Hii kwa M-Pesa MasterCard Nitaiita LoopHole

Hii kwa M-Pesa MasterCard Nitaiita LoopHole

SuperImpressor

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
1,505
Reaction score
649
Hii kwa M-Pesa MasterCard Nitaiita LoopHole

Kama mnavyojua kampuni ya Vodacom wametuletea huduma nzuri ya kutuwezesha kufanya manunuzi mtandaoni kupitia huduma yao ya M-Pesa Virtual Card ambayo inapatika kupitia USSD *150*00# ambayo ni menu ya Vodacom M-Pesa. Tukumbuke kwamba taarifa za kadi hii zinatakiwa kuwa siri ya mtumiaji tu ili kuiepusha kadi yake kutumiwa na mtu mwingine kufanya miamala. Lakini sasa cha kushangaza ni kwamba hii M-Pesa Mastercard ambayo ni msaada kwetu, iko “UCHI” (NAKED) kwa sababu unapoingia katika menu ya M-Pesa, 4 Lipa kwa M-Pesa, 6 M-Pesa Mastercard, 2 Taarifa za Kadi, utatumiwa taarifa zako za kadi hadi ile CVV bila hata kuombwa namba za siri na hiyo itampa nafasi mtu mbaya kuona taarifa za kadi.

Swali langu ni kwamba hawa jamaa hawajaona kuwa huo ni mwanya unaoweza kumsababishia mteja wao hasara?
 
Nieleweshe hiyo vurnelability ya kuibiwa ni ipi wakati mwishoni kuna kuingiza password au labda sielewi vizuri!?
Hakuna password
Password ipo kwenye kuweka pesa kwenye kadi kutoka m pesa
Note: Weka pesa unapotaka kununua kitu
 
Kama alivyosema jamaa happy just transaction za online hazitumii password ya ATM ana account bank, zinatumia tu namba ya kadi, expire date na ile cvv nyuma ya kadi, vyote vipo wazi tu.
Ok sasa nimekupata
 
Kwa kukushauri tu, hizi credit card usizifanye kuwa ndo sehemu ya kuweka hela. Weka pesa tu unapotaka kufanya malipo au pale unapotumiwa hela kupitia hio card basi uwe na sehemu nyngne ya kuzideposit. Kuna markets nyingi sana zinauza hizo credits card za watu mbalimbali kwenye darkweb. So ili hela yako iwe safe inabidi uweke tu wakati wa kuitumia
 
i strongly agree with you, nina special card kwa ajili ya online purchases na siweki pesa mpaka pale ninapotaka kununua kitu flan tena naweka kiasi kile kile au nazidisha kidogo tu. Sitakuja kuchanganya kadi ya kawaida na ile ninayotumia kwa online purchases
 
Thumbs Up!!!!

That's how it should be.
 
Kwa kukushauri tu, hizi credit card usizifanye kuwa ndo sehemu ya kuweka hela. Weka pesa tu unapotaka kufanya malipo au pale unapotumiwa hela kupitia hio card basi uwe na sehemu nyngne ya kuzideposit. Kuna markets nyingi sana zinauza hizo credits card za watu mbalimbali kwenye darkweb. So ili hela yako iwe safe inabidi uweke tu wakati wa kuitumia
Shida inakuja pale unapokuwa umetumiwa refund na bila kujua au ukachelewa kuiona notification ya money return, mbona mtu mbaya akifanya miamala atafanikiwa kabla hujahamisha hela yako.
 
Shida inakuja pale unapokuwa umetumiwa refund na bila kujua au ukachelewa kuiona notification ya money return, mbona mtu mbaya akifanya miamala atafanikiwa kabla hujahamisha hela yako.
Okay ni kweli unachosema coz kuna siku nlitumiwa refund kwenye MPESA mastercard yangu lkn hata hakuna notification yyt, ni kama bahati tu niliangalia na nkakuta hio refund, mwanzo nlikua najua kwa mpesa mastercard watakua wanatuma notifications kwa sms coz imefanyiwa linking na simu zetu lakin kumbe sivyo

Ila tu cha muhimu ni kwamba mtu asitumie hizo cards kama shm ya kutunza hela, maybe itokee katumiwa bila kujua basi hio itakua ni bahati mbaya tu
 
Nitajie namba ya kadi yako ya bank, cvv na majina yako nikuibie 10000 tu. Nitaweza ikiwa tu kadi yako IPO activated kufanya online purchasing.
Sasa unasubiri nini kuibia watu ata mia tano per day ujilipue ili likibuma uwe angalau umeinjoy na watoto wa dar
 
Si kweli kwamba Card zote za Bank nalipo ya ntandaoni haupaswi ingiza password!
Kwa wale walojiunga kutumia card za CRDB kulipa mitandaoni kinaitwa Mastercard Passcode au Visa Secure Code!

Ambayo kabla haija authorize kukatwa hela lazima uijaze!

Baadhi ya Makampuni yanayotumia hixo Visa na Mastercard services nafikiri wamelipuuza hili swala!
 
Back
Top Bottom