Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 37,340
- 56,053
Mpaka tujadiliane; ingawa mi naona haiko sawa, ndio maana nimeleta mada tuijadiliLabda nkuulize kabla sijatoa mawazo yangu, hapo kwako mke wako hua unamruhusu kwenda kila mara akiitwa?
Haya maandiko yanatesa sana wazaziMwanamke ataachana na wazazi wake na ye ataambatana na mumewe
Huu mfumo ndio unatakiwa ubadilikeWe mke wako anaondoka bila ruhusa ?
Mfano akiondoka bila ruhusa au ingali we umemkataza utajisikiaje ?
Tupe uzoefu mkuuAcheni kunyanyasa wanawake sio lazima aombe ruhusa 50/50
Na kama kuna mahusiano mazuri ataombwa mumewe baada ya kusalimiana,kwanza hatabagua kwa kuwaomba wote wamtembelee.Kama mwanaume yuko bize atamruhusu mke wake aende peke na samahani nyingi kwa mkwe.Ni ngumu sana wazazi kuomba binti yao aende kuwasalimia kisha mume ugome kumruhusu, ni ngumu na hiyo hutokea tuu endapo mnakuwa hamna mahusiano mazuri na wakwe zako.
Pia kikawaida kama wazazi wameomba inabidi muende wote, kama mna nafasi. Kama haipo basi anaweza kwenda peke yake.
Na kama wakwe zako watakuwa na busara basi wataongea na mume direct, mume ndiye watampa taarifa kisha yeye ndiyo atamjulisha mkewe.
One man down, requesting air back upAcheni kunyanyasa wanawake sio lazima aombe ruhusa 50/50
KASHAOLEWA YUPO CHINI YA UANGALIZI MWINGINE NA MAMLAKA MENGINE (KAMA AMBAVYO ULIKUBALI KUMUOZESHA)Umepambana kumlea na kumsomesha mtoto wako wa kike, mpaka akafikia hatua fulani ya elimu; iwe cheti, diploma, degree, masters, PhD, au u-profesa.
Baada ya hapo, akaolewa na akawa na mji wake.
Changamoto: Leo hii unataka binti yako aje akusalimie nyumbani; itamlazimu mpaka aombe ruhusa kwa mumewe, na amruhusu, ndio aweze kufika, asiporuhusiwa hatokuja kukujulia hali.
Swali: Hii kwako unaichukuliaje, ukiangalia wewe ndio mzazi, uliyemlea na kumgharamikia elimu; lakini cha ajabu, leo mtu baki ndio anayempangia aje akuone ama asije kukuona?