Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 35,744
- 104,974
- Thread starter
- #21
Unacholalamika ni sawa ila jitahidi sana barua yako ya kuomba kazi pamoja na CV iwe inavutia kwa maana ya kwamba inajieleza vizuri na inakuelezea uwezo wako kiasi kwamba mwajiri akiiona atavutiwa kukuita kwenye interview. ni bora uchelewe kutuma maombi kuliko kutuma maombi ya hovyo halafu mwajiri akakuona wewe ni wa hovyo na huwezi kumsaidia chochote kwenye ofisi yake. barua ya maombi na CV ya mtu inaonyesha namna huyo mtu alivyo hata kabla hujamuita kwenye interview na hicho ndio kitu kinawasumbua sana graduates wengi watanzania. unakuta akiona tu nafasi imetangazwa anakimbilia kuapply kwa kupanic kabla ya kukaa chini na kutafakari ni namna gani atamshawishi mwajiri ili avutiwe kumpa kazi. watu wenye vyeti wapo wengi ila watakaopata kazi mapema ni wale ambao wanajua namna ya kupangilia CV na maombi ya kazi haswa kwenye private sector achilia mbali serikalini ambapo kuna kujuana sana na vimemo vya wakubwa. so kijana jipange andaa CV yako vizuri na andika barua yako vizuri kulingana na vigezo vilivyoandikwa kwenye tangazo la kazi na sio kulipua au kucopy na kupest maombi ya kazi uliowahi kuomba huko nyuma simply kwa sababu post zinafanana!!!!!!wageni wataishia kuchukua kazi zetu watanzania kwa sababu ya kudharau kwetu kwenye kuandaa CV nzuri na maombi mazuri ya kazi!!!!!!
Umeongea ukweli mtupu kaka. Mara nyingi tuna copy and paste, kikubwa tunabadili address na date tu.
Tutalifanyia kazi mkuu.
Ila sasa, unajua mimi naweza andika barua nikaiona iko perfect, je wewe mwajiri/hr ukiisoma itakuvutia? Nashindwa kujua wewe unapenda nini?
Ila umeongea mambo nyeti mkuu. Tutajitahidi kuhakikisha cover letter zinapendeza unaposoma mkuu.