa nne niliwambia mie huyo simgusi mana hawa watakuwa sio snakes wa kawaida coz walikuwa size moja rangi moja time tu walikuja tofauti
. Yaani kwetu ilikuwa akionekana mdudu naitwa mie ndio nlikua starring wao. Ajab saivi ndio nimekuwa mwoga mwoga yaani hata sipendi kuona wadudu wadudu
 
Nyoka wa kijani hangati kutokana na maumbile ya meno yake, hana meno kwa mbele, meno yake yameanzia katikati ya taya, hivyo kungata mpaka umkanyage na ahangaike kutoka
Wakuu hapa naona umeseleleka na mazoea.

Ni kweli Kuna nyoka wa kijani wasio na madhara (Green Grass Snakes, Green Rough Scale snakes na Green Snakes) Hawa unaweza hata kucheza nao lakini don't take a chance Kama huwezi kuwatambua nyoka kwa muonekano wao na sio rangi yao peke yake.

Kuna nyoka wa kijani wenye madhara Kama Boomslang na Green Mamba Hawa usijaribu kunyoosha mkono uwashike na uzuri au ubaya wao mbinu yao ni moja "Wait and see" kifupi patience ni silaha yao.

Green Mamba akikung'ata huna hata saa ya kuishi Kama utakosa msaada, sumu yake huathiri mfumo wa fahamu na moyo. Na kwa faida ya watu wa pwani Green Mamba wanapatikana Sana pwani ,Tanga, Dar es Salaam, Morogoro mtwara na Lindi.

Boomslang ni mpole na watu huzani hana madhara lakini katika nyoka wa kijani mwenye sumu Kali na yeye yumo akikuuma unaweza pitisha masaa bila kuona madhara na hapa wengi wamekufa pasipo kujua kwasababu ya kupuuzia. Sumu yake huathiri mfumo mzima wa damu.

Ukimsogelea Green Mamba Kama yupo Chini husimama hii ni ishara ya mapambano na Kama akiamua kukufukuza hufiki mbali.

Ukimsogelea Boomslang hutengeneza umbo "S" tayari kuattack yeye Hana tabia ya kufukuza. All in all kama huwezi kuwatambua chukua tahadhari, binafsi naweza kuwatambua but I never take a chance to belittle them.

Chizi Maarifa
Nyoka ni ngumu kupambana nao lakini unaweza ukachukua hatua chache wasifanye makazi yako kuwa makazi yao.

👉Mosi hakikisha ujenzi wa nyumba yako umezuia penyo kwa nyoka kuingia ndani ya nyumba hapa namaanisha milango na madirisha yawe well fitted
👉Hakikisha chemba za maji machafu zimefunikwa na mifuniko sawasawa bila kuacha nafasi
👉Fukuza au ondoa upatikanaji wa chakula Cha nyoka Kama vyura, mijusi,konokono,vinyonga,panya etc
👉Ondoa maficho ya nyoka Kama mashimo, nyufa, na pia nyoka hupenda kukaa kwenye sehemu zenye giza vivuli vizito na zenye unyevu
👉Fuga mifugo inayokula nyoka Kama Turkey (Bata mzinga) Nguruwe (Samahani Kama nimekukwaza kiimani) na Guinea Hens (Hawa nadhani ni Kanga)
👉Kuna harufu nyoka huwa hawapendi na moja ya harufu wasiyoipenda ni Moshi was Moto Kama mapira so you can smoke them out hili hufanyi kwa siku moja yawezakua wiki nzima Moshi haukati
👉Panda mimea inayofukuza nyoka Kama Michaichai kuanzia getini
👉 Landscaping, fyeka majani na epuka vichaka nyumbani
👉Chunguza fence yako kwa ndani na kwa nje Kama Kuna mashimo na nyufa ziba.

Mengine ni expensive Kama kuspray mafuta ya karafuu na mdalasini kwa wakati moja.

Salaam.
 
Nyoka huogopi wewe? Mimi naogopa hata picha yake.
 
Tooba..hilo eneo siwezi kukaa asilani
 
Mm sipendi mnyama paka....
Tena
Ile anakufuata na mkia wake anakugusa gusa sipendi mnyama anaitwa paka Wala huwa sipendi anisogelee...
Kuna siku nilikua nimekaa grossary na Rafiki zangu wawili wadada....
Tukawa tunakula nyama ya mbuzi ilikua jioni
Mapaka ya kibabe yakawa Yana zengea zengea nyau nyau mm nimepiga buyu....ile Sina hili Wala like paka mmoja akaja kunikwapua nyama mkononi
Nilishituka mpka wale wadada WALISHANGAA....
Binafsi nachukiaga paka Ila sio kwamba nawaogopa...
Sitamani hata kuguswa au kumshika huyo kiumbe...
 
Nashangaa had kahama twn wazee kuna kamtaa kanaitwa phantom kuna nyoka kilaa sku huku nyuma tunauwaa nmenusurika kukanyaga mara 2 nyoka kahama mjin
 
Mzee baba unamoyo aisee, ningekuwa nishahama kitambo hapo. Dah, bafe nimwone na niendelee kukaa hapo, bafe yule hatari, ligi moja na cobra.
 
Huyo kenge mbanike tu umle na ugali
 
Fumigation???.Naona mnaitaja sana lkn Sijui km mnafahamu maana yake?!!!!.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…